UVCCM: Kutoka tanuru la kuzalisha fikra mpya hadi kuwa kiwanda cha kuzalisha vyeo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Hapo ndipo UVCCM ilipofikia imekuwa kama taasisi ya watafuta vyeo wanaotumia mbinu mbadala mbali na elimu. Ninaikumbuka UVCCM ile enzi za akina Sendeka na baadaye Nchimbi na Uhalula kabla Nape naye hajaingia na cheche zake, vijana walishindana kifikra na si " kujipendekeza". Taabu ilianzia pale wazee walipoivamia taasisi na kujiita wadhamini na makamanda wa vijana na kuanza kuitumia jumuiya kama ngazi ya kujipatia madaraka ya " juu" na hapa ndipo vijana walipolewa kabisa. Niwashauri tu UVCCM ambao mko uchaguzini kwa sasa, JITAMBUENI na muikomboe jumuiya yenu ambayo kwa sasa ni kama imetekwanyara na watu fulani fulani ulojo, kuweni makini. Nawatakia uchaguzi mwema!!
 
Hata hiyo unayoisema tayari ilishaoza na tayari walikuwa na mitandao iliyoanza 1995, kumbuka ugomvi wa Nchimbi na Uhalula hadi Nchimbi akahamishiwa BUnda kuwa Mkuu wa Wilaya.

TYL ndiyo ilikuwa na watu unaowasema na kama hujui historia basi angalia vijana wa TYL ndiyo akina Generali Ulimwengu.
 
Fikra bila cheo zafaa nini kwenye siasa?
Au hujui kuwa tuliwahi kusalimiana "zidumu fikra za mwenyekiti? " siyo zidumu fikra kutoka tanuru la fikra?
Siasa ni cheo, hizo fikra ni nyenzo za kufanya siasa. Maana ukiwa na cheo fikra ziro, siasa itakutema!
 
Back
Top Bottom