Mizizi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,275
- 391
Nimeshangaa kusikia, Makamo mwenyekiti UVCCM bara Beno Malisa na Yule wa Zanzibar Jamal Ally, kufika Arusha na kutaka kufanya kazi za umoja huo bila uongozi wa huko kufahamu na kupewa taarifa. Hata hivyo, zoezi la viongozi hao kutaka kufungua matawi ya Umoja huo huko Arusha ulikwama baada ya viongozi wa maeneo hayo akiwemo Mwenyekiti wa wilaya ya A. mjini kukataa kutambua shughuli hiyo
Kama kweli hawa ndio viongozi wanaondaliwa kutuongoza hapo baadaye basi Tanzania bado tuna safari ndefu sana.
Huyu kijana Malisa huwa anapenda kufanya vitu anavyofikiria yeye na maslahi ya kundi analolisupport bila kujali maslahi ya vijana anaowaongoza!
Kwenye kipindi hiki cha uongozi wake tumeshuhudia UVCCM ikiwa kwenye mgawanyiko mkubwa sana, kila kijana kwenye umoja huo ni kama anamamlaka yake mwenyewe, kila kijana ni msemaji wa umoja huo, na kila kijana ana mtazamo wake na msimamo wake.
Hakuna tena ile spirit ya Youth League, hakuna tena mshikamano, hakuna tena nidhamu. Vijana wamegawika kwenye makundi ya wasaka madaraka, wakiwemo viongozi wenyewe.
Hii ni UVCCM ya Malisa