Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Arusha. Kamanda wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha,Matias Manga amepinga uamuzi wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) mkoani Arusha kumfukuza kwa tuhuma za usaliti.
Akizungumza na mwananchi leo jijini hapa,Manga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Wilaya ya Arumeru, amesema aliteuliwa kuwa kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya Arusha na siyo mkoa.
"Nimesikia taarifa za kuondolewa lakini mimi nataka utaratibu ufuatwa, sikuteuliwa na mkoa na sijawahi kupokea malalamiko ya kukiuka taratibu za cham,” amesema Manga.
Amesema hadi sasa anachokifahamu, yeye bado ni Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arusha na ataendelea kufanya kazi za kusaidia umoja huo wa vijana.
Mapema wiki iliyopita Mwenyekiti wa Umoja UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya alitangaza katika mkutano na waandishi wa habari kumfukuza Manga kwa madai ya kutumia uwezo wake kifedha kuwagawa vijana wa CCM kwa malengo binafsi na kukidhohofisha chama.