UVCCM Mtafanya nini ikiwa Raisi Hatafanya maamuzi magumu.?

majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
431
179
Hongereni kwa tamko lenu lenye harufu ya uchungu kwa chama chenu ili kiache kukumbatia uovu wakati wananchi wamekiamini na wakakipa dola, ila hamkupaswa kumchafua Mh Dr slaa kwani dhambi zake ni mali yake yeye binafsi na Mungu ndie atakaye Mhukumu na sio sisi binadamu,Dr slaa ameaminiwa na watanzania wengi na amekuwa msatari wa mbele kutetea hata hicho ambacho leo nyie mnapinga kisisambaratishe chama chenu. Ameungwa mkono na zaidi ya watu 2000000 pamoja na uchakachuzi wa tume.

"Je nyie UVCCM Ikiwa JK atakaa kimya katika mambo mliyoyataja katika tamko lenu Mpo tayari Kumtunisia?"

Kama Hamko tayari kumtunisia Tamko lenu halina Maana yeyote.
 
Wanakula na kulipwa kodi za wananchi toka TRA na sasa watapewa pesa za Dowans. Ubinafsi mkubwa wanao UVCCM. Watanzania gani hao? Hivi Tunawatoa wapi Watanzania wa Namna Hii?
 
Hongereni kwa tamko lenu lenye harufu ya uchungu kwa chama chenu ili kiache kukumbatia uovu wakati wananchi wamekiamini na wakakipa dola, ila hamkupaswa kumchafua Mh Dr slaa kwani dhambi zake ni mali yake yeye binafsi na Mungu ndie atakaye Mhukumu na sio sisi binadamu,Dr slaa ameaminiwa na watanzania wengi na amekuwa msatari wa mbele kutetea hata hicho ambacho leo nyie mnapinga kisisambaratishe chama chenu. Ameungwa mkono na zaidi ya watu 2000000 pamoja na uchakachuzi wa tume.

"Je nyie UVCCM Ikiwa JK atakaa kimya katika mambo mliyoyataja katika tamko lenu Mpo tayari Kumtunisia?"

Kama Hamko tayari kumtunisia Tamko lenu halina Maana yeyote.

Mkuu,mimi jana niliweka jamvini hapa maneno yangu kuwa Uvccm ni genge la wahuni,wanaotokwa mate mdomoni,kutafuta kujipendekeza,na kuachiwa madaraka..tena hawana Vision na huko tuendako.tena hawasomi alama za nyakati.wasifikiri ccm inanafasi mioyoni mwa watz.labda mafisadi wenzao ,wevi.ambao hata hivyo katiba mpya tuitakayo itaziba mianya yote ya ulaji wao..
 
mbona huo walaka wao wameuandika kwa lugha wazimu, haina tofauti na mipasho ya tuarab.
 
"Je nyie UVCCM Ikiwa JK atakaa kimya katika mambo mliyoyataja katika tamko lenu Mpo tayari Kumtunisia?"

Kama Hamko tayari kumtunisia Tamko lenu halina Maana yeyote.

Nadhani tuwape muda tuone watachukua hatua gani. Lakini sidhani kama wana hatua yoyote ya kuchukua kwa chama na serikali yao kama serikali itailipa Dowans.
 
Angalau wamefurukuta wandugu, tuwape "benefit of doubt" kwa sasa!

Ni ful usanii..wenye Hekima tulishaona..labda sana sana,wamekosa nidham, wanatakiwa waombe radhi ccm kubwa..kwamba sikio limezidi kichwa hivy wamekuwa sungura...zaidi hapo ni utumbo.
 
nimesikitishwa sana na tamko la uvccm

limekosa lugha sawia, utashi, mlolongo na adabu kwa wote... Hivi hawa vijana hawana washauri ndani ya chama??? hawana walezi?
 
hilo tamko lina maana kubwa katika kupambana na ccm iliyochafuka, ila wasiwasi wangu tamko limetolewa bure, na hakuna hatua zozote wanazoweza kuchukua ilikuudhihirishia uma kwamba yanayoendelea ndani ya ccm yamewachosha kikweli.

huenda wameandika kwa ushawishi wa RA na lengo ni kuwachafua wapambanaji wa ukweli Dr slaa,Mzee6 na mwakyembe.
 
hawa wametumwa na Ridhwani, UVCCM ya kweli inayowakilisha mawazo yetu wana CCM ni le ya musoma. Hawa ni mbwa koko yaani ukisikiliza utaona kabisa hawa mapandikizi ndio kama ccm kata na wale wa musoma ndio hasw national leaders. Kwa tabia hii ya hawa wakina shigela hiyo february watapigwa viboko. Watoto wetu wa mkoa wa mara kama mlivyowaona juzi hawataki mchezo, hawana unafiki, hawahitaji kupewa hela wala ahadi na wakina RA na Makamba ili kukitetea chama chao. Hawahitaji ruhusu kukitetea chama kilichoanzishwa na muasisi aliyetoka mkoani kwao. Acha hawa waendelee ku dance kwenye tune za wakina JK na genge lake la majambazi wanaotutawala kwa mabavu. Chama hiki kimekufa na vijana badala ya kuki rescue wanafanya upumbavu. Ngoja tuwasikie Bavicha wakijibu hawa hawana hoja mambo ya upadri wa Slaa yanawahusu nini?
 
Ni ful usanii..wenye Hekima tulishaona..labda sana sana,wamekosa nidham, wanatakiwa waombe radhi ccm kubwa..kwamba sikio limezidi kichwa hivy wamekuwa sungura...zaidi hapo ni utumbo.

Contradiction ndani ya society huwa zinaleta maendeleo wandugu, hizo heshima za woga hazitufikishi popote! Mimi ninachosubiri ni next move ndiyo itakayotoa mwelekeo wa tamko lao!
 
hapana jamani let us call a spade , wameonyesha njia. Tunaichukia CCM kwa mabaya yake hivyo wakifanya jambo zuri japo dogo tuna sababu za kuwaunga mkono...
 
umenena mkubwa,sijash2shwa na tamko lao,ila waliolopoka ndo wenyeshda

Ni ngumu kushtushwa au kuipokea kauli yao kwa uzito kwa sasa

Hivi huyu mwenyekiti anaekaimu ndo anahusishwa na nini tena vile? Mmmh, credibility na public image yake tata sana kunifanya kuamini matamko anayotoa

Ila vilevile hawa si ndo Riz nasikia mshauri wao (though nahisi kwa mlango wa uwani)....hivi inawezekana kutoa tamko pembeni ya mshauri...yaani namaanisha hivi mshauri wao kweli alipitia na kuu-approve? Naona utata mtupu na nataka kuamini it some kind ya chenga za kisiasa katika kunogesha mchezo

Anyway, let us give them time...tutaona na kama wako kimsimamo wa maslahi ya taifa zaidi, hongera zao and keep it up
 
Hongereni kwa tamko lenu lenye harufu ya uchungu kwa chama chenu ili kiache kukumbatia uovu wakati wananchi wamekiamini na wakakipa dola, ila hamkupaswa kumchafua Mh Dr slaa kwani dhambi zake ni mali yake yeye binafsi na Mungu ndie atakaye Mhukumu na sio sisi binadamu,Dr slaa ameaminiwa na watanzania wengi na amekuwa msatari wa mbele kutetea hata hicho ambacho leo nyie mnapinga kisisambaratishe chama chenu. Ameungwa mkono na zaidi ya watu 2000000 pamoja na uchakachuzi wa tume.

"Je nyie UVCCM Ikiwa JK atakaa kimya katika mambo mliyoyataja katika tamko lenu Mpo tayari Kumtunisia?"

Kama Hamko tayari kumtunisia Tamko lenu halina Maana yeyote.

Kama kweli wanamaanisha wayasemayo basi msemo wa wahenga unakaribia kutimia "Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha"!

Hatuwezi kuridhika na kauli zao tu, kwani watanzania tumezoea kusikia kauli tamu tamu kutoka kwa viongozi wa juu wa ccm lakini tabu ni utekelezaji!

Yetu macho na kumbukeni "Njia ya mwongo ni fupi"

jamani, hubu tuwape muda maana wamesema kabisa kwamba mwenyekiti wao JK asipotekeleza ndani ya siku 5 hayo waiyomtaka kuyafanya, ikiwa ni pamoja na "Kuchukua Maamuzi Magumu" - sina hakika wanamaanisha nini, kwamba wataandamana kwenda kuwatoa kwa nguvu wale wote waliowaita wazembe. Sijui hawaogopi Risasi za moto za Mwema na vijana wake!!
 
wanabwabwaja tu hao UVCCM besides wote wanalipwa mishahara na maposho kwa pesa za ufisadi za mafisadi who controls the presidency
 
Back
Top Bottom