SoC01 Uvamizi wa maeneo ya kilimo unaathiri shughuli za uzalishaji wa mazao

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Habari za jioni wapendwa katika bwana,

Siku leo ningeliomba kugusia maswala yanayohusu kilimo ambapo kama tujuavyo kwamba kilimo ni uti wa mgongo katika kuchochea ongezeko kwa pato la taifa lakini Katika uzalishaji wa mazao ya vyakula na biashara maeneo mbalimbali bado imekuwepo changamoto kubwa sana ya uvamizi wa makazi katika maeneo yenye shughuli za kilimo Jambo ambalo kwa kiasi kikubwa sasa linachochea kupunguza uzalishaji wa mazao katika maeneo mbalimbali.

Na hili linatokana na ufinyu wa ardhi isiyotosheleza matakwa ya raia katika kujikimu na maisha yao ya kila siku.

Na kama tujuavyo kwamba idadi ya watu huongezeka kila siku katika maeneo yetu. Ambapo idadi hiyo pindi iongezekapo huzidi kuchochea uhitaji mkubwa wa ardhi. Ambapo wapo wanaopata ardhi hizo na kufanya shughuli za kilimo pia wengine kulifanya eneo hilo kuwa makazi yao.

Sasa tunaiomba serikali iweze kuchukua hatua za kuthibiti raia wanaoendelea kuvamia ardhi iliyowekwa mahususi kwa kilimo na hatimaye wao kufanya makazi katika maeneo hayo.

Kwa kuwa kama itawekwa sheria na kanuni za mipaka katika maeneo hayo basi kwa kiasi kikubwa tutaweza kuongeza uzalishaji katika nchi yetu na hatimaye tukaweza kuinua uchumi wa nchi yetu.
Asante
 
Back
Top Bottom