fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,644
2,000
Habari!

Niliandika uzi kuwa mbunge wa Kawe ana nia ya kugombea Urais 2025. Na kwa mujibu wa mifumo ya CCM 2025 ni zamu yako tena Mh. Samia Suluhu kugombea Urais.

Huyu Gwajima mtu mwenye nguvu na mjanja sana, kavipiga vita vingi na kushinda. Usipojifunga kiume umdhibiti mapema huyu Askofu Gwajima atakuharibia njia na kukimegamega chama chenu nasi wapinzani tutashangilia maana huwenda tukapata mpenyo.
Gwajima afukuzwe ccm mara moja!
 

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
9,933
2,000
Dodoma. Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema

Source: Mwananchi
Kweli nimeamini CCM kuna mazezeta,yaani serioualy wanataka wananchi wapigwe a kill shot.Unspeakable.Now I can see a war between the unvaccinated and vaccinated.Wananchu tunasema no to the shot,the Nuremberg Code ambayo Tanzania ni signatory inatulinda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom