UVCCM kwafukuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM kwafukuta

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, May 17, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  HOFU ya kung'oana madarakani imegubika mkutano wa baraza kuu la ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) unaofanyika kesho, huku mwenyekiti wake, Hamad Yusuph Masauni, ambaye anadaiwa kuwa alighushi umri, akibeza tuhuma hizo kuwa ni za kipuuzi.

  Masauni alichaguliwa kushika wadhifa huo Desemba, 2008 katika uchaguzi uliokuwa umejaa utata na kusababisha mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kuamua mgombea atoke Zanzibar. Awali wagombea walikuwa Hussein Bashe na Benno Malisa kutoka Bara.

  UVCCM leo inafanya mkutano wa kamati ya utekelezaji pamoja na semina wakati kesho kutakuwa na mkutano wa baraza kuu, ambao pia utahudhuriwa na Kikwete. Vikao vyote vinafanyika mjini Iringa.

  Hofu ya kung'oana ilionekana dhahiri jana wakati zaidi ya wajumbe 60 kutoka Zanzibar walipokuwa wakiondoka jijini Dar es salaam kuelekea Iringa, wakiimba nyimbo za kumsifu Masauni na kubeza wanaofanya mipango ya kumuengua.

  Hata hivyo, vyanzo vingine vya habari vilifafanua kwamba tayari baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar wameandaa maazimio ambayo yanalenga kumng'oa mmoja wa vigogo wa UVCCM kutoka visiwani humo.

  Kwa mujibu wa maazimio hayo, wajumbe hao wanataka kigogo huyo aachie ngazi kutokana na kushindwa kusimamia umoja wa vijana visiwani humo na kusababisha shughuli mbalimbali kuzorota.

  Awali, habari zilizosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari zilidai kuwa Masauni ameghushi umri wake na hivyo anatakiwa ajiuzulu.

  Waraka unaosambazwa unadai kuwa kuna cheti kinachoonyesha kuwa alizaliwa Oktoba 3, 1973 wakati fomu zake za kuomba hati mpya ya kusafiria zinaonyesha alizaliwa Oktoba 3,1979. Lakini Masauni alionekana kutotetereshwa na tuhuma hizo.

  "Sijaona huo waraka, lakini naamini ni tuhuma za uongo; zinalenga kunipunguzia kasi yangu ya utendaji katika usimamizi wa rasilimali za umoja, maadili na uwajibikaji," alisema Masauni alipohojiwa na Mwananchi kuhusu waraka huo.

  "Labda kuna watu walifikiri wangeweza kuniburuza katika nafasi yangu, lakini sitaacha kusimamia rasilimali za umoja wetu; umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na uwajibikaji."

  Kiongozi huyo mkuu wa UVCCM alitamba kwamba umoja huo ni imara na ataendelea kusimamia vema matumizi bora ya rasilimali za chama, maadili na uwajibikaji bila kujali watu wanaotaka kumpunguza kasi.

  Lakini alipoulizwa kuhusu umri wake halisi, Masauni hakutaka kuwa bayana. "Nilikupa nafasi hiyo ya kuzungumza (na mimi) kwa kifupi kwa sababu ya heshima.

  Hapa nipo na watu wengine katika gari nitakuwa nawasumbua. Hizo tuhuma nazisikia tu sijaziona ila naamini hazina msingi," alijibu.

  Ingawa hakufafanua tuhuma hizo, Masauni aligusia mchakato wa kumpata mwenyekiti wa jumuiya hiyo, akisema kuwa ulifuata taratibu zote na hivyo tuhuma zinazoibuliwa sasa zina lengo la kuvunjia heshima vikao vya umoja na chama.

  "Nilichaguliwa kwa vikao halali, kabla ya hapo watu waliangalia rekodi zetu. Waliangalia mambo ya uadilifu na yote ya msingi... katika mambo yote haya vikao vya chama na hata vyombo vya usalama vilishiriki, sasa sijui watu wanachosema," alilalamika.

  Mkuu huyo wa jumuiya hiyo kongwe alisema lengo lake kuu ni kuunganisha vijana, kuleta umoja na kuwajengea uwezo wa kimaendeleo. "Kamwe sitakubali kuona vijana wanagawanyika; lengo ni kuona wanakuwa kitu kimoja, amani, mshikamano na utulivu. Haya ni malengo yangu makuu katika uongozi wa UVCCM," alisisitiza.

  Masauni anatarajiwa kumaliza muda wake wa kikatiba ifikapo 2012. Alipoulizwa kama chama chake kimepokea tuhuma hizo dhidi ya Masauni, katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alijibu:, "Hilo ni jambo dogo tu haliwezi kumega UVCCM wala kusumbua chama.

  "Kama ni tuhuma zitachunguzwa tu na kubainika ukweli au uongo wake... huwezi kusema zinaweza kumega umoja, hilo ni jambo dogo tu mbona!" alibeza Makamba.

  Makamba aliongeza:"Kwa sababu tuhuma hizo nimezisikia na kuziona kama ambavyo naamini na wewe (mwandishi) umeziona, jambo la msingi ni kusubiri vikao vya UVCCM vikae na kuleta ukweli."

  Aliweka bayana kwamba UVCCM ni taasisi huru ambayo ina vikao vyake vya maamuzi ambavyo ni pamoja na baraza kuu na kamati ya utekelezaji.

  Mtendaji huyo mkuu wa chama alisema vikao hivyo vya maamuzi vinaweza kulifanyia kazi suala hilo na kupata ufumbuzi wake wa kina bila chama kuingilia kati.
   
 2. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wajamani hili la vyombo vya Usalama vina wajibu gani katika hili la mchakato wa Uchaguzi wa UVVCCM?
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  CCM wanatumia pesa za wanachama wao ambazo zinaweza kujumuishwa kama public fund ukiongeza na pesa za ruzuku kwa hiyo unaweza kuona kuwa hao ni kuana national interrest. Si CCM pekee yao hata CHADEMA na vyama vingine, ndio maana Chacha wangwe alikuwa anataka Mkaguzi mkuu wa fedha za serikali awe na mamlaka ya kuangalia mahesabu ya vyama vya siasa.

  Kwa hiyo basi vyombo vya Usalama wanapaswa kuangalia mwenendo mzima wa chaguzi ndani ya vyama (kama wangekuwa neutral), kuforge cheti ni kosa la jinai na anayeweza kuthibisha kama kosa lilitendeka au laa ni mahakama, lakini nani wa kupeleka mahakamani ni Public Prosecutor, kutoa Takrima na rushwa na habari zisizo za kweli zote zinaangukia kwenye public interrest kwa hiyo vyombo vya dola vinapaswa kuwa na interrest ya kujua what is going on ndani ya vyama vya siasa, kwani ndivyo vinavyounda dola vikishinda uchaguzi.
   
 4. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hii la kufoji cheti kwa nchi kama Tanzania ni jambo la kawaida wala wanaolifuatilia ni kupoteza muda wao fuatilia mambo mengine. Hivi tukianza kufuatiliana nani atabaki? Acha watu waponde maisha, maisha yenyewe ni mafupi.
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  nashangaa sana kama kweli huyu mwenyekiti wa umoja wa vijana ndugu masauni ,kama ni kweli amefoji cheti cha kuzaliwa atakuwa amekiabisha chama chake.....kama amezaliwa mwaka 1973....na kusema ni amezaliwa mwaka 1979 .....atakuwa ame risk sana ukizingatia kwa zanzibar mji ulivyo habari huenea sana...

  ila ni vema bwana masauni apewe benefit of doubt....kama angeweza kuanika cheti chake mbele ya waandishi wa habari kudhibitisha kuwa amezaliwa mwaka 1979 na sio mwaka 1973 basi atakuwa amewashinda wabaya wake ambao pia inasemekana ni siasa za kupakana matope za kuwania uwakilishi wa kikwajuni vile vile..ndio maana moja ya kashfa pia ni kuwa hajajiandikisha kwenye daftari la kupiga kura zanzibar na daftari la mzazibar mkaazi..........nadhani yeye masauni get chance to prove people wrong or to let himself sink with this!!!
   
 6. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha kuwa hata CHADEMA na CUFna vyenginewe wakifanya uchaguzi Usalama wa Taifa unapitia kuthibitisha sifa za waombaji?. Kwa mujibu wa Masauni jina lake lilifanyiwa uchunguzi na vyombo vya usalama wa Taifa na hivyo Mnyika kwa mfano itabidi jina lake liwasilishwe Usalama wa Taifa ili lifanyiwe uchunguzi?

  Kuhusu huduma za serikali kuwa lazima zitolewe kwa vyama vya siasa, sasa chama kisicho na wabunge na kwa vile rzuku inatolewa kwa mujibu wa uwakilishi wa wabunge, jee hawa pia wanapata huduma hiyo ya usalama wa Taifa? Halafu nashangaa kuwa kunatokea vitendo vya kuvunja katiba za vyama ndani ya vyama sijasikia serikali ikiingilia kati hadi pale mtu binafsi anapoamuwa kulishtaki tendo kwenye vyombo vya sheria.
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Katika haya yote mi halistaajabishi jambo kwani langu muhimu ni kuwa je wanaufanyia nini UMOJA WA VIJANA CCM tanzania na nini mtazamo wao na kauli mbiu yao? that is my point to them na sio wawe wanafki kila kukicha wanakuwa watumwa kwa viongozi walioko ngazi za juu na kuhongwa sana na wanashindwa kujua lipi wafanye kwa maendeleo ya UVCCM.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Usichukulie mazoea kuwa sheria kosa ni kosa time is not an excuse.
   
 9. M

  Madevu Member

  #9
  May 20, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni aibu tupu...
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  masauni keshazoea siasa za kufoji za kwao zanzibar anashinda mwengine anatangazwa mwengine, ila safari hii amenowa na kama watakuwa hivi hivi hata kwa uteuzi wa wakilishi kule zanzibar mambo yatakuwa mazuri akina mwakilishi shihata aliefoji cheti cha form four na yeye ajiandae kuumbuka au asigombee
   
Loading...