UVCCM Kagera watoa vifaa kwa ajili ya mapambano ya Covid-19

manyonga

Member
Oct 3, 2012
44
21
_*UVCCM KAGERA WAUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA CORONA*_

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Ndg.HAPPINESS RUNYOGOTE pamoja na wajumbe wa Baraza kuu mkoa wa Kagera leo tarehe 21/05/2020 wameunga mkono juhudi za Mh Rais katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) kwa kugawa vifaa kama ndoo, sabuni, sticker na barakoa kwa wilaya zake zote nane.

Wilaya ya Ngara na Kyerwa imepewa vifaa vya kutosha kwa sababu zipo mpakani kadhalika wilaya ya Muleba imepewa vifaa ili vipelekwe visiwani katika kata zake zote.

Umoja wa Vijana mkoa wa Kagera umesisitiza wananchi wazidi kuzingatia na kutekeleza matakwa yote yaliyoelekezwa na wizara ya afya.

Viongozi wa chama Ndg.Michael Chonya, Katibu CCM (M), Ndg. Hamimu Mahamoud katibu mwenezi wa CCM (M) na Ndg.Julius Peter Nansongelea katibu CCM(W)-BK Manispaa walihudhuria katika tukio hilo la ugawaji wa vifaa.

Imeandaliwa:
SAMIDU KAJUMULO
Katibu Uhamasishaji mkoa wa-KAGERA.
 

Attachments

  • IMG-20200521-WA0027.jpg
    IMG-20200521-WA0027.jpg
    69.5 KB · Views: 1
  • IMG-20200521-WA0028.jpg
    IMG-20200521-WA0028.jpg
    78.8 KB · Views: 1
  • IMG-20200521-WA0022.jpg
    IMG-20200521-WA0022.jpg
    73.1 KB · Views: 1
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom