Smartboy
JF-Expert Member
- Nov 12, 2010
- 1,110
- 128
Wanajf niko Hapa Monduli, nimekutana na msafara wa magari, costa na Hiace zimejaza vijana wa ccm na bendera zimefungwa kwenye magari, ndo nikauliza kuna nini leo? Wenyeji wameniambia vijana wanaenda Arusha town kuzindua matawi baadae kuna mkutano wa hadhara, nasikia vijana wamesombwa kutoka Babati, karatu, Manyara na maeneo mengine ya Arusha kwena mjini kuhudhuria mkutano.
Sasa mimi nacho jiuliza kwanini Uvccm inawasomba vijana kutoka kila kona kufanikisha ufunguzi wa matawi Arusha mjini, au wanataka kuwaonyesha watanzania kwamba bado ccm inapendwa na vijana. Ama kweli ccm maji shingoni.