Uvaaji kwenye Send Off na tamaduni za kiafrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvaaji kwenye Send Off na tamaduni za kiafrika

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ndachuwa, Jan 13, 2011.

 1. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwa muda sasa nimebahatika kuhudhuria baadhi ya sherehe za "send off" na kushangazwa sana na uvaaji wa yule anayeagwa.

  Waalikwa wote kwa maana ya wake kwa waume huwa wamevaa nadhifu kwa maana ya kufunika sehemu zote za miili yao. Lakini kituko ni yule anayeagwa ambaye siku hiyo huwa nusu uchi yaani ngua inaanzia kwenye chembe cha moyo shuka chini.

  Nisichoelewa wote tumealikwa ili tukamuage tayari kwa maisha mapya ya kuwa na mwanaume mmoja, badala ya yeye kuonyesha staha ya jinsi atakavyokuwa kwa mumewe siku hiyo yeye hugeuka kituko fulani kwani kwa tamaduni za kiafrika huo uvaaji haukubaliki mbele ya wazazi wake.

  Sasa kama ameshafanya maamuzi ya kuwa na mwanaume mmoja, hiyo vaa yale inatuma ujumbe gani kwa wanaume wa aina ya fataki walioko kwenye hiyo sherehe? au anataka kuwaambia nini wale vijana ambao pengine nao walikuwa kwenye mbio za kumtaka wakazidiwa?
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Married But Available (MBA)
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Waswahili wanasema "kiingiacho mjini si haramu"
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo si aolewe kimya kimya bila kukusanya watu kushuhudia wakati moyoni anajua anaongopa?
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Meaning?
   
 6. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uanajua tatizo letu sisi sote tunapenda sana mambo ya ki magharibi tunaiga kila kitu vingine hata havina maana bora tu viwe kama vya kizungu. Utamkuta mtu yuko Njombe kuna baridi ya kufa mtu lakini kwenye hiyo send off kavaa mabega wazi! ukiuliza maana yake ni nini wanasema kisasa Ah! haya wajameni.
   
 7. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  life is too short to be taken seriously
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Taking seriously, huyu binti anawaaga ndugu zake na si marafiki zake. Walio marafiki wataendelea kuwa marafiki zake lakini kwa upande wa ndugu anahama kwao anao kwa boma lingine; sasa kwanini haya mambo yasifanyike zaidi nyumbani ili na hao ndugu zake washiriki wengi zaidi?
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ikimaanisha kuwa kuwa Mswahili hajali 'uharamu' wa tendo madhali ni fashion mtaani. Sad but true
   
Loading...