Huyu jamaa ana undugu na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Arusha ndipo akahamishwa na Samia?

Naona sura kama ya mtu mmoja hivi
 

NUKUU ZA KATIBU MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) NDUGU. KENANI LABAN KIHONGOSI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO 27/07/2021

"Tunapenda kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama chetu Kwa namna ambavyo ameendelea Kufanya Kazi bila kuchoka na kuendelea kulinda Amani ya Nchi yetu, na sisi Vijana tupo pamoja naye kuhakikisha adhma ya serikali ya Awamu ya 6 inaenda kutimia"

"Lakini jambo lingine sisi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunasimama na Rais Wetu na Serikali yetu, Watanzania msirubunike, nendeni Kwa hiari yenu mkapate Chanjo. Rais ndiye raia namba moja na hawezi kuliongoza Taifa Kwenye mambo yasiyofaa"

"Sambamba na Hilo sisi Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunasimama na viongozi Wetu wa Serikali kwani Maendeleo tunayoyapigania ni Kwa manufaa ya Watanzania wote kwa hiyo wale wote wanaopinga Maendeleo yanayofanywa waache mara Moja"

"Sisi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kauli zile tunazilaani na tunazipinga vikali Maana kama utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge ana hoja Kuna party cocus ambazo zipo peleka hoja zako kwenye vikao, na anaposema anayesisitiza kuhusu Chanjo atakufa ajue yeye sio Mungu"

"Tunaomba Chama kiwachukulie hatua Kali na waache mara Moja kuropoka"

"Niwaombe Watanzania twendeni tukapate Chanjo Kwa hiari yetu Huku tukiendelea Kufanya mazoezi ili Taifa letu lipate kuwa na watu wenye Nguvu Kwa Maendeleo ya Taifa letu"

"Tunapomuongelea Rais tunamuongelea Raia namba moja kwenye nchi hii ambaye Mungu ametupa, kama huwezi kumheshimu kama Mzazi basi mheshimu Kwa mamlaka yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

"Kuna jambo pia naomba niliseme, Juzi Kuna viongozi wameongea kuhusu Chanjo, Mbunge wa Kawe Gwajima ameongea maneno yasiyofaa kuhusu Chanjo ya Corona na Chanjo imeshaletwa, Sasa anapotokea Kiongozi wa mhimili mwingine anaenda kuwahubiria Waumini na kuwatisha watu kuwa wanaosapoti watakufa sasa Tumweleze kuwa anayetoa Uhai ni Mungu na anayechukua Uhai ni Mungu"

"Tunapenda kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama chetu Kwa namna ambavyo ameendelea Kufanya Kazi bila kuchoka na kuendelea kulinda Amani ya Nchi yetu, na sisi Vijana tupo pamoja naye kuhakikisha adhma ya serikali ya Awamu ya 6 inaenda kutimia"

View attachment 1870429

View attachment 1870430

View attachment 1870432

View attachment 1870433

View attachment 1870434

View attachment 1870435

View attachment 1870436

View attachment 1870437
Kila siku mtaishia kulaani tuu. Huo ndio upuuzi wenu Ccm mlio peleka bungeni. Yaani mmesambaratishana. Hamuelewani. Huyu kulia yule kushoto. Na bado..
 
Huyu jamaa ana undugu na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Arusha ndipo akahamishwa na Samia?

Naona sura kama ya mtu mmoja hivi
Alikuwa mwenyekiti uvccm iringa,Magu akamteua kuwa mkuu wa Wilaya Arusha July mwaka Jana,mama akamteua kuwa mkuu wa Wilaya iramba,ndani ya siku chache akafanya mabadiliko na kumuweka kuwa katibu uvccm taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dodoma. Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema

Source: Mwananchi
Gwajima AFUKUZWE CCM....

Wala GWAJIMA hajawahi kuwa na ITIKADI YA CHAMA CHETU.....

MSHENGA huyu ndiye ALIYEMPELEKA LOWASSA CHADEMA kuwa mgombea wa URAIS kwa "kuzoza" na mh.Mbowe.......

Gwajima akiachwa ndani ya CCM atakuja Kusababisha MTAFARUKU MKUBWA......mtakuja tu kuuona panapo uhai!!!!!

#GwajimaAfukuzweCCM
#SiempreCCM
#HastaLaVictoriaSocialistParty
 
Watu wanapenda demokrasia na uhuru wa kutoa maoni lakini hawana hamu na demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Hizi ndizo gharama za demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Halafu hii kitu si ni hiari!? Mbona hivi jamani!? Watanzania ni waelewa wanajua mbivu na mbichi, msiwahukulie ki hivyo!
 
Hayo ni maoni yake na ametumia haki yake kikatiba.......

Kama ambavyo wengine wanatumia haki yao kikatiba kupigia debe chanjo ndivyo ambavyo Gwajima anatumia uhuru huo kupingana na chanjo.....

Mwisho wa siku chanjo ni hiyari ya mtu.......
 
Watu wanapenda demokrasia na uhuru wa kutoa maoni lakini hawana hamu na demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Hizi ndizo gharama za demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Halafu hii kitu si ni hiari!? Mbona hivi jamani!? Watanzania ni waelewa wanajua mbivu na mbichi, msiwahukulie ki hivyo!
Hata nashangaa huo uhuru wanaouhitaji waTanzania ni wa aina gani.......??

Yaani wanaopigania uhuru wa kutoa maoni ndio wa kwanza kupingana na maoni ya wengine wanaotumia uhuru huo huo kutoa maoni yao.....
 
Aliongelea jimboni au kanisani?

Tusichanganye dini na siasa!
Komredi kwani WAZIRI MWENYE DHAMANA akiongea jambo zito la kuleta mtafaruku ndani ya jamii akiwa ndani ya nyumba ya IBADA linachukuliwa kiwepesi.......

Jambo hili si la KISIASA.....

Kama angeamua kulipinga tu kwa hoja zinazoeleweka na kutotoa LAANA YA KUFA MADAKTARI wetu ningemuelewa vyema tu kwani kila mtu ana Uhuru wa kutoa maoni.....

Mh.Gwajima amekwenda mbali mno kwa kusema "waliofanikisha hii chanjo wamenunuliwa na kuhongwa na mabeberu"....

These are serious ALLEGATIONS.....

It's time for him to be taken to the party's AD HOC committee to prove it the allegations.....

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#TujiandaeNaChanjo
 
Back
Top Bottom