Uuzwaji nyumba za NHC: kumbe viongozi wetu hawajifunzi kabisa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uuzwaji nyumba za NHC: kumbe viongozi wetu hawajifunzi kabisa!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Jun 3, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nimeshtushwa sana na habari hii, inaonekana serikali ya awamu ya nne haijajifunza kitu chochote kutoka makosa ya uuzwaji wa nymba za serikali uliofanyika wakati wa awamu ya tatu. kweli tuna safari ndefu sana!!
  Kuuza nyumba za serikali si suala geni - Tibaijuka
  Na Mwandishi wetu  2nd June 2011


  [​IMG]
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka


  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amesema kwamba suala la wananchi kuuziwa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) siyo geni nchini na kwamba limekuwepo kwa muda mrefu.
  Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipoombwa na NIPASHE kutolea ufafanuzi taarifa iliyoandikwa na gazeti hili jana kwamba, kuna mikakati iliyopangwa chini ya kamati maalumu ya wapangaji wa nyumba za NHC jijini inayotaka wapangaji wa nyumba hizo kuuziwa kwa bei sawa na bure,kwa hoja kwamba wamekaa kwa muda mrefu katika nyumba hizo.
  “Hata hivyo, NIPASHE nakualika pale Diamond Jubilee Juni 4 mwaka huu, saa tatu asubuhi ambapo nitakutana na wadau wote wa nyumba katika mkutano mkubwa utakaohudhuriwa na mimi na wasaidizi wangu wizarani, bodi ya NHC ,wapangaji wa nyumba za NHC na wadau wengine wote, uje utapata majibu,” alisema.
  Alisema katika mkutano huo, ndipo ufafanuzi wote utatolewa na msimamo wa serikali kuhusiana na ombi hilo utaelezwa. Jana gazeti hili liliandika kuhusu nyumba za Shirika la Nyumba nchini NHC ambazo ziko katika hatari ya kuporwa kama uporaji uliofanywa na serikali ya awamu ya tatu kwa kisingizio cha kuwasaidia watumishi wa serikali, hali iliyomweka Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwenye mtego mkubwa.
  Safari hii mikakati imepangwa chini ya kamati maalum ya wapangaji wa nyumba za NHC wakijenga hoja mufilisi kwamba wanastahili kuuziwa nyumba za shirika hilo kwa bei sawa na bure kwa kuwa wamekaa muda mrefu kwenye nyumba hizo.
  Uchunguzi huru wa NIPASHE na vielelezo mbalimbali vilivyokusanywa juu ya njama hizo, unaonyesha kuwa chini ya kamati hiyo shinikizo sasa linaelekezwa kwa Waziri Tibaijuka ili asaidie kulazimisha NHC kuuza nyumba hizo kwa wapangaji wake kwa bei ya chee kama walivyofanyiwa watumishi wa serikali wakati wa awamu ya tatu  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Tupige yowe njama za kuipora NHC
  Na Mhariri  2nd June 2011


  Kwa ujumla taifa hili limekuwa na tatizo kubwa sana la kutumia rasilimali zake vizuri kwa ajili ya ustawi wa watu wake; kumekuwa na kelele juu ya uchimbaji wa madini, uwindaji katika mbuga za wanyama, mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali na mashirika au makampuni mbalimbali; kote huko kuna kilio kimoja, taifa kutokunufaika. Kelele hizi aghalab zimeongezewa uzito na maamuzi mbalimbali ambayo yamefanywa na viongozi wetu juu ya matumizi ya rasilimali za taifa; kwa mfano hadi sasa wananchi kwa ujumla wao wanaamini kwamba mikataba yote ya uchimbaji wa madini hainufaishi taifa hili, ndiyo maana baada ya kufunguliwa kwa migodi mingi mikubwa ya dhahabu nchini bado uchumi wetu kama taifa haujaona nafuu ya kuweko kwake.
  Ni muhali kusadiki kuwa pamoja na wingi wa migodi hii, bado sarafu ya Tanzania mwaka baada ya mwaka inazidi kutetereka dhidi ya dola ya Marekani wakati uzalishaji wa dhahabu ni wa kiwango cha juu kabisa nchini. Jibu pekee la kushindwa kubadili hali ya uchumi wetu wakati shughuli za uchimbaji madini zikipamba moto ni mikataba ya ovyo isiyokuwa na maslahi ya kitaifa.
  Maamuzi na mikakati ya namna hii, yaani isiyoakisi hata chembe ya maslahi ya taifa, yamekuwa ni ya kawaida kabisa nchini; kwa mfano wakati serikali ya awamu ya tatu ilipoamua kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa kabisa, ilijengwa hoja muflisi kwamba nia ilikuwa ni kuwasaidia watumishi wa serikali maskini, wasio na uwezo kupata makazi bora.
  Umma ulitaharuki kwa kuwa uliamini maamuzi yale hayakuwa na tofauti yoyote na mengine mengi ambayo yalikuwa yanaonekana yakichukuliwa kwenye sekta ya madini, uwindaji wa kitalii, na zaidi sana katika uuzaji wa mashirika ya umma na vitega uchumi vingine vilivyokuwa vinamilikiwa na serikali kwa niaba ya wananchi.
  Pamoja na kelele zilizopigwa na kwa kweli hata leo zikiendelea kupigwa, viongozi wa serikali waliojaa jeuri na kiburi walibeza wananchi kwamba walikuwa wanasumbuliwa na wivu ndiyo maana walikuwa wanapinga uporaji huo uliobatizwa jina la ‘uzwaji wa nyumba za serikali kuwawezesha watumishi maskini'. Hakika haukuwa uuzaji na asilani hakuna mwananchi anayesaidiki kwamba ulikuwa uuzaji ila uporaji wa mchana kweupe.
  Tunasisitiza kuwa ulikuwa ni uporaji wa rasilimali za taifa mchana kweupe kwa sababu watu wale waliodaiwa kutokuwa na uwezo na hivyo kuwa kisingizio kama si kichaka cha kuhalalisha uporaji huo, punde tu wengi wao baada ya kukabidhiwa hati zake walizibomoa nyumba zile na kuporomosha majengo ya kisasa ambayo sasa ni vitegauchumi vya uhakika vinavyowaingizia mamilioni kila mwezi.
  Baada ya mkakati huo haramu kufanikiwa habari ambazo zimethibitishwa na gazeti hili, ni kwamba sasa hivi mipango imeiva kwa kikundi kidogo cha wapangaji wa nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) kutaka nao waruhusiwe kufanya uharamia kama ule uliofanywa dhidi ya nyumba za serikali. Inasikitisha na kuuma sana.
  Kuna habari kwamba mkakati huo unasukumwa na wananchi wazawa, lakini ukweli ni kwamba nyuma yao kuna jumuiya fulani ya raia wenye asili ya nje kutaka kumiliki nyumba hizo kwa nguvu ya fedha. Hawa wameandaa mikakati kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kurejesha himaya yao waliyokuwa nayo kabla ya utaifishaji wa miaka ya sabini uliofanywa chini ya sera za Azimio la Arusha.
  Tunasikitika kwamba juhudi hizi kwa hakika ni mikakati mibaya ya kutaka kuhujumu NHC ambayo katika siku za hivi karibuni imejipanga vilivyo ili kupambana na tatizo la uhaba wa makazi bora nchini, lakini pia kutoa mchango wake katika upangaji wa miji yetu ili walau ikaribiane na ile ya wenzetu waliopiga hatua.
  Kwa njama hizi, NHC inaporwa rasilimali kidogo walizonazo ambazo zinahitajika sana kuwapa uwezo wa kujenga nyumba nyingi zinazohitajika kwa wakazi si wa mijini tu bali hata vijijini; tunaamini kwa dhati kabisa kwamba mwelekeo huu wa mambo kama kweli utapata baraka za viongozi wakuu serikalini, yaani kuanzia wizarani basi NHC itakuwa imezikwa kama ambavyo maamuzi mengi mabovu yamechangia kuua mashirika mengi ya umma ambayo kama leo yangelikuwako pengine hali yetu kiuchumi isingelikuwa mbaya kama ilivyo sasa.
  Kwa jinsi hii tunakataa na kupinga kwa nguvu zetu zote njama za kikundi kidogo cha wapangaji wa nyumba za NHC kutumia bahati na fursa ya kuwa wapangaji sasa wageuke kuwa wamiliki wa nyumba hizo. Huu ni uporaji na wizi kama ulivyo uporaji mwingine wowote.
  Taifa hili liliibiwa mara moja nyumba za serikali kwa kisingizo kama hiki, sasa umma ni lazima ukatae kuingia katika mtego huu, ni wajibu wetu sote kuhami mali za taifa hili ili zitufae leo na wale wa vizazi vijavyo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Acha wafu wazike wafu wenzao maana tuliwachagua wenyewe na kuamua kufuata sera zao. Sera za CCM ndo hizo za kuuza kila tulichonacho kuanzia ardhi, mashirika ya umma hadi nyumba. Kupita kelele na kulia sana hakufufui maiti ingawa itaonesha majirani kuwa una msiba.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Nyumba za NHC hata zikigaiwa bure ni sawa tu kwani nyingi kati ya hizo nyumba zilidhulumiwa kwa wamiliki wa halali na nyerere.
   
 5. p

  pointers JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nchi hii watu wameshachoka kufikiria sasa hv wanaenda alimradi tu kesho ipo
  na siku zinasogea........
   
 6. Kamtori

  Kamtori Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  What ever msajili, nhc, nyumba za serikali etc whats the difference.... Mambo ni yale yale either kupeana au kuuziana, iwe halali au sio halali . One can not meet the needs opf tanzanians ni gumu sana gumu kweli
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Serikali haina pesa inaelekea kufilisika.Kumbuka hata kampuni binafsi linapoanza kuuza immovable assets ujue liko taabani kifedha na linafilisika, kwa hiyo hizi ni dalili za serikali kufilisika hawana ujanja na ndiyo maana tunaanza kusikia viwanja vinauzwa kinyemela na serikali.Serikali yetu imekamilika kuwa ni ya kisanii.Tutaona mengi get tuned
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  tibaijuka na CEO wa NHC mchechu kama wasomi na wenye uzoefu wa masuala ya nyumba ya kimataifa wanapaswa kukumbuka waliyoyaona katika nchi zingine na tena huyo mchechu nafahamu alikuwa mkurugenzi wa benki inayotoa mikopo ya nyumba kabla hajawa mkurugenzi wa NHC. nyumba zinajengwa na kuuzwa, sasa shirika kama NHC lisilojenga nyumba ukiachilia mbali ahadi za kisiasa kuwa "litajenga nyumba 15,000 nchi nzima na tunyuma tuchache inatojaribu kujenga kwa mikopo na ubia wenye tija ya kutiliwa shaka za kifiadi" linawezaje kuuza nyumba? na likishauza nyumba zake litakwepaje hali iliyowakumba ATCL ya kuwa na sirika lisilo na ndege? yaani siku wakibaki NHC bila nyumba watakauwa wakifanya kazi gani?

  nafikiri kwanza watuanbie kuwa baada ya kuuza nyumba walizokwishauza (kama zile mbili za chalinze) wamezi-replace kwa kujenga nyumba ngapi nyingine na je biashara yao ya kujenga na kununua iko katika soko huru na inawapatia faida? inawezekana kufanyika hata kwa mtu ambaye hajawahi kupanga nyumba za shirika hilo lakini mwenye uwezo na utashi wa kununua na kulipa kwa haraka ili kuwezesha mtaji kuzungushwa kwa haraka na kujenga nyumba zingine?

  mi nilitegemea kuwa hata baadhi ya nhyumba zilizoko prime locations zingewekwa kama dhamana ili kupata mikopo mikubwa ya kujenga nyumba zaidi za apartments maeneo zitakakouzika kirahisi kabisa na kwa kasi kama manzese, kinondoni, magomeni nk hata kwa kuingia ubia na wamilikiw a maeneo hayo ili kuokoa fedha ambazo zingepaswa kulipwa kwao kama fidia ya ardhi. hii ikiwa sehemu ya mkakati wa kuligeuza jiji la dar kuwa la kisasa na lenye uwezo wa kuwa-accomodate wakazi wake. pia mkakati kama huo ungweza kabisa kupelekwa katika miji mingine yenye potential ya soko la nyumba la kutosha ili kuboresha makazi na mazingira ya miji yetu.

  sasa haya madudu ya kuuza kila asset unayoikuta na bila kuwa na mkakakti wowote wa kuongeza stock kama replacements, na kweli ni uzalendo huu jamani? hatukujifunza kweli kwa madudud ya waziri maghufuli enzi za mkapa walipouza nyumba za serikali na leo kodi yetu inatumika tena kuwapangia maafisa makazi mahotelini? angalieni jamani hadi spika kfunga barabara, as consequence ya kuuza nyumba za serikali, damu kimwagika pale wananchi watakapotaka kufungua hiyo barabara kwa nguvu, maghufuli anaweza kusema hahusiki? naye atasema wa kulaumiwa ni chadema peke yake? hizi siasa gani hizi jamani?
   
 9. MALUNGU

  MALUNGU JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miss Judith kwenye Magamba hakuna cha msomi! hujasikia wasomi ving'ang'anizi wanavyolalamika taaluma zao haziheshimiki?
   
 10. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimekugongea Senksi kwa pumba zako
   
Loading...