Uvaaji wa mavazi haya ni ulimbukeni wa kiwango cha juu sana

Ndugu yangu historia ya Emperor Constantine ipo tena hata kanisa Katoliki kwenye "archives" zao kule Vatican City wamehifadhi historia ya huyu mtu. Kila kitu alichokifanya kinajulikana, mimi nimeandika kwa kifupi sana, siwezi kuandika kila kitu. Kwa kifupi tu elewa kwamba Emperor Constantine alikuwa ni "wakala" shetani. Unaelewa alama ya "msalaba" inayotumiwa na Roman Catholic Church ilitoka wapi na nini maana ya maneno yaliyopo kwenye msalaba ule??
Mimi binafsi naamini uwepo wa MUNGU mmoja tu, MUNGU BABA muumba wa mbingu, dunia, nyota, jua, mwezi, sayari zote na kila kitu kilichomo ndani yake. Naamini kuwa BABA MUNGU ndiye aliyeumba kila aina ya "uhai" unayoifahamu wewe. Ningeweza hata kukuandikia Jina lake lakini jina hilo ni TAKATIFU mno kiasi kwamba siwezi kuliandika humu kwenye JF iliyojaa kila aina ya uchafu.
Fahamu tu kwamba Huyo BABA MUNGU ninayemwamini Ndiye BABA ya YESU KRISTO, BWANA NA MWOKOZI WETU.

Lucifer ambaye ndiye shetani na Ibilisi, aliumbwa na BABA MUNGU, lakini huyu Lucifer amekuwa akijifanya na yeye ni mungu kwa kuwadanganya watu ili wamwabudu na kumsujudia. Lucifer amekuwa akiwatokea watu katika namna nyingi, mfano mzuri ni kama alivyomtokea Emperor Constantine na kumpatia nguvu za ajabu. Emperor Constantine alikuwa anamwabudu Mithra ambaye ndiye huyo huyo Lucifer. Huku Africa mababu zetu walikuwa wakiabudu mizimu, ambayo ndiyo hayo hayo mashetani, akina Lucifer.
Kwahyo huyo Baba Mungu Mtoto wake ni Yesu?
 
Kwani hizo nguo ni pure 100% cotton
Au ni material sawa na nguo zingine zivaliwazo Daresalama?
 
Mtoa mada we umeona kitu tulichoiga ni hilo vazi tu? Mbona hata boxer uliyovaa ni umeiga pia maana sio utamaduni wetu, vua nguo zote vaa magome ya miti ndo tukuone kweli we una machungu
 
Kwahyo huyo Baba Mungu Mtoto wake ni Yesu?
Ulikuwa hujui kama YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU??
Hujui kuwa hata wewe pia unaweza kufanyika mwana wa MUNGU??
Hujui kama Malaika wanaitwa "wana wa MUNGU"??
Unajua kuwa kuna Ufalme wa MUNGU unakuja duniani na YESU KRISTO ndiyo atakuwa Mfalme katika ufalme huo?
Unajua kuwa ili upate kuingia katika Ufalme huo ni lazima "Umwamini YESU KRISTO, Ubatizwe, na uyashike mafundisho yake yote na kuyafanya?
Unajua kuwa usipoamini na kutubu utachomwa moto na kuangamizwa?
Unajua kuwa wale wote watakao amini watafanywa kuwa wana wa MUNGU na wataishi milele katika Ufalme wa MUNGU? Haujachelewa bado, unaweza kuamini kuanzia sasa.
 
Mbona na kama una jazba vile
Hiyo "jazba" umeiona wapi? Au na wewe unaabudu mashetani ukidhania una mwabudu MUNGU. Lucifer ni mjanja sana, amewadanganya wengi na mnamwabudu bila hata kujua. Lakini, ukitaka kuijua KWELI utaijua tu, ukiwa na shingo ngumu, haya shauri yako.
 
Ulikuwa hujui kama YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU??
Hujui kuwa hata wewe pia unaweza kufanyika mwana wa MUNGU??
Hujui kama Malaika wanaitwa "wana wa MUNGU"??
Unajua kuwa kuna Ufalme wa MUNGU unakuja duniani na YESU KRISTO ndiyo atakuwa Mfalme katika ufalme huo?
Unajua kuwa ili upate kuingia katika Ufalme huo ni lazima "Umwamini YESU KRISTO, Ubatizwe, na uyashike mafundisho yake yote na kuyafanya?
Unajua kuwa usipoamini na kutubu utachomwa moto na kuangamizwa?
Unajua kuwa wale wote watakao amini watafanywa kuwa wana wa MUNGU na wataishi milele katika Ufalme wa MUNGU? Haujachelewa bado, unaweza kuamini kuanzia sasa.
Naomba unieleweshe vizuri hapo kwenye neno mwana ni sawa na Mtoto si ndio?
 
Aina hii ya mavazi huvaliwa Ulaya na Amerika ya kaskazini kipindi hichi cha mwaka kwa sababu ya baridi kali na barafu inayodondoka huko. Kichekesho ni pale unapomwona mtu mzima na akili zake amevaa mavazi haya hapa Dar huku joto likiwa kali kiasi kwamba wewe uliyevaa T-shirt tu unatamani kuivua utembee kifua wazi.

Huu ni ulimbukeni wa kiwango cha kupitiliza, hata Wazungu waliobuni aina hii ya mavazi wakiona mtu amevaa mavazi haya huku kwetu na joto lote hili la Dar huwa wanacheka sana, wanatudharau sana na kutuona bado sana sisi ni watumwa wa fikra.


View attachment 656653 View attachment 656654 View attachment 656655

Kuna watu watatetea ulimbukeni huu kwa kisingizio cha sikukuu ya X-mass ambayo nayo ni upagani tu wala haina maana yoyote katika dini ya KWELI ya KIKRISTO. Na wengine watasema ni namna ya kuvutia biashara; lakini bado haileti maana hata kidogo. Nasema haileti maana sababu hakuna uhalisia wowote ule wa kuvaa nguo kama hizi sana sana anayevaa anageuka kuwa kituko kwa wale wanaoelewa maana ya mavazi haya.

Kwa akili hizi sisi Waafrika tutabakia kuwa watumwa wa Wazungu mpaka siku ile BWANA YESU atakaporudi tena kwa mara ya pili. Kwa akili hizi ndio maana Wazungu wanatuibia madini yetu mpaka na mchanga pia wanachukua na kusafirisha kwenda kwao tena tukiwasindikiza sisi wenyewe mpaka uwanja wa ndege na bandarini huku tukiwalinda na silaha nzito, na wao kutuachia mahandaki matupu.

Ningekuwa mimi ni Rais wa nchi hii ningepiga marufuku kabisa aina hii ya ulimbukeni kama alivyofanya Rais wa Korea ya Kaskazini Kim Jong-un; amesema hataki kabisa kuona raia wake wanasheherekea X-mass ama wanajihusisha na tamaduni zozote zinazoambatana na sherehe hizi za kipagani zilizoanzishwa na Wazungu wa Rumi.
Kwa hiyo ungefurahi kama angevaa suruali, kanzu, na koti juu? Labda una lako jambo!
 
japo umechanganya lugha ila ukweli kile ulicho kilenga kuwakumbusha wanajamii kimefika; hakna kitu ambacho ni sumu mbaya kama ubaguzi ndani ya mioyo ya watu, leo mkristo unambagua muislaum au muislaum unambagua mkristo kwa kigezo kipi hasa na ukiangalia hizi din tumeletwa tu na tumejikuta leo mm ni mkristo kwa sababu pengine kizazi changu kilikuwa katka mazingira ambayo wanzungu wenye imani ya kikristo walipita na leo mm najiita mkristo na vilex2 muislaum pia leo una imani hiyo ni kwa vile wazungu wenye imani hiyo walipita maneo ambayo ndio asili yako, lkn ebu fikiria kama hao wazungu wasingeweza kuja uku na kuambukiza imani zao kwa wazee wetu je ww ungezaliwa ukiitwa mkristo au muislam lahasha ww ungeitwa kwa majina ya wazee wako kwa imani yao ila ungeendelea kuitwa ni mtanzania, sasa kwann leo unaskia mtu anasema hupaswi kuchangamana na mkristo au muislaumunabaki unashangaa ni kwa kigezo gani wanena h, mara nyingi huwa nasikitika sana,naona ufahamu wetu umetekwa tayari na hao ambao mtoa mada anasema hataki kuwatumikia japo imani na tamaduni zingine za kwao unazitumikia. ebu ndg zangu tuache kujenga mazoe mabaya ya ubaguzi kati yetu na mara nyingi watu huwa hatufatilii hizi mambo ila ukianza kuzifatlia na ukazijua huwezi kumkuta shehe anatamka maneno ya hovyo kama haya au kiongozi wa kikristo aliyeiva akatamka maneno ya hovyo kma haya kw sababu wanajua
 
Kila mtu apambane na hali yake,achana nao mkuu na joto hili vijipu uchungu viwanyooshe unawambia lkn hawaelewi!! Jamaniiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom