UVCCM Busega yaonya jina la Dk. Chegeni kukatwa NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM Busega yaonya jina la Dk. Chegeni kukatwa NEC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145


  [h=2][/h]IJUMAA, SEPTEMBA 21, 2012 06:10 NA MWANDISHI WETU, BUSEGA

  HEKAHEKA za uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeanza kuchukua sura mpya, ambapo Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, kutoa tamko la kuitahadharisha Halmashauri Kuu (NEC), isilogwe ikakata majina ya baadhi ya wagombea akiwamo Dk. Raphael Chegeni.

  Kutokana na hali hiyo, wameitaka NEC itende haki kwa kuteua majina ya wagombea wenye sifa na uwezo mkubwa wa kukijenga chama hicho tawala.

  Walisema iwapo majina hayo likiwamo la Dk. Chegeni yatakatwa, wapo tayari kuchukuwa uamuzi mgumu.

  Akizungumza mjini Nyashimo jana, Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Busega, Samuel Ngofilo, alisema: “UVCCM imebaini kuwapo kwa njama hizo chafu zinazolenga kumchafua Dk. Chegeni ili asipitishwe na NEC kugombea wilaya hii ya Busega.”

  Alisema kuna mbinu chafu zimeanza kufanywa na baadhi ya viongozi wa CCM wilayani humo, akiwamo Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani, anayedaiwa kuandika barua kwenda makao makuu ya CCM Mkoa wa Mwanza, akiomba jina la Dk. Chegeni lisipitishwe na kamati ya siasa, kwa sababu ambazo hazijafahamika.

  Aliwataja wagombea wengine watatu wanaogombea Unec wilayani Busega, kuwa ni pamoja na Amos Onesmo, Kashen Fanuel na Miknes Mahela na nafasi hiyo iliombwa na wana CCM wanne akiwamo Dk. Chegeni, anayedaiwa jina lake kukatwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza.

  “Hapa Busega kuna baadhi ya watu wameanza kutengeneza fitina na njama chafu na kupakana matope. Njama hizi chafu zimelenga kupanga safu za watu wanaowataka wao.

  “Dk. Chegeni ambaye pia ni Kamanda wa Vijana wa Wilaya hii ya Busega, ndiye anayesakamwa na kuundiwa njama hizi mbaya za kutaka asipitishwe kugombea Unec katika wilaya yetu hii ya Busega.

  “Tunachotaka sisi vijana wa Busega NEC itende haki. Isimuonee Dk. Chegeni wala mtu mwingine yeyote mwenye sifa za kiuongozi,” alisema Ngofilo.

  Alisema kwa kutambua uchapakazi, ushawishi na uhodari wa kujenga na kutetea hoja kwa maslahi ya chama na jamii alionao Chegeni, ndiyo sababu kuu kilichowasukuma kumchukulia fomu ya kugombea Unec, hivyo kama NEC itakata jina hilo, wapo tayari kuchukuwa uamuzi mgumu.

  “Hatuwezi kusema kama tutaenda Chadema au la, maana bado mapema mno. Ila tunachotaka chama kisituletee watu wasiokubalika ndani ya chama na kwa wananchi wenyewe,” alisema Ngofilo.

  Aidha, alisema wanategemea wajumbe wa NEC hawatakubali njama hizo chafu zipenye, badala yake watatumia busara na hekima zao kurudisha majina ya wana CCM wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi za kijamii.

  “Kwa mfano, mbunge wetu wa Busega, Dk. Kamani kuna barua kuandika na kuituma kwenda kwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza. Barua hiyo anaomba jina la Dk. Chegeni lisipitishwe kwenda ngazi ya Taifa.

  “Kuna maana gani kumchafua mtu? Mtu anayefanya hivyo anakitakia nini chama chetu?. Tunachotaka ni kujenga chama chetu kwa kuwa na viongozi makini, hodari na imara katika kupigania maendeleo ya chama na wananchi wetu. Tunaisihi NEC ipuuze uzushi wa aina yoyote na ilete majina ya watu wanaokubalika kijamii,” alisema Nyofilo.

  MTANZANIA lilipomtafuta Dk. Kamani, hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mwaka huu kuna kazi CCM - NEC

  Kila mtu anataka NGUVU za kumiliki hiyo NEC kwa kuweka MAJINA ya watu wao... Hii ni sababu ya PRINCE na Mama

  TAMWA kupita bila kupingwa?
   
 3. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,536
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Hawa si ndo walitaka kuuana juzi juzi hapa!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naona hakuna haja ya NEC kukutana tena maana kila mtu alishaamua jina lake lazima lipite. Okoeni fedha, cancel mkutano wa NEC.
   
 5. vicdala55

  vicdala55 JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 958
  Trophy Points: 180
  Siasa za Chama Cha Mapinduzi zimejaa unafiki na fitina zisizo na sababu. siyakatai wala kuyakubali madai ya Mwenyekiti wa UVCCM Busega, ni haki yake kusema kile anachokiona hakiendi vema katika chama. Hata hivyo tuhuma zake zimenishitua kidogo. Ukweli ni kwamba namfahamu vizuri sana Bwana Ngofilo, nimefanya na tunaendelea kufanya nae kazi kwa muda mrefu sana katika kuwasaidia vijana wa Wilaya ya Magu bila kujali vyama vyao vya siasa.(Ikumbukwe Wilaya ya Magu ndio iliyoizaa Wilaya ya Busega) Kilichonishitua ni hatua ya sasa ya Bwana Ngofilo kuwa mtetezi wa Chegeni na kuwaacha hao wagombea wengine. Ninachokijua mimi ni kwamba,yeye ni mmoja kati ya vijana jimbo la busega waliochangia kwa kiwango kikubwa kumfanya Bwana Chegeni ashindwe na Bwana Kamani katika kura za maoni za ubunge wa jimbo la Busega,hilo hata yeye mwenyewe analifahamu. Je wakati huo hakumjua Chegeni kuwa ni mchapa kazi na mtu anaekubalika katika jamii? Haya madai na vitisho anavyotoa sasa uhalali wake ni upi? Ninachokiona ni unafiki na njia ya kujitafutia maslahi binafsi kwa mgongo wa UVCCM! Hii ni tabia ya kuogopwa hasa inapofanywa na kiongozi mwenye hadhi kama yake. Katika uchaguzi wa UVCCM wilaya ya Busega, mwenyekiti huyu alikusanya michango (Ufadhili) kutoka kwa watu wote hao (Chegeni na Kamani) huku akijua watu hao hawaivi chungu kimoja,lakini kwa kuwa alikuwa anatafuta ushindi iwe ni kwa njia halali au haramu,watu hao wawili kwake kwa wakati ho walikuwa wazuri na bila shaka wanakubalika ndani ya jamii (kwa madai yake). Kuna madai kwamba siku ya uchaguzi aliegemea zaidi kwa Chegeni huku Chegeni nae akiegemea zaidi kwa Ngofilo bila shaka kila mmoja kwa maslahi yake. Inawezekana Chegeni akijua anawekeza kwa ajili ya kura za NEC na Ubunge 2015 na Ngofilo nae bila shaka akifukuzia ufadhili zaidi ili ashinde uchaguzi. Kauli na madai yake ya sasa yanaleta harufu ya ukweli huo.. Hii ni hatua mbaya inayoweza kuleta mgawanyiko katika UVCCM na chama kwa ujumla. Hili likitokea, nina hakika hata nafasi yake kama mwenyekiti wa UVCCM Busega haitakuwa salama. Ni vizuri kama kiongozi akatambua kwamba nan wajibu wa kuleta umoja na mshikamano katika chama na sio kujitafutia maslahi binafsi. Siasa za maji taka hazina nafasi hasa kwa kizazi kipya ndani ya CCM kilicho na wajibu wa kuleta mvuto uliopotea ndani ya chama. Yeye ni kiongozi mpya, anaeongoza UVCCM katika wilaya mpya ya Busega, anahitaji kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi mema kwa chama na Tanzania kwa ujumla. Nashawishika kuamini kwamba kauli yake haina baraka za vijana wote wa UVCCM Busega. Ninachokiona ni mwendelezo wa siasa za makundi maslahi katika chama. Kila mmoja anajua madhara ya hilo kwa sasa ndani ya CCM. Naamini hakuomba kuwa kiongozi wa UVCCM Busega ili kueneza dhambi hiyo. Nakumbuka nilimpigia simu kumpongeza baada ya kuwa ametangazwa mshindi, lakini pia nilimwambia uchaguzi umepita, makundi wayavunje na kukijenga chama,huku nikimkumbusha kwamba hakuna rafiki au adui wa kudumu katika siasa. Sina hakika kama alinielewa. Bila shaka kwa madai haya mapya, nitamkumbusha tena. Naamini bado anayo busara ya kujua mema na mabaya.
   
Loading...