UVCCM Dar wazindua kampeni ya kurudisha majimbo yaliyochukuliwa na upinzani

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1552919242696.pngUmoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, umezindua kampeni ya ‘Dar es Salaam ya Kijani’ ikiwa na lengo la kurudisha mitaa na majimbo yaliyokwenda upinzani.

Kampeni hiyo inalenga kuweka mikakati kwa kuanzia ngazi za jumuiya zote za mkoa huo, kuanza kujipanga kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa kampeni hiyo itachochea ustawi zaidi wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuzidi kukita mizizi katika ngazi zote kuanzia mkoa hadi majimbo, wilaya hadi kata, na matawi hadi mitaa.

“Leo tunazindua kampeni yetu ya “Dar es Salaam ya Kijani kuelekea serikali za mitaa 2019”, kampeni kabambe kwa ajili ya kuirejeshea CCM mitaa iliyopotea katika uchaguzi uliopita ambayo kwayo itatusaidia kupata ushindi mkubwa kimkoa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 wa udiwani, ubunge na urais.

“Sote tu-mashuhuda kwamba katika uchaguzi uliopita wa 2014 wa Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa 2015 tulipoteza baadhi ya mitaa, kata na majimbo yaliyokuwa yakishikiliwa na CCM.

“Na sababu za kupoteza huko zinajulikana, sina haja ya kuzirejea sasa. Hivyo sisi vijana wa CCM tunatambua kuwa ndiyo damu na roho ya chama chetu, na kwamba tunao wajibu wa asili wa kusafisha njia katika kutimiza malengo ya uwepo wa vyama vya siasa kikatiba ya kushika dola,” amesema Kilakala

Mwenyekiti huyo wa UVCCM, amesema kuwa CCM inahitaji ushindi mkubwa kwa kuweka mikakati ya awali kwa kuwahusisha wanachama wa chama hicho wa ngazi zote.

“Kampeni yetu hii itashuka katika wilaya, kata na matawi yote katika Mkoa wetu ili kuwa na ufahamu wa pamoja na kuhakikisha kila Kijana wa UVCCM anawajibika ipasavyo kuhakikisha falsafa ya Dar es Salaam ya kijani yaani Dar es Salaam ya CCM inaenea kwa wanachama na wananchi ili ikifika wakati wa uchaguzi tuvune wapiga kura wa kutosha.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitatoa pongezi zangu za dhati kwa niaba ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais John Magufuli kwa kutuongoza vyema kupitia Serikali yetu ya CCM katika jukumu la kutatua changamoto za watanzania na kuwaletea maendeleo.

“Tumejionea dhahiri shahiri namna yale yaliyochelewa yakiwahishwa, yaliyoshindikana yakiwezekana, magumu yakiwa mepesi, yaliyokwama yakikwamuliwa,”amesema Kilakala

Kwa upande wake mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa UVCCM, Mwal. Raymond Mwangwala, amesema ameridhishwa na kasi kubwa inayofanywa na vijana wa Dar es Salaam ya kuhakikisha chama kinapata heshima katika chaguzi
zote.
 
ni UVCCM au usalama wa CCM maana siku hizi ni ngumu sana kuwatofautisha.
 
UPUUZI MTUPU!

View attachment 1048369

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, umezindua kampeni ya ‘Dar es Salaam ya Kijani’ ikiwa na lengo la kurudisha mitaa na majimbo yaliyokwenda upinzani.

Kampeni hiyo inalenga kuweka mikakati kwa kuanzia ngazi za jumuiya zote za mkoa huo, kuanza kujipanga kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa kampeni hiyo itachochea ustawi zaidi wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuzidi kukita mizizi katika ngazi zote kuanzia mkoa hadi majimbo, wilaya hadi kata, na matawi hadi mitaa.

“Leo tunazindua kampeni yetu ya “Dar es Salaam ya Kijani kuelekea serikali za mitaa 2019”, kampeni kabambe kwa ajili ya kuirejeshea CCM mitaa iliyopotea katika uchaguzi uliopita ambayo kwayo itatusaidia kupata ushindi mkubwa kimkoa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 wa udiwani, ubunge na urais.

“Sote tu-mashuhuda kwamba katika uchaguzi uliopita wa 2014 wa Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa 2015 tulipoteza baadhi ya mitaa, kata na majimbo yaliyokuwa yakishikiliwa na CCM.

“Na sababu za kupoteza huko zinajulikana, sina haja ya kuzirejea sasa. Hivyo sisi vijana wa CCM tunatambua kuwa ndiyo damu na roho ya chama chetu, na kwamba tunao wajibu wa asili wa kusafisha njia katika kutimiza malengo ya uwepo wa vyama vya siasa kikatiba ya kushika dola,” amesema Kilakala

Mwenyekiti huyo wa UVCCM, amesema kuwa CCM inahitaji ushindi mkubwa kwa kuweka mikakati ya awali kwa kuwahusisha wanachama wa chama hicho wa ngazi zote.

“Kampeni yetu hii itashuka katika wilaya, kata na matawi yote katika Mkoa wetu ili kuwa na ufahamu wa pamoja na kuhakikisha kila Kijana wa UVCCM anawajibika ipasavyo kuhakikisha falsafa ya Dar es Salaam ya kijani yaani Dar es Salaam ya CCM inaenea kwa wanachama na wananchi ili ikifika wakati wa uchaguzi tuvune wapiga kura wa kutosha.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitatoa pongezi zangu za dhati kwa niaba ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais John Magufuli kwa kutuongoza vyema kupitia Serikali yetu ya CCM katika jukumu la kutatua changamoto za watanzania na kuwaletea maendeleo.

“Tumejionea dhahiri shahiri namna yale yaliyochelewa yakiwahishwa, yaliyoshindikana yakiwezekana, magumu yakiwa mepesi, yaliyokwama yakikwamuliwa,”amesema Kilakala

Kwa upande wake mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa UVCCM, Mwal. Raymond Mwangwala, amesema ameridhishwa na kasi kubwa inayofanywa na vijana wa Dar es Salaam ya kuhakikisha chama kinapata heshima katika chaguzi zote.
 
Mambo ndio yaamenza ila munajiamini sana utadhani taifa nilakwenu ngoja tuone hilo picha linavyokwenda
 
Back
Top Bottom