Uvamizi wa Eneo Meru na Mahojiano na Aloyce Kimaro (MB)

Kwa mishahara yao tunashindwa kujua nani kakopa nani katukwapulia!
Je,Kimaro akitoa vielelezo kwamba ana 'mkopo' mara kadhaa ya mshahara wake wanaosuspect ni fisadi wataingia wapi?
 
Hii habari imetiwa chumvi pengine kuficha baadhi ya mambo.
Kwa uhakika kabisa Bwana Kimaro shamba lake lina ukubwa wa eka 50 tu si 500 kama baadi ya vyombo vya habari vilivyoripoti.

Nidhahiri kwamba wananchi walikuwa mobilized kuvamia shamba la Bwana kimaro kwa kisingizio cha uhaba wa ardhi lakini kuna ajenda ya siri imeficha hapa,ebu tujiulize wananchi zaidi ya 3000 wanavamia eka 50 na kuziacha eka 1700 zinazomilikiwa na wazungu katika eneo hilo hilo !!!!!!!!!!!!!!!!!!!.wengi wa wavamizi ni vijana tena wasiokuwa na kazi wako tayari kufanya lolote kwa ujira mdogo.

Wameru ni watu ambao wako tayari kufanya hata mambo ya kipuuzi kwa kutumia visingizio vya ajabu ajabu.Wengi mtakumbuka ule mgogoro wa kudai dayosisi ya Meru KKKT ulivyosababisha maafa makubwa hadi Bwana Mrema alipofanikiwa kuuzima.Rais A Hassan Mwinyi alishashindwa kumaliza umwagaji wa damu na ndiyo sababu kubwa ya Bwana mrema kuzawadiwa cheo cha Naibu Waziri Mkuu.
 
To be precise siyo wameru ambao wako tayari kufanya mamboi ya lipuuzi Ndugu Ngongo bali wakazi wa eneo hilo la Singisi ni kama wanapepo. Hata daladala huwa hazisimami pale kupakia wala kushusha abiria. Jamaa wale wake kwa waume ni very violent jamani.
 
Ni aibu kwa Mtanzania wa leo kushabikia uhalifu!

1982,83,... Wasukuma, Wanyamwezi walianzisha sungusungu na walikuwa najichukulia sheria mikononi kama awa jamaa.

Hivyo haya sio mambo ya watanzania wa leo. Tanzania ya zamani ilitegemea magazeti ya uhuru na RTD, hivyo mambo mengine yaliwekwa makapuni.
 
Mheshimiwa Kimaro anasema kuwa yeye shamba hilo alilinunua kihalali kabisa na anadhani kuna mkono wa mtu katika uvamizi wa shamba lake na inawezekana kuhusiana na vita dhidi ya MAFISADI anayoshiriki, ndio inaashiria yeye na mali zake viandamwe!! Kuna hata wanaodhania kuwa EL is behind the instigation of this campaign especially knowing that the MP of the area where the farm is situated is closely related to EL through the marriage of their chidren. It could be far fetched but may merit close scrutiny as to its credibility.
 
vurugu_2.jpg

vurugu_1.jpg
Ni watu wajinga tu wanaojua kuharibu na kuua katika karne hii ya Mtanzania.Kuna njia lukuki kufikia mwisho unao uhitaji, cha hapo juu ni cha kusikitisha.
 
Inaonekana watu wengine wanaandamwa na bahati mbaya; mara mawe yanajitokeza barabarani na kusababisha "kosa kosa" na wananusurika na kabla hawajashusha pumzi mradi wao mkubwa unatekekezwa kama ilikuwa Zimbabwe mbele ya pua za polisi. Sijui what is next.
 
Hata hawa ambao sura zao zimenaswa wakiharibu mali ya Mbunge hawatashughulikiwa. Lakini ole wao wale watakaochoma moto dala dala za EL.
 
How can we forget the ANATOMY OF STUPIDITY ?

Kimaro alielezewa kuwa:
3. Aloyce Kimaro – it baffles many that this semi-illiterate thug can even be a Member of Parliament. It speaks volume to the desperation of CCM to do anything, including recruiting thugs and former thieves, to win back opposition seats.

The biggest comedy in the country at the moment is that this man is mentioned among principled Members of Parliament who can stand up and speak truth to power, including pointing a finger at Mkapa. Well, just few weeks ago he extorted a tender to guide VIPs to climb Mt. Kilimanjaro during the Sullivan Summit by threatening officials at the Ministry of Foreign Affairs that he will blast them in the Parliament. Pure blackmail.

huyo ndie KIMARO mnayemmzungumzia
 
Hapa naona kuna hatari inapikwa. Kwanini ni shamba la Kimaro tu ambalo wananchi hawa wamepatwa uchungu nalo mpaka wakafanya walilofanya? Watu zaidi ya 100 wanaenda kufanya uhalifu bila ya kushawishiwa! Kuna mashamba mangapi Meru yaliyobinafsishwa? Kwanini wananchi waumie na shamba la Kimaro tu?
Bila shaka tumefikia hatua mbaya, na bila shaka kuna watu nyuma ya hili tukio ambao lengo ni kuonyesha 'Unyangumi' wa Kimaro ambao kimsingi haupo, kwani lengo hapa ni kuonyesha kuwa Kimaro amemilikishwa mali za serikali kama BWM alivyomilikishwa Kiwira kinyume cha sheria, hivyo kumuondolea uhalali Kimaro wa kula sahani moja na BMW kuhusiana na mgodi wa Kiwila.
Shime hawa jamaa wasituondoe kwenye ajenda kuu, VITA DHIDI YA UFISADI. Hatuwezi kugeuka wala kufananisha KIWILA na mashamba ya KIMARO kwa tetesi au kwa kigezo cha "WAHALIFU WENYE ASILA KALI" ambao hawafuati sheria wala kuheshimu sheria kama mabwana zao waliowatuma kufanya uhalifu huo.
 
wakati wa kuchoma daladala za EL umefika

hii inaonyesha jinsi gani nchi yetu watu walivyokuwa na vichwa vibovu, wanamshambulia mtu anayewatetea na mwenye nia ya kuinua maisha yao, huku wakimlinda mtu ambae anawafanya wao wanakuwa maskini siku hadi siku......

asante mungu kwa kuweza kunipa uwezo wa kumjua adui wangu ni nani hata kama anatoka kabila moja na mimi
 
Nimezungumza na Kimaro leo na ameelezea mambo fulani muhimu kuyajua. Hii safari ndiyo baaado hata treni kuondoka halijaondoka..
 
Looh! Zimbabwe imehamia Tanzania? Kazi kweli mwaka huu!

Wale wa kwa Ballali mbona walitolewa haraka haraka, hivi huyu mkuu wameamua kumwacha juani peke yake?

Ila tu ushauri kwa wapiganaji wa ufisadi ni muhimu kuwa whiter than white otherwise wajanja watajua pa kukukamata.
 
Looh! Zimbabwe imehamia Tanzania? Kazi kweli mwaka huu!

Wale wa kwa Ballali mbona walitolewa haraka haraka, hivi huyu mkuu wameamua kumwacha juani peke yake?

Ila tu ushauri kwa wapiganaji wa ufisadi ni muhimu kuwa whitter than white otherwise wajanja watajua pa kukukamata.

hapo panakuwa pagumu kidodo maana kama mtu alipata shamba lake kwenye process ile ile iliyompatia mzungu next door halafu yeye ndiyo anavamiwa, utafanya nini kuwa whitier!?
 
Jamani JF we are better than this,
Kwanini tunampa Kimaro ''easy ride''?
Shamba limevamiwa, ni habari ya kusikitisha, na kusikitisha kwa pande zote mbili.
Sisi kama JF nyumbani kwa GT, tunatakiwa kufanya a more systematic aproach kwa hili suala. Tusichague upande.
Tuanze kwa kuangalia,
Kimaro alilipata lini hilo shamba la ekari 500?
Alilipa kiasi gani cha pesa? Alimlipa nani?
Utaratibu gani ulitumika wakati anapewa umiliki wa shamba hilo toka kwa settler aliyenyang'anywa?
Sheria inasemaje juu ya umilikishwaji wa mali kama hizi zilizochukuliwa toka kwa wageni?

Baada ya hapo ndio tuendelee na kutafuta ''mchawi'' etc.
 
that is the wrong approach. The right approach ni kuwa wale wanakijiji ni wahalifu wachukuliwe hatua. Vitendo vyao haviwezi kuhalalishwa na bei ya Kimaro kununua shamba au mwaka gani alinunua shamba hilo. Uhuni walioufanya hauwezi kuhalalishwa kwa kujua kama shamba alilinunua kwa nani.

Lakini zaidi kama kungekuwa na issue ya umiliki wake swali lingekuwa ni hawa wanakijiji wamechukua hatua gani za kisheria kuzuia umiliki huo wa Kimaro? Nadhani hicho ndicho cha kuulizwa. Ni wana kijiji wana burden of proof ya kuonesha kuwa Kimaro kalipata shamba kwa njia kinyume na sheria.
 
Ni muhimu kutambua kuwa hii ni legal-political issue.
Unachokisema ni sahihi, lakini hakifanyi approach ya kuangalia uhalali wa Kimaro kumiliki shamba wrong. Kama kuna madai, sisi ni JF. Sisi sio mahakama. Ndio maana nikasema JF we are better than this. Sisi ni jukumu letu kutafuta ukweli wa tatizo lote. Kimaro ni kiongozi, hivyo kunapokuwa na tuhuma juu ya kiongozi ni muhimu tukaziangalia kwa ukaribu zaidi.
Ukisoma vizuri post yangu hakuna niliposema kuwa waliovamiwa waachiwe huru, ila nimesikitishwa na kuhusishwa kwa uvamizi huu na harakati za kisiasa za Mh. Kimaro bila vetting yoyote!Kabla hatujahusisha uvamizi na siasa za Kimaro ni lazima tupate uhakika kuwa chuki ya wanakijiji imepandikizwa na si genuine.
 
Jamani JF we are better than this,
Kwanini tunampa Kimaro ''easy ride''?
Shamba limevamiwa, ni habari ya kusikitisha, na kusikitisha kwa pande zote mbili.
Sisi kama JF nyumbani kwa GT, tunatakiwa kufanya a more systematic aproach kwa hili suala. Tusichague upande.
Tuanze kwa kuangalia,
Kimaro alilipata lini hilo shamba la ekari 500?
Alilipa kiasi gani cha pesa? Alimlipa nani?
Utaratibu gani ulitumika wakati anapewa umiliki wa shamba hilo toka kwa settler aliyenyang'anywa?
Sheria inasemaje juu ya umilikishwaji wa mali kama hizi zilizochukuliwa toka kwa wageni?

Baada ya hapo ndio tuendelee na kutafuta ''mchawi'' etc.

Hilo suala la objectivity humu ndani halipo sasa dawa kwenda hivi hivi kisanii sanii tuu

tualiacha serious discussions humu in 2006

wewe piga soga na hawa watu wa USA,EUROPE kisha kalale hamna jipya sikuhizi humu
 
Back
Top Bottom