UVCCM mjirekebishe vinginevyo mtazidi kusugua benchi

diranqhe

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
1,268
2,000
UVCCM mnatakiwa kubadili mitazamo yenu.

Ndugu zangu nawasalimu.

Leo tena nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni. Leo nitaongelea kuhusu Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na kushauri machache.

Toka uteuzi wa wakuu wa wilaya utangazwe siku chache zilizopita kumekuwa na maneno ya kebehi kwa wanachama wa UVCCM. Hili ni jambo la kusikitisha na kukemewa kwenye jamii ya wastaarabu. Watu mitandaoni wamekuwa wakidai kwamba wanachama wengi halisi wa UVCCM kwa maana ya wale waliokulia kwenye chama wanakosa sifa za uteuzi kwa nafasi mbalimbali hali inayopelekea mamlaka ya uteuzi kuteua waliohamia toka upinzani au wale wanaUVCCM wasio na haiba ya ukada kindakindaki.

Mimi napinga hii hoja kwasababu mtu anapojiunga na CCM tayari anakuwa na sifa sawa na mwanachama mwingine aliyekuwepo miaka mingi iliyopita. Na anastahili kuteuliwa au kugombea nafasi yoyote ya uongozi. CCM haina ubaguzi. Isitoshe kwa Tanzania kiongozi wa ngazi ya kwanza kuanzia chini ni mjumbe wa nyumba kumi kumi. Ukitaka kufungua akaunti benki lazima utaanzia kwa mjumbe ambao karibu ni makada wa CCM. Kwahiyo utaona watanzania wote wana angalau kaharufu ka uanaCCM.

Pamoja na utetezi wangu dhidi ya wanaokosoa uteuzi bado kuna mambo ambayo hayavutii kabisa kwa UVCCM. Huu umoja wa vijana umezidi kupoteza mvuto siku za hivi karibuni. Vijana ni kama wamekosa ajenda inayowaongoza. Vijana wengi wamedhani kuvaa nguo za kijani na njano na kujipendekeza kwa viongozi kutafanikisha mipango yao ya kupata ulaji. Matokeo yake tumeona watu ambao hawajawahi kuonekana na shati la kijani wakiteuliwa. Vijana wa CCM lazima mbadilike na mjifunze kujenga hoja zenye mvuto kwa wananchi. Zinazoakisi uhalisia wa maisha yao. Sio kukurupuka na kutaka kufurahisha viongozi wa chama na serikali ambao kwa sasa wameonyesha kabisa wako makini na mambo ya kusifiana ovyo.

Kwa mfano sasa hivi kumetokea baadhi ya vijana wa CCM wakitamka hadharani kwamba wananchi hawataki katiba mpya bali maendeleo. Nikataka kujua kwanini vijana wanasema hivyo ila kukawa hakuna point. Hivi mwananchi gani asiyetaka kuona katiba inamzuia DC au RC kumuweka ndani mtuhumiwa kwa saa 48? Mwananchi gani asiyetaka kuona mamlaka ya DPP yanafanyiwa mabadiliko? Ni mwananchi gani asiyependa kuona katiba hairuhusu vilaza kuingia bungeni?

Mwananchi gani asiyetaka kuona haki za mtoto wa kike kwenye elimu zinalindwa?... Hawa vijana wana akili kumzidi Mwalimu Nyerere aliyeona mapungufu ya katiba na kutamka hadharani kwamba kwa katiba hii Rais akiamua kuwa dikteta anaweza? Tumesikia mtoto kachomwa moto wakati wa kuhamisha wananchi hifadhini lakini cha kushangaza UVCCM wako kimya.

Vijana wa CCM someni alama za nyakati na mwende sawa na mahitaji ya wananchi kisiasa kwa sasa. Pia muhimu sana mwende sawa na mamlaka za teuzi. Hii mamlaka ya sasa hivi inaonekana haingalii sana kama ni kada. Inaangalia mtanzania mwenye sifa zinazohitajika. Msipobadilika msishangae kina Malisa GJ, Yericko Nyerere na Bavicha wengine wakiteuliwa.
 
Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,547
2,000
Umesema "Mamlaka ya Uteuzi inaangalia Mtanzania mwenye Sifa" sawa.

Je, ni sifa zipi hizo zinazozingatiwa au kuhitajika ambazo waliopata Uteuzi wanazo kuzidi hao UVCCM wengine waliobaki?
 
diranqhe

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
1,268
2,000
Umesema "Mamlaka ya Uteuzi inaangalia Mtanzania mwenye Sifa" sawa..,
Je, ni sifa zipi hizo zinazozingatiwa au kuhitajika ambazo waliopata Uteuzi wanazo kuzidi Watanzania wengine waliobaki?
Sifa ya kwanza ni kutoandika comment ya kijinga kama hii yako.
 
Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,547
2,000
Sifa ya kwanza ni kutoandika comment ya kijinga kama hii yako.
Kwa "Mjuvi" yeyote anaelewa kuwa hata kwenye "Ujinga" kuna la kujifunza.

Hivyo kutokuwa kwenye kundi hilo la "Wajuvi" ndio mana umekosa la kujifunza na siwezi kukulaumu kwa hilo kwa kuwa sio kosa lako!
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,609
2,000
Sifa ya kwanza ni kutoandika comment ya kijinga kama hii yako.

Mkuu kwenye post yako namba moja kuna mahali umesema uvccm imepoteza mvuto, kimsingi sio uvccm tu, bali ni ccm kwa ujumla, ndio maana unaona matumizi ya vyombo vya dola yanazidi kuwa makubwa siku hadi siku. Ufahamu ccm sio chama cha kizazi hiki, bali ni cha kizazi kilichopita, hivyo vijana wengi hawavutiwi kujiunga nacho. Na wale wanaojiunga nacho ni wale wenye uwezo mdogo sehemu nyingine.

Hivyo ccm kuchagua wahamiaji ama watu wenye mvuto nje ya ccm, ni ili kulazimisha ccm kupata mvuto. Hiyo ccm kwa sasa ni kama mwanamke mzee ambaye hakubaliani na umri wake, utaona analazimisha kupakaa vipodozi vikali ili kupata ujana lakini uso unagoma.
 
VON BISMACK

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
1,096
2,000
Ulianza vizuri mwishoni umepuyanga sana!

Toa hoja na suluhisho lake sio kuandika umajawa hisia hasi kwa upande mmoja.
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,778
2,000
UVCCM mnatakiwa kubadili mitazamo yenu.

Ndugu zangu nawasalimu.

Leo tena nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni. Leo nitaongelea kuhusu Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na kushauri machache.

Toka uteuzi wa wakuu wa wilaya utangazwe siku chache zilizopita kumekuwa na maneno ya kebehi kwa wanachama wa UVCCM. Hili ni jambo la kusikitisha na kukemewa kwenye jamii ya wastaarabu. Watu mitandaoni wamekuwa wakidai kwamba wanachama wengi halisi wa UVCCM kwa maana ya wale waliokulia kwenye chama wanakosa sifa za uteuzi kwa nafasi mbalimbali hali inayopelekea mamlaka ya uteuzi kuteua waliohamia toka upinzani au wale wanaUVCCM wasio na haiba ya ukada kindakindaki. Mimi napinga hii hoja kwasababu mtu anapojiunga na CCM tayari anakuwa na sifa sawa na mwanachama mwingine aliyekuwepo miaka mingi iliyopita. Na anastahili kuteuliwa au kugombea nafasi yoyote ya uongozi. CCM haina ubaguzi. Isitoshe kwa Tanzania kiongozi wa ngazi ya kwanza kuanzia chini ni mjumbe wa nyumba kumi kumi. Ukitaka kufungua akaunti benki lazima utaanzia kwa mjumbe ambao karibu ni makada wa CCM. Kwahiyo utaona watanzania wote wana angalau kaharufu ka uanaCCM.

Pamoja na utetezi wangu dhidi ya wanaokosoa uteuzi bado kuna mambo ambayo hayavutii kabisa kwa UVCCM. Huu umoja wa vijana umezidi kupoteza mvuto siku za hivi karibuni. Vijana ni kama wamekosa ajenda inayowaongoza. Vijana wengi wamedhani kuvaa nguo za kijani na njano na kujipendekeza kwa viongozi kutafanikisha mipango yao ya kupata ulaji. Matokeo yake tumeona watu ambao hawajawahi kuonekana na shati la kijani wakiteuliwa. Vijana wa CCM lazima mbadilike na mjifunze kujenga hoja zenye mvuto kwa wananchi. Zinazoakisi uhalisia wa maisha yao. Sio kukurupuka na kutaka kufurahisha viongozi wa chama na serikali ambao kwa sasa wameonyesha kabisa wako makini na mambo ya kusifiana ovyo.

Kwa mfano sasa hivi kumetokea baadhi ya vijana wa CCM wakitamka hadharani kwamba wananchi hawataki katiba mpya bali maendeleo. Nikataka kujua kwanini vijana wanasema hivyo ila kukawa hakuna point. Hivi mwananchi gani asiyetaka kuona katiba inamzuia DC au RC kumuweka ndani mtuhumiwa kwa saa 48? Mwananchi gani asiyetaka kuona mamlaka ya DPP yanafanyiwa mabadiliko? Ni mwananchi gani asiyependa kuona katiba hairuhusu vilaza kuingia bungeni? Mwananchi gani asiyetaka kuona haki za mtoto wa kike kwenye elimu zinalindwa?... Hawa vijana wana akili kumzidi Mwalimu Nyerere aliyeona mapungufu ya katiba na kutamka hadharani kwamba kwa katiba hii Rais akiamua kuwa dikteta anaweza?.... tumesikia mtoto kachomwa moto wakati wa kuhamisha wananchi hifadhini lakini cha kushangaza UVCCM wako kimya.

Vijana wa CCM someni alama za nyakati na mwende sawa na mahitaji ya wananchi kisiasa kwa sasa. Pia muhimu sana mwende sawa na mamlaka za teuzi. Hii mamlaka ya sasa hivi inaonekana haingalii sana kama ni kada. Inaangalia mtanzania mwenye sifa zinazohitajika. Msipobadilika msishangae kina Malisa GJ, Yericko Nyerere na Bavicha wengine wakiteuliwa.
Mara nyingi sana wale vijana wanaoongea kuhusu katiba kwamba katiba mpya haina muhimu hawajui maana ya katiba. Kwenye katiba Bora ndiyo kunamaendeleo jumuishi na shirikishi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom