UVCCM Kigoma Wakimbia na Michango ya Fund rising

Kitwasi

New Member
Feb 24, 2019
2
45
Katika hali ya kushangaza Umoja wa Vijana mkoa wa kigoma wamejikuta katika lawama na kupasuka pasuka hayo yalitokea katika kikao cha baraza la vijana wa uvccm mkoa wa kigoma kinachojumuisha wajumbe wote wa mkoa wa kigoma ambapo kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Vijana mKoa wa kigoma Ndugu Silvia Sigula ambapo kilipata baraka za wageni kama Mjumbe wa Wazazi ndugu Felix Ntibenda, Mnec kutoka mkoa wa Kigoma ndugu Ngenda, mbunge wa vijana kutokea kigoma Mh katimba na wengine wenyeji.

Kikao hicho kilichohusisha uchaguzi wa wajumbe wa Kamati ya utekelezaji uccm kigoma na kumchagua mhamasa wa mkoa kilifanya pia fund rising ambapo wajumbe wote waliahidi na wengine kutoa pesa taslimu lakini hadi sasa Mwenyekiti amekimbia na michango hiyo kwani hajawahi kuizungumzia katika vikao vyote vya kamati ya utekelezaji mkoa na kwa sasa Hajulikani alipo kwani hata ofisini hapatikani.

Gazeti hili ilipo jaribu kuongea na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Ndugu Steven alisema kuwa "Mwenyekiti hajaitisha kikao chochote cha kamati ya utekelezaji pia yeye hajui alipo"
Katibu wa uvccm ndugu Adamu alipoulizwa alisema kuwa yeye kwa sasa amehamishiwa kuwa katibu wa vijana mkoa wa mtwara hivyo mambo ya kigoma hayajui kwani tayari ashakabidhi ofisi Pia gazeti letu lilimtafuta Mbaraza wa vijana Taifa ndugu Moses hakupatikana kwa simu lakini kada mmoja ambaye hakutaka kutaja Jina alisema kuwa Moses ambaye ni mtumishi wa wilaya ya Uvinza upande wa elimu amesimamishwa kazi kutokana na kuhusika katika tuhuma za kura rushwa kutoka kwa wafugaji wa mapori ya uvinza kiasi cha mil 68 za kitanzania hivo amesimamishwa kazi hadi uchunguzi umalizike.

Pia gazeti hili lilimtafuta Mbunge wa Vijana Mh Katimba kuhusu kujibu ahadi zake kwa wajumbe wa baraza kuhusu milioni saba alizoahidi hadi sasa hajatoa alisema "Ile ni ahadi hivyo itatekelezwa tu" .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom