UVCCM Arusha hapatoshi!

Smartboy

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,110
128
Wanajf niko Hapa Monduli, nimekutana na msafara wa magari, costa na Hiace zimejaza vijana wa ccm na bendera zimefungwa kwenye magari, ndo nikauliza kuna nini leo? Wenyeji wameniambia vijana wanaenda Arusha town kuzindua matawi baadae kuna mkutano wa hadhara, nasikia vijana wamesombwa kutoka Babati, karatu, Manyara na maeneo mengine ya Arusha kwena mjini kuhudhuria mkutano.
Sasa mimi nacho jiuliza kwanini Uvccm inawasomba vijana kutoka kila kona kufanikisha ufunguzi wa matawi Arusha mjini, au wanataka kuwaonyesha watanzania kwamba bado ccm inapendwa na vijana. Ama kweli ccm maji shingoni.
 
Tena wawe macho, vinginevyo watashughulikiwa na akina Mong'oo wa Arusha!..Wasilete uporipori wao mjini bana!
 
Wanajf niko Hapa Monduli, nimekutana na msafara wa magari, costa na Hiace zimejaza vijana wa ccm na bendera zimefungwa kwenye magari, ndo nikauliza kuna nini leo? Wenyeji wameniambia vijana wanaenda Arusha town kuzindua matawi baadae kuna mkutano wa hadhara, nasikia vijana wamesombwa kutoka Babati, karatu, Manyara na maeneo mengine ya Arusha kwena mjini kuhudhuria mkutano.
Sasa mimi nacho jiuliza kwanini Uvccm inawasomba vijana kutoka kila kona kufanikisha ufunguzi wa matawi Arusha mjini, au wanataka kuwaonyesha watanzania kwamba bado ccm inapendwa na vijana. Ama kweli ccm maji shingoni.
CDM wanashauriwa kwenda vijijini ili wapate nguvu halafu wewe unakuja kuuliza swali la kipumbavu kama hili badala ya kujifunza na wanayo fanya CCM.
 
CDM wanashauriwa kwenda vijijini ili wapate nguvu halafu wewe unakuja kuuliza swali la kipumbavu kama hili badala ya kujifunza na wanayo fanya CCM.

haa haa! Omr tuliza boli kijana hawa watabalika as time goes.
 
CDM wanashauriwa kwenda vijijini ili wapate nguvu halafu wewe unakuja kuuliza swali la kipumbavu kama hili badala ya kujifunza na wanayo fanya CCM.

Kaka sasa naanza kuamini vita hii tutashinda tu. Asante kwa kusoma katikati ya mistari ndugu yangu...
 
Narudi town ngoja nikawachek hawa wa kutoka mapori wanavyo tumiwa.
 
kweli ccm imechoka miaka hamsini ya utawala wao wanafikiria kukitambulisha chama mjini?
wakati chadema inaingia vijijini baada ya kumaliza kazi mjini ndani ya miaka kama saba hivi ccm ndo wanaamka?
tunawakaribisha sana a town kwa wajanja.
 
CDM wanashauriwa kwenda vijijini ili wapate nguvu halafu wewe unakuja kuuliza swali la kipumbavu kama hili badala ya kujifunza na wanayo fanya CCM.
Duh!! Kaka taratibu! Inaonekana wewe ni mwelevu sanaee!? Ila naskitika welevu wako haukufanyi kuwa mwelevu ktk upumbavu unaoujibu! Heshima ya ukimya ni kubwa kuliko heshima ya uropokaji!!
 
hapo furaha kwa watoto wa mji kuletewa totoz mpya kutoka kijiji... Baada ya wiki mbili watachoma hizo t-shirt za ofa
 
Wanajf niko Hapa Monduli, nimekutana na msafara wa magari, costa na Hiace zimejaza vijana wa ccm na bendera zimefungwa kwenye magari, ndo nikauliza kuna nini leo? Wenyeji wameniambia vijana wanaenda Arusha town kuzindua matawi baadae kuna mkutano wa hadhara, nasikia vijana wamesombwa kutoka Babati, karatu, Manyara na maeneo mengine ya Arusha kwena mjini kuhudhuria mkutano.
Sasa mimi nacho jiuliza kwanini Uvccm inawasomba vijana kutoka kila kona kufanikisha ufunguzi wa matawi Arusha mjini, au wanataka kuwaonyesha watanzania kwamba bado ccm inapendwa na vijana. Ama kweli ccm maji shingoni.

vijana na allowance bana.
 
Mjini watamkusanya nani tena? ccm ishapoteza mvuto kwny miji.
 
Wanajf niko Hapa Monduli, nimekutana na msafara wa magari, costa na Hiace zimejaza vijana wa ccm na bendera zimefungwa kwenye magari, ndo nikauliza kuna nini leo? Wenyeji wameniambia vijana wanaenda Arusha town kuzindua matawi baadae kuna mkutano wa hadhara, nasikia vijana wamesombwa kutoka Babati, karatu, Manyara na maeneo mengine ya Arusha kwena mjini kuhudhuria mkutano.
Sasa mimi nacho jiuliza kwanini Uvccm inawasomba vijana kutoka kila kona kufanikisha ufunguzi wa matawi Arusha mjini, au wanataka kuwaonyesha watanzania kwamba bado ccm inapendwa na vijana. Ama kweli ccm maji shingoni.

Waache kwasababu kwa sasa hiyo ndiyo njia pekee ya kujiingizia kipato.
 
Mussa Juma, Arusha.

MAKUNDI ya vigogo wanaowania urais mwaka 2015, ndani ya CCM yamezidi kuugawa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), baada ya Kaimu Mwenyekiti wake, Beno Malisa na viongozi wengine wa kitaifa kujikuta wakikwama kufungua matawi ya umoja huo mjini hapa jana.

Malisa aliyekuwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Jamal Ally, mbunge wa vijana CCM, Catherine Magige pamoja na vigogo kadhaa wa umoja huo, jana walikuwa wazindue matawi 16 ya vijana katika Manispaa ya Arusha, lakini uongozi wa UVCCM wilaya ukagoma.

Viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Godfrey Mwalusamba walipinga ujio wa ghafla wa vigogo hao na kufanya kazi ya kuzindua matawi huku uongozi wa umoja huo wilaya ukiwa hauna taarifa.

Mwalusamba pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya hiyo, walitoa uamuzi huo katika kikao kilichozua malumbano ambacho kilifanyika juzi, ofisi ya UVCCM Mkoa.

Jana, Mwalusamba alithibitisha kupinga kazi ya ufunguaji matawi hayo ya UVCCM kwa maelezo kwamba, walikuwa hawana taarifa za kazi hiyo.

"Wanasema mimi natumiwa na kundi moja la wanaogombea urais, hapana labda wao ndio wanatumiwa, itakuwaje wafike hadi wilayani kwangu na kufanya kazi kwenye kata, bila taarifa hata hizo kata hawana taarifa,"alisema Mwalusamba.Kazi ya uzinduzi wa matawi hayo, ulikuwa umepangwa kufanyika katika Kata za Sokone One,Sombetini, Kaloleni, Sekei na Elerai, lakini haikufanyika licha ya kuwa tayari mabango na baadhi ya vijana walikuwa wamejiandaa.

Kauli ya UVCCM Mkoa Arusha
Mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, Ally Benanga ambaye ni mmoja wa waliokuwa waandalizi wa kazi ya ufunguaji wa matawi, alituhumu baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Arusha kutumiwa kukihujumu chama.

"Hawa ni wasaliti, tulikuwa tayari tumewaandaa vijana, tumetengeneza mabango sasa wamegomea, tunajua wanatumiwa na kundi moja la urais na Chadema kudhoofisha CCM Arusha,"alisema Benanga.

Hata hivyo, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Abdul Mpokwa alipotakiwa kuelezea mtafaruku huo, licha ya kukiri kuahirisha zoezi hilo, lakini alikataa kufafanua zaidi chanzo chake.

"Ni kweli leo (jana) tulikuwa na kazi hiyo ila tumeahirisha na tutaifanya siku nyingine, "alisema Mpokwa.

Katibu huyo, hata hivyo, alikataa kuelezea ni hatua zipi watachukuliwa viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha ambao waligomea zoezi hilo kwa maelezo kuwa walikuwa hawana taarifa.

"Naomba uwasiliane na Katibu wa Mkoa Mary Chatanda yeye ndiye msemaji wetu katika chama,"alisema Mpokwa.

Malisa akana kutumiwa na makundi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jioni, Malisa alikiri kuahirishwa jana kufanyika kazi ya uzinduzi wa matawi hayo kwa kile kilichoelezwa siyo siku nzuri.

Hata hivyo, alisema taarifa alizopewa na mkoa ni kuwa kazi hiyo itafanyika leo huku akikanusha kutumiwa na makundi. "Sidhani hapa kuna makundi, ufunguzi wa matawi ni kuimarisha chama na madai kuwa wilaya haina taarifa sisi haituhusu kwani uongozi wa Taifa unawasiliana na Mkoa,"alisema Malisa.

Tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu, CCM Mkoa wa Arusha kimekuwa katika vurugu kubwa za makundi ambayo yanadaiwa kusababisha kuangushwa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Arusha, Dk. Batilda Burian.
Source: Mwananchi 10/10/2011
 
Waache kwasababu kwa sasa hiyo ndiyo njia pekee ya kujiingizia kipato.

haa haaa! Duh mwita hata wewe umekili sio mchezo. Vijana wameshapewa Tshirt baadae wanapewa msosi na buku ten ten siku inakuwa imesonga
 
Mpwa una busara ya ajabu sana, jibu lako au comment yako imekaa vizuri sana, Thank you
Kaka sasa naanza kuamini vita hii tutashinda tu. Asante kwa kusoma katikati ya mistari ndugu yangu...
 
Hivi ccm kwanini wanapenda kujidanganya, sasa unatoa vijana Monduli kuja kufungua tawi Sombetini Arusha mjini. Hii inamaana gani? Hawa vijana wanatoa tafsiri gani kuwepo kwao hapo, naona hapa wanawahadaa wakazi wa Arusha kwamba bado ccm inashine. Na hizi rasilimali fedha za kutawanya hivi wanazitowa wapi, manake kwa misafara ya magari kutoka maeneo tofauti posho za hawa vijana nk leo tu wanaweza kuteketeza pesa nyingi, ila kwa vile wanazo ngoja wazitumie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom