Uvamizi wa Marekani uliopora uhuru na ardhi ya Hawaii

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Ungana nami mhabarishaji wako ASIWAJU katika makala hii fupi inayo elezea uvamizi wa marekani katika eneo la HAWAII ulivyo acha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Makala hii imeandaliwa na kuhaririwa na BBC NEWS karibuni muungane nami mwanzo mpaka mwisho wa makala hii.

-----
1.jpg

Mfalme Kalākaua alikuwa mtawala wa kwanza wa kifalme kufanya ziara sehemu mbalimbali duniani.

Disemba 11, kifo cha Abigail Kinoiki Kekaulike Kawānanakoa, anayejulikana kama "binti wa mwisho wa Hawaii", kilitangazwa huko Honolulu.

'Kasri la Iolani - makazi pekee ya kifalme nchini Marekani - ilisema mrithi huyo wa kiti cha enzi alifariki dunia kwa amani akiwa na umri wa miaka 96, akiwekeza karibu nusu ya utajiri wake wa zaidi ya dola milioni 200 kwa taasisi inayounga mkono jamii ya Hawaii.

Kifo cha Kawānanakoa kwa mara nyingine tena kiliibua suala ambalo bado linazua utata katika kisiwa hiki maarufu kwa fukwe zake nzuri: suala hilo ni kupinduliwa kwa ufalme wa Hawaii na wafanyabiashara wa Marekani mnamo mwaka 1893, kitendo ambacho kingesababisha nchi hiyo kukitwaa kisiwa hicho.

Hapa tunakueleza jinsi visiwa hivi vilivyoko katikati ya Bahari ya Pasifiki, kilomita 3,200 kutoka bara la Amerika vilivyoendelea kuwa jimbo la 50 la Marekani, na la mwisho kuingizwa kwenye Muungano, na nini kilitokea kwa familia ya kifalme ya Hawaii iliyotawala hadi wakati huo.

2.jpg

Abigail Kinoiki Kekaulike Kawānanakoa alikuwa mmoja wa warithi wa familia ya kifalme ya Hawaii, iliyofukuzwa na wafanyabiashara wa Marekani karibu miaka 120 iliyopita.

Ufalme wa hawaii​

Visiwa 137 vya volkeno vinavyounda Hawaii vilitawaliwa na koo mbalimbali ndogo hadi mwaka 1810, zilipounganishwa chini ya Kamehameha wa Kwanza, chifu kutoka kisiwa cha Hawaii.

Mfalme Kamehameha -alipobatizwa- alianzisha nasaba ambayo ingetawala kwa miongo sita.

Mnamo 1820, mrithi wake, Kamehameha II, alifungua milango kwa kikundi cha wamisionari kutoka New England, USA, ambao katika miaka michache waliweza kubadilisha idadi kubwa ya watu kuwa Wakristo wa Kiprotestanti.

Wamisionari pia walivutia wawekezaji kutoka nchi yao, ambao walikuwa wakinunua vipande vikubwa vya ardhi huko Hawaii, wakishawishiwa na ripoti za ardhi safi na hali bora ya hali ya hewa ya kilimo cha miwa.

Ushawishi wa wamiliki hawa wa ardhi wa Amerika ulikuwa ukiongezeka.

3.jpg

Kufikia miaka ya 1870, uchumi wa Hawaii ulikuwa unategemea sana biashara yake na Marekani, na wafanyabiashara na wamiliki wa ardhi katika Chama cha Wamisionari walianza kuwa na nguvu zaidi ya kisiasa na kuunda chama chao cha siasa kiliuchoitwa chama cha wamisionari.

Mnamo 1887 wakamlazimisha mtawala wa wakati huo, Mfalme Kalakaua wa Kwanza, kutia saini Katiba mpya ambayo ilitoa tu haki ya kupiga kura kwa wamiliki wa ardhi weupe, tukio linalokumbukwa kama "Katiba ya Bayonet".

Utawala mpya wa urithi​

David Kalakaua, ambaye alikuwa amepata kiti cha enzi kama uzao wa binamu ya Kamehameha wa Kwanza -na baada ya Kamehameha wa tano kufa bila warithi-, alikuwa mwanzilishi wa kile ambacho kingekuwa nasaba ya mwisho kutawala Hawaii.

Katika miaka yake ya awali ya utawala wake, ilibidi akabiliane na ongezeko la shinikizo kutoka kwa Chama cha Wamisionari, ambacho kilitaka kurekebisha mfumo wa kifalme ili kuufanya ufanane zaidi na ule wa Uingereza, ambapo mfalme ni mtu wa kifahari, lakini hana mamlaka yenye nguvu.

Wakati wa utawala wake, Kalakaua alitilia mkazo sana uhusiano wa kimataifa, akiwa mfalme wa kwanza katika historia kuzunguka ulimwengu, mnamo 1881.

Miaka michache baadaye, mnamo 1890, mfalme huyo mwenye umri wa miaka 54 alianza kusumbuliwa na matatizo ya kiafya na, chini ya ushauri wa matibabu, alisafiri tena kwenda San Francisco, Mrekani.
Alifariki katika jiji hilo la Marekani, bila kuacha kizazi chochote.
Kwa hivyo, aliyerithi kiti cha enzi alikuwa dada yake, Liliʻuokalani, ambaye angekuwa mfalme wa mwisho wa Hawaii.

4.jpg

Liliʻuokalani, malkia wa mwisho wa Hawaii.

Mwisho wa utawala wa kifalme Hawaii​

Liliʻuokalani alikuwa amehudumu kama mwakilishi mwaka wa 1881 wakati kaka yake mfalme alipokuwa katika ziara yake ya kimataifa.

Alipoingia madarakani alijaribu kufuta "Katiba ya bayonet" kurejesha haki za kupiga kura za wenyeji, lakini alishutumiwa na raia wake wa kizungu kwa kupindua Katiba.

Mbali na kutafuta mamlaka ya kisiasa, kundi hili lilitaka kumpindua mfalme huyo kwa sababu za kibiashara: Marekani ilikuwa imeamua kuondoa hali ya upendeleo ya sukari ya Hawaii na walitaka Hawaii iingizwe na mamlaka hayo ili wapate manufaa sawa na ya wazalishaji wazawa.

Akihoji kwamba haki za wafanyabiashara wa Marekani na wamiliki wa ardhi zilikuwa zikikiukwa, balozi wa nchi hiyo huko Hawaii, John L. Stevens, aliwaomba wanajeshi wa Marekani walioko visiwani humo kuingilia kati.

Mnamo 1893, Malkia Lili'uokalani aliwekwa chini ya kizuizi nyumbani katika Jumba la Iolani na serikali ya muda iliundwa.

5.jpg

Malkia Liliʻuokalani aliendelee kushikiliwa Hawaii.​

Ingawa Rais wa Marekani Grover Cleveland aliagiza ripoti iliyohitimisha kwamba mapinduzi hayo yalikuwa kinyume cha sheria, Bunge la Marekani liliamuru ripoti nyingine, iliyoitwa ripoti ya Morgan, ambayo mwaka 1894 iligundua kuwa si Balozi Stevens wala wanajeshi wa Marekani waliokuwa na hatia ya kufanya mapinduzi.

Tarehe 4 Julai mwaka huo huo, siku ambayo uhuru wa Marekani unaadhimishwa, serikali ya muda ya Hawaii ilitangaza Jamhuri ya Hawaii huku Sanford Ballard Dole akiwa kiongozi, serikali ambayo ilitambuliwa na Marekani.

Malkia Lili'uokalani aliendelea kuwa chini ya kuizuizi hadi 1896 alipoachiliwa na kuhamia makazi mengine ambapo aliishi maisha duni hadi kifo chake mnamo 1917.

Kama kaka yake, na yeye hakuwa na watoto. Walakini, kufuatia mila, aliwaita warithi wengine wa familia.

Abigail Kinoiki Kekaulike Kawānanakoa, ambaye aliaga dunia Jumapili iliyopita, alikuwa mzao wa mmoja wa warithi hao.

Mnamo mwaka wa 1898, Rais wa Marekani wakati huo William McKinley - kutoka chama cha Republican ambaye alikuwa amemshinda Cleveland - alitia saini kunyakukuliwa kwa Hawaii na kuwa sehemu ya Marekani, licha ya maandamano kutoka kwa upinzani ambao uliona unyakuzi huo mi kinyume cha sheria.

Kitendo hicho kikafungua njia miongo kadhaa baadaye, mnamo 1959, Hawaii ikawa jimbo la hamsini na la mwisho la Marekani, uamuzi ulioegemea kwenye jukumu kuu la visiwa hivyo wakati wa Vita vya pili vya dunia.

6.jpg

Katikati ya Vita Baridi, wakati wa serikali ya Dwight D. Eisenhower, Bunge la Marekani hatimaye liliidhinisha kujiunga kwa Hawaii katika Muungano, uamuzi ambao uliidhinishwa sana na Wahawai wenyewe.

Hata hivyo, baadhi ya wenyeji wameendeleza maandamano yao dhidi ya kile kinachochukuliwa kuwa mojawapo ya mifano kuu ya ukoloni wa Marekani.

Mnamo 1993, miaka 100 baada ya mapinduzi, serikali ya Marekani iliomba radhi rasmi kwa Wahawai kwa kupindua ufalme wao, na kuwanyima haki yao ya kujitawala.

Lakini, ingawa pia walitambua kuwa wenyeji walilazimika kuachia zaidi ya hekta 700,000 za ardhi kwa nguvu, hawakutoa fidia yoyote na hata waliweka wazi kwamba hawatakubali madai yoyote.

Chanzo: BBC
 
Hebu Marekani wanyakue ile nchi ya kusadikika labda kitaingia kizazi chenye akili maana kilichopo hata kujitawala tatizo.
 
Wakiruhusiwa wapige kura kuamua hatima yao wanaweza kuchagua kujitenga na USA ?......kwani hawana wawakilishi kwenye mabunge ya Senate na Congress ?......kwani si wanapiga kura kumchagua Rais wa USA ?

Yoda MALCOM LUMUMBA Kichuguu
Swala la kujitenga wao na Texas wame kuwa wakilipigia kelele kila uchwao.

Kwa hiyo maamuzi ya wao kujitenga ni ya muda mrefu sana.
 
Dah!...nadhani hata hiyo Texas na New Mexico yaliporwa na Marekani kutoka Mexico kwa nguvu.
Kichuguu
Ndio, Muunganiko wa United States of America ndio muunganiko ulio pora maeneo mengi sana kwa nguvu na kwa ulaghai wa kifedha.
 
Ndio, Muunganiko wa United States of America ndio muunganiko ulio pora maeneo mengi sana kwa nguvu na kwa ulaghai wa kifedha.
Ina maana enzi hizo wakubwa walijitanua ki-mabavu sababu dunia ilikuwa ya wenye nguvu tu........ Saddam alijaribu mwaka 1991 ila waliomshambulia ndio hao hao wenye historia ya uvamizi na uporaji ardhi.

Kama Putin kinachompata huko Ukraine baada ya uvamizi na kumega yale majimbo ya Ukraine, Ila wanaompinga hawataki kupoteza maeneo yao waliyoyapora kwa wenyeji zamani.

Hii dunia ni kizunguzungu tu...
dudus Yoda
 
Ina maana enzi hizo wakubwa walijitanua ki-mabavu sababu dunia ilikuwa ya wenye nguvu tu........ Saddam alijaribu mwaka 1991 ila waliomshambulia ndio hao hao wenye historia ya uvamizi na uporaji ardhi...
Ndio hata USSR ilijengwa kwa mabavu same to Roman Empire, Mali Empire n.k haya mambo hayata kwisha kama bado kuna mataifa makubwa na kuna jirani wadogo.
 
Ungana nami mhabarishaji wako ASIWAJU katika makala hii fupi inayo elezea uvamizi wa marekani katika eneo la HAWAII ulivyo acha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo...
Mkuu baada ya ufafanuzi huu mzuri, unaweza na kutuwekea kathread namna waarabu walivyoivamia Africa, tena wakahamia kabisa na wenyeji wa maeneo husika kupotea mazima!
 
Wakiruhusiwa wapige kura kuamua hatima yao wanaweza kuchagua kujitenga na USA ?......kwani hawana wawakilishi kwenye mabunge ya Senate na Congress ?......kwani si wanapiga kura kumchagua Rais wa USA ?

Yoda MALCOM LUMUMBA Kichuguu
Mambo ya kizamani hayawezi kutumiwa katika dunia ya kisasa.

Marekani nzima ilikuwa kama Afrika; yaani ilikuwa imegawanywa kama makoloni ya Uingereza (upande wa Mashariki na kaskazini pamoja na visiwa vya Hawaii), Makoloni ya Uhispania (sehemu ya Kusini, magharibi), na makoloni ya Ufaransa sehemu ya kati, na koloni la Urusi (Alaska) halafu na sehemu zilizokuwa na utawala wa wenyeji (Sehemu za Maaharibi kaskazini).

Baada ya George Washington kuongoza maasi yaliyoondoa utawala wa kiingereza kwenye makoloni ya Virginia, Massachusetts, Rhode Island, Connecticut, New Hampshire, New York, New Jersey, Pennsylvania, Delaware, Maryland, North Carolina, South Carolina, na Georgia makoloni hayo yaliungana na kuwa nchi moja iliyoitwa Muungano wa Nchi za Amerika - United States of America (USA).

George Washington na washirika wake walioongoza maasi yale walikuwa ni waingereza pia ila hawakutaka kuendelea kuwa chini ya himaya ya mfalme na kulipa kodi (TOZO) isiyokuwa na manufaa kwao. Ndiyo maana bendera ya marekani na mistali 13 kuashiria makoloni hayo kumi na tatu yaliyoungana kwanza.

Baada ya hapo, makoloni mengine yalijiunga na muungano huo wa USA ama kwa kununuliwa (makoloni yote ya Ufaransa yalinunuliwa na vile vile Alaska ilinunuliwa kutoka Urusi), ama kwa vita (makoloni yote ya Uhispania yaliungana na USA baada ya kupigana vita na Uhispania) ama kwa hiari (nchi ambazo hazikuwa makoloni kama vile Washington State na majirani zake, zilishawishiwa kujiunga na USA kwa kuahidiwa ulinzi hasa kwa vile massetla waliokuwamo katika maeneo hayo walitaka ulinzi huo).

Swala na Hawaii ambalo lilikuwa Koloni la Uingereza (chini ya indirect rule) ni kama ambavyo majimbo yote ya Marekani yalivyokuwa makoloni ya Ulaya; siyo sawa na swala la Ukraine ambayo ni nchi huru.
 
Mkuu baada ya ufafanuzi huu mzuri, unaweza na kutuwekea kathread namna waarabu walivyoivamia Africa, tena wakahamia kabisa na wenyeji wa maeneo husika kupotea mazima!
Nita jaribu kufuatilia pia hilo nikipata nafasi, nitaweka thread yake.
 
Mambo ya kizamani hayawezi kutumiwa katika dunia ya kisasa.

Marekani nzima ilikuwa kama Afrika; yaani ilikuwa imegawanywa kama makoloni ya Uingereza (upande wa Mashariki na kaskazini pamoja na visiwa vya Hawaii), Makoloni ya Uhispania (sehemu ya Kusini, magharibi), na makoloni ya Ufaransa sehemu ya kati, na koloni la Urusi (Alaska) halafu na sehemu zilizokuwa na utawala wa wenyeji (Sehemu za Maaharibi kaskazini).

Baada ya George Washington kuongoza maasi yaliyoondoa utawala wa kiingereza kwenye makoloni ya Virginia, Massachusetts, Rhode Island, Connecticut, New Hampshire, New York, New Jersey, Pennsylvania, Delaware, Maryland, North Carolina, South Carolina, na Georgia makoloni hayo yaliungana na kuwa nchi moja iliyoitwa Muungano wa Nchi za Amerika - United States of America (USA).

George Washington na washirika wake walioongoza maasi yale walikuwa ni waingereza pia ila hawakutaka kuendelea kuwa chini ya himaya ya mfalme na kulipa kodi (TOZO) isiyokuwa na manufaa kwao. Ndiyo maana bendera ya marekani na mistali 13 kuashiria makoloni hayo kumi na tatu yaliyoungana kwanza.

Baada ya hapo, makoloni mengine yalijiunga na muungano huo wa USA ama kwa kununuliwa (makoloni yote ya Ufaransa yalinunuliwa na vile vile Alaska ilinunuliwa kutoka Urusi), ama kwa vita (makoloni yote ya Uhispania yaliungana na USA baada ya kupigana vita na Uhispania) ama kwa hiari (nchi ambazo hazikuwa makoloni kama vile Washington State na majirani zake, zilishawishiwa kujiunga na USA kwa kuahidiwa ulinzi hasa kwa vile massetla waliokuwamo katika maeneo hayo walitaka ulinzi huo).

Swala na Hawaii ambalo lilikuwa Koloni la Uingereza (chini ya indirect rule) ni kama ambavyo majimbo yote ya Marekani yalivyokuwa makoloni ya Ulaya; siyo sawa na swala la Ukraine ambayo ni nchi huru.
Kitendo walicho fanya marekani kwa HAWAII kilikuwa sahihi ?
 
Hawaii ilikuwa ni koloni la uingereza, haikuwa nchi huru.
Mkuu hujajibu swali kabisa, jibu la swali langu wala hali hitaji maelezo mengi.

Swali: Je kitendo alicho fanya marekani kwa HAWAII kilikuwa sahihi ?
 
Back
Top Bottom