Uvamizi wa viwanja vya wazi na viwanja vya makaburi Manispaa ya Moshi Mjini

DIWANI 2015

Member
Dec 26, 2014
67
12
Mh Rais.

Kumekuwa na uvamizi mkubwa ma maeneo ya wazi public area ndani ya manispaa ya Moshi Mjini. Mh Rais watu wameuza open space na mbaya Zaidi wameuza mpaka viwanja vya makaburi na hakuna wakulisemea hilo.

Mh. rais makaburi ya National housing wameuza kwa mfanyabiashara ajulikanae kama boi safi akajenga bar inaitwa kili home kwa upande wa polisi cotter na upande wa arusha road wameuza kwa mfanyabiashara mngine aliyejenga bar pan africa ya zamani sasa ni hugos na upande wa national housing wameanza kujenga ukuta na inasadikiwa ni mama samweli sita ndio mmiliki mara wengine wanasema mama anna mkapa ndio mmiliki.

Moshi manispaa makaburi yamejaa mpaka manispaa ikaamua kununua kiwanja cha makaburi kifisadi huko moshi vijijini maeneo ya mtakuja kama unaenda kahe au newland.

nimesema wamenunua kifisadi eneo la makaburi heka 15 kwa tsh 102M wakati sio dhamani sahihi ya bei katika eneo hilo.

Mh. Rais dhamani halisi kwa hekari 1 ya shamba la mvua mtakuja ni 1-1.5 milioni kwa namna yoyote dhamani halisi haifiki 15 Milioni lakini manispaa kupitia kodi za wananchi tumepata hasara ya Zaidi ya 87 Milioni ambayo ni kodi ya wananchi wa manispaa ya moshi.

Mh Rais dili hili lilipigwa na watu baada ya baraza kuvunjwa mwaka jana na dili hili lilipigwa na diwani wa korongoni mzee ally mwamba (CHADEMA) Na mkurugenzi uliyemhamisha kabla ya huyu wa sasa.

Mh. Rais sheria inasema diwani au mtumishi haruhusiwi kufanya biashara na manispaa na ikitokea manispaa kupata hasara atahusika na kulipa hasara hiyo kwa mantiki hiyo uyu diwani anastahili kulipa hasara hiyo kwani ndiye aliyepewa kaziya kuwa dalali wakati akijua yeye ni diwani.

Mh. Rais na hawa wafanya biashara walio nunua sehemu ya makaburi ndio wafadhili wa wanasiasa kwenye kampeni akiwemo mmbunge wa moshi mjini sababu inayo pelekea kushindwa hata kumuwajibisha hivyo basi kwa kasi yako ya kutumbua majipu tunaomba uje utusaidie kuyatumbua haiwezekani wauze eneo la makaburi manispaa alafu wakanunue moshi vijijii kwa bei mbaya na pia kutupa adha wananchi ya kusafirisha miili ya wapendwa wetu kwenda kuzika moshi vijijini kwani ni mbali sana na pia dhamani yake ni kubwa sana.

na kwenye kikao cha bajeti juzi nilifanikiwa kuhudhuria kwani kilikuwa kikao cha wazi madiwani walishikia bango lakini waliwaita waandishi baada ya kikao na kuwapooza ili wasiandike habari iyo.

Nikiwa safarini kutoka Moshi

Naomba kuwasilisha
 
Yaani CHADEMA mnaongaza manispaa kwa karibia miaka miaka ishirini lakin linapokuja suala la ubadhilifu eti mnawasukumia CCM.
 
Ungerekebisha heading muungwana awali nili dhani humtakii mema mheshimiwa wetu hiyo taaluma ina wenyewe, watu wamepumzika tena akawatumbue majipu mh?!! inalazimu kusoma habari nzima ndio ieleweke,ila habari inajenghapana shaka.
 
Kumbe hii tabia ya kununua makaburi ni ya huko. Sasa ndio nimeamini, nilisafiri na haoo jamaa kwenye basi moja tukafika sehemu wakayaona makaburi mmoja wao akasema sasa si watuuzie haya maeneo ili tujenge Bar hapo.
Nilishangaa kwa kweli yaani wauziwe makaburi wajenge Bar sikutia neno
 
Na kule mtakuja barabara amna


SIO BARA BARA TUU BALI PIA SIO ENEO RASMI LA MAKABURI WAMEPIGA ZAIDI YA M64 WENYE KUIJUA HELA TUTAYATUMBUA TUU HAYA MAJIPU MAANA HAMNA NAMNA.

BARAZA LILILOPITA PIA MKURUGENZI ALIYE HAMA ALITOA HELA KWENYE KAMPENI ZA CCM 60M BAADA YA KUBANWA WAMEZIRUDISHA KIMYA KIMYA HATA HIZI ZA MAKABURI ZITARUDI HADHARANI
 
SIO BARA BARA TUU BALI PIA SIO ENEO RASMI LA MAKABURI WAMEPIGA ZAIDI YA M64 WENYE KUIJUA HELA TUTAYATUMBUA TUU HAYA MAJIPU MAANA HAMNA NAMNA.

BARAZA LILILOPITA PIA MKURUGENZI ALIYE HAMA ALITOA HELA KWENYE KAMPENI ZA CCM 60M BAADA YA KUBANWA WAMEZIRUDISHA KIMYA KIMYA HATA HIZI ZA MAKABURI ZITARUDI HADHARANI
Mkurugenzi wa manispaa au moshi vijijini?
 
MKURUGENZI KWENYE HILI LA MAKABURI PIA YUPO YEYE MADIWANI WAWILI NA WA TAALAMU WA MANISPAA ANA MAJIPU MAWILI
 
Ila Kili Home pamekaa poa sana! Jamaa amepapangilia vizuri - ila kama ni jipu itabidi patumbuliwe tu, hatuna namna nyingine!!!
 
Ila Kili Home pamekaa poa sana! Jamaa amepapangilia vizuri - ila kama ni jipu itabidi patumbuliwe tu, hatuna namna nyingine!!!


HAHAHAHA NORTHEN HIGH LAND SCHOOL, KILI HOME, MASIKINI NA HUGOS SEHEMU NYETI TUTAZIPOTEZA TUU MAANA HAMNA NAMNA NYINGINE
 
EMBU ANGALIENI HILI. UMEFIWA MOSHI MJINI ITAKUBIDI UKODISHE GARI LA MAITI, SHEHE AU PADRI, WACHIMBA KABURI NA WAOMBOLEZAJI WOTE ZAIDI YA KILOMETA 20 MOSHI VIJIJINI KWENDA KUZIKA KISA ENEO LA MAKABURI KAPEWA MWEKEZAJI WA BAR?
 
Back
Top Bottom