Uvamizi wa viwanja 52 arusha

Mpucha

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
1,203
1,501
Mkurugenzi wa jiji la Arusha amekaririwa hivi karibuni kuwa yupo mbioni kutumbua viwanja 52 ambavyo vimetolewa nje ya utaratibu, na ni maeneo ambayo kwa njia moja ama nyingine yalitakiwa kuwa maeneom ya uma. Hili litaleta faraja, kuna maeneo kama pale soko la kilombero,[ndani ya mwezi mmoja limepigwa fensi ya ukuta haraka haraka], nyuma ya NHC ngarenaro[hapa inasemekana tajiri BAJUTA amenunua, na amejenga nyumba na kuzipangisha haraka haraka] na pale kijenge shule ya msingi ambapo LEOPARD TOURS wamemega eneo la shule na kujenga gorofa, haya maeneo huhitaji kuwa na elimu ya juu kujua kuwa ni maeneo ya uma, sasa sijajua kama haya nayo ni miongoni mwa hayo maeneo 52. Mkurugezi tupia macho na mikataba iliyotanabaishwa uuzwaji wa maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom