UVAMIZI SHAMBA LA KILARI- AIBU KWA SERIKALI YA CCM, na RC KILIMANJARO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVAMIZI SHAMBA LA KILARI- AIBU KWA SERIKALI YA CCM, na RC KILIMANJARO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MADORO, Sep 15, 2012.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Shamba la Kilari lipo Kijiji cha Magadini, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro. Shamba hili lilikuwa linamilikiwa na Wahindi, lilikuwa linalindwa sana na serikali ya CCM, halikuvamiwa.Wahindi hao wameuza Shamba hilo lenye hati miliki, Limenunuliwa na Masista wa Holy Spirit, wanalitumia kwa kazi za huduma za Jamii: Wamejenga Shule ya Sekondari, wamejenga Kituo cha Afya, wamejenga Nyumba za waganga wanaotibu wanakijiji hao hao na vijiji jirani, wamemega eneo wakaipa serikali shule ambayo ipo tayari inatumika ili serikali iendeshe wakabaki na shule moja ya Sekondari. Wameipa serikali shule ya Msingi wakabaki na sekondari. Masista hao wanataka kujenga Mortuary kwa ajili ya kuhifadhi maiti, lakini eti sasa ndio shamba linamiwa. Watu mbalimbali wanaletwa na Mbunge wa Jimbo hilo Aggrey Mwanri ili ajipatie umaarufu wa kupata wapiga kura. Siku za hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa huo, Mkuu wa Wilaya, Kamishna wa Ardhi, na kamati nzima ya Ulinzi na Usalama wametinga Kijijini kuwaomba masista wawe na huruma japo wana hati miliki. Kauli nyingine ya Utata katika suala hili ni ya Waziri Anna Tibaijuka aliyewaambia Masista, ninyi ni watu wa huruma wahurumieni wavamizi. Hivi Ukiwa Mwekezaji katika nchi yetu lazima uwe mzungu, Mhindi au mwarabu ndo utalindwa. Huduma za hawa wanazozifanya kwa watanzania zinaonekana ni Ujinga kwa serikali? Kwanini serikali inataka wavamizi wa maeneo wahurumiwe, Mwanri anaingiza watu toka Kenya kuwapa maeneo katika Shamba la Masista, Masista wanatishiwa maisha. Lakini serikali yetu Kimyaaaaaaaaaa............... Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aibu. Nchi yetu haina sheria?
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ukitaka kujua serikali imelala basi kwenye maswala yanayohusu jamii ndio basi kabisa kimya kimya
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Very sad!
   
 4. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,379
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 280
  rushwaa! ni zaidi ya adui wa haki! watu hawaoni hata kwa macho yao faida za wananchi wanazopata ikiwemo kupanua ajira wanachovikiria ni ubinafsi wao tu na si vinginevyo iko siku.
   
Loading...