UVCCM acheni kulalamika, ni matokeo ya tamaa zenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM acheni kulalamika, ni matokeo ya tamaa zenu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Oct 25, 2012.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kwanza niseme wazi mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa na hiyo haininyimi haki ya kuchangia mijadala inayoendelea.

  Uchaguzi wa UVCCM kama ilivyo chaguzi nyingi naamini umefanyika kwa kupiga kura, kwa maana ya kwamba kila mjumbe alipewa karatasi na kalamu (aghalabu naamini hivyo) na kupewa nafasi ya usiri wa kupiga kura.

  Sasa basi kama hilo ndilo lililofanyika, napata wasiwasi na watu wanaolalamika kuwa viongozi waliochaguliwa wamechaguliwa kwa rushwa.

  Swali la msingi ni je, kura zilipigwa kwa kunyoosha mikono ili wale waliopewa rushwa waone aibu kwa fedha walizokula na wapige kura kumchagua aliye wahonga? Kama sivyo hivyo, je wakati wa kupiga kura kuna mtu alimsimamia kila mpiga kura ili kuona anampigia kura aliyemhonga? Swali lingine ni je chumba cha mkutano kilikuwa na mitambo maalumu ya kung'amua nani amemchagua nani? Kama mambo haya matatu hayajitokeza na kama kijana amepewa rushwa na yeye kwa UJINGA na TAMAA zake akampigia kura yule aliyempa rushwa then HAMPASWI kulalamika.

  Binafsi, naona utamaduni wa rushwa katika chaguzi hasa za CCM umezoeleka, ipi njia nzuri ya kuwakomoa watoa rushwa? Moja ni Kuwa na wagombea imara wasafi kimaadili na kwa usafi wao wafanyike mvuto kwa wapiga kura, hiyo ni hatua ya kwanza swali je UVCCM kuna msafi kimaadili? Hatua ya pili, kwa kuwa utamaduni wa kupokea rushwa umezoeleka na ni kama vile hauwezi kudhibitika katika chaguzi za CCM, then ni kuunda mifumo mizuri ya usiri mkubwa katika kupiga kura na Mwisho ni kutompigia kura yule aliyekupa rushwa.....kwa kumchagua yule aliyemsafi kimaadili. Kamwe hakuna atakayetamani kutoa rushwa na hakuna atakayekuja kukudai rushwa aliyokupa!

  Hoja yangu hii imejikita katika ukweli kwamba kupokea rushwa ktk chaguzi za CCM imekuwa ni kawaida, na kwa kuwa mikakati ya kuzuia watu kupokea rushwa pia haipo au imeshindikanika kutekelezeka basi tudeal na MAAMUZI ya mpokea rushwa.

  Mimi kama mtaalamu wa kuandaa mikakati mingi ,naamini kuwa kuna ngazi (levels) nyingi za kutatua tatizo na kama ngazi moja ikishindikana ( kama kukemea na kauli za viongozi au uwajibishwaji ulivyoshindwa), na watu wameshindwa kuacha kutoa na kupokea rushwa..ni wakati sasa wa kuangalia ngazi ya watu kufanya maamuzi wakati wa kupiga kura ili mtu asichague kwa kusukumwa na vijisenti alivyopewa au alivyoahidiwa....

  Mwisho nasema, kwa kuwa usiri wa kupiga kura ulikuwapo (ninavyoamini) na bado mtu akapiga kura kwa kusukumwa na nguvu ya rushwa...then vijana msilalamike kwa kushwa tamaa zentu zimewafanya mshindwe kukataa kupokea rushwa na mmeshindwa hata kutompigia kura aliyetoa rushwa mlipopewa nafasi ya usiri kufanya hivyo!

  Njaa na tamaa zenu
  Mawazo na akili yenu
  Mkiwa wenyewe sehemu
  mkapiga kura zenu
  Chagua wezi wenzenu

  Mwalalamika nini?

  Mnatangaza uasi kumtishia nani?
  Hakumbuki baba ridhiwani
  Wagonjwa kuweka rehani
  Alipotamka hadharani
  Madaktari ondokeni?

  Nanyi basi ondokeni...
   
 2. Van persie

  Van persie JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 917
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 60
  Mi nakuunga mkono mleta mada. Ila mi naomba kuuliza hivi hao magamba vijana wameamua rasmi kuvaa gwanda?. Mbona wanapenda sn kuiga?. Maana ukiwaangalia mpaka inatia kinyaa. Walitukana gwanda la cdm, kumbe wanalitaman.Angalia walivyokuwa dodoma.
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hata hao wanaolalamika wa kambi ya makonda pia walipokea rushwa toka kwa riz one, ni upumbavu tu vijana kutumiwa namna hiyo, UVCCM ni tanuru la kuivisha wala rushwa wakubwa wa siku zijazo
   
 4. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Once you find Symptoms of CCMonia sicjness, immediately swallow CHADEMAquine tablets you will be cured. CHADEMAquine tablets are available all over the Country. If illness persist consult Dr. Slaa. Do not wast you time do it now!
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Seriously??!
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa wamelia sana, ngoja arobaini ipite.
   
 7. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Wap................................mbavu sana hao,waacha wakione cha moto!Magamba yana wenyewe!
   
Loading...