Uuzaji wa viwanja Manispaa ya Dodoma:Muda wa mwezi mmoja kukamilisha malipo ni mfupi mno kwa watanzania wa kawaida

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,985
144,312
Tunashauri uongozi wa Manispaa ya Dodoma kutafakari upya muda walioutoa kwa wananchi waliojitokeza kununua viwanja katika Manispaa hiyo ambapo wanatakiwa kukamilisha malipo yote ndani ya siku 30 tangu tarehe ya kukabidhiwa invoice.

Kwanza bei ya viwanja kwa mita ya mraba kiasi fulani iko juu kwa kiasi fulani kwani bei ya chini kwa square meter moja ni sh 3,000, bei ya kati ni sh 6,000 kwa mita moja ya mraba na bei ya juu ni shilingi 8,000 kwa mita moja ya mraba na hizi bei ni kwa viwanja ambavyo ni kwa ajili ya makazi tu na tukumbuke hii ni bei ya serikali na si ya mtu binafsi.

Bei kwa viwanja vya makazi na biashara ndio ziko juu zaidi kwa mita moja ya mraba ambayo bei ya chini ni kama shilingi 5,000kwa mita ya mraba, bei ya kati shilingi 7,500 na bei ya juu ikiwa ni shilingi 8,500 kwa mita moja ya mraba.

Bei kwa ajili ya viwanja vya kufanyia biashara tu ndio inafika mpaka shilingi 10,000 kwa mita ya mraba na hivi viwanja viko katika eneo la Mtumba eneo liliko katika barabara kuu ya Dodoma to Dar-es-Salaam.

Maeneo mengine ambayo viwanja bado havijaanza kuuzwa ni Nala, Michese na Iyumbu ambako kote bei zinafanana.

Ukweli ni kwamba licha ya kila mtu kutakiwa kuchagua kiwanja chenye ukubwa na bei atakayoimudu lakini muda huo wa siku 30 uliotolewa ni mfupi mno kwa wananchi wengi wa kawaida kumudu.

Kwa mfano kiwanja cha ukubwa wa mita za mraba 700 kwa bei ya shilingi 3,000 kwa mita moja ya mraba thamani yake ni shilingi 2,100,000 ambayo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30 tu na ukishindwa unanyang'anywa tena hawalazimiki kukupa taarifa kulingana na maelezo yaliyoko katika invoice.

Kweli wapo watu wenye fedha zao ambao hela kama hiyo ni ndogo sana kwao ila kwa wananchi wa kawaida wenye majukumu mengi ya kifamilia kulipa hela hiyo ndani ya siku 30 ni changamoto unless viwanja hivi vimelenga watu wenye vipato vikubwa kwani hata kwa watumishi wa umma hapo ni lazima wengi watafute mkopo ndio waweze kulipa ndani ya hizo siku 30 zilizotolewa.

Mimi ningewashauri watoe walau miezi miwili mpaka mitatu ya kukamilisha malipo na mtu akishindwa ndio anyang'anywe kiwanja ila tofauti na hapo sitashangaa wananchi wengi wakaja kushindwa kukamilisha malipo haya ndani ya muda uliopangwa licha ya wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye ununuzi wa hivyo viwanja.

Wakati wa CDA walikuwa wanatoa muda wa kutosha kwa watu kulipia kidogokidogo tofauti na leo hii sasa sjui kwasababu Dodoma imekuwa makao makuu ya serikali watu ndio hatuelewi!!

Ile dhana kwamba awamu hii ni wanyonge basi tuitekeleze kwa vitendo na sio kwa maneno tu ya majukwaani.

Anyway, labda wanapima upepo kwanza wakiona hali ni tofauti huenda wakaongeza muda.
 
Mleta mada sema huna hela usiseme watu hawana hela utashangaa nafsi yako
 
Mleta mada sema huna hell usiseme watu hawana hela utashangaa nafsi yako
Vile viwanja vya Bagamoyo vilivyotangazwa zaidi ya mwezi vimeisha?

Mwisho wa siku kuna vitakavyobaki na kuna ambavyo watu wastashindwa kuvikomboa na si ajabu huko mbeleni hata bei ikaja kushushwa na muda ukaongezwa.

Siku JPM akiagiza muda uongezwe utakuja hapa na kuanza kusifia.Nyie ni bendera fuata upepo.
 
Watu waliipuuza Dodoma ndo maana viwanja bado bei iko chini. Ukitoka km 7 tu nje ya mji bado bei ndogo Dar Bunju, Kibaha, Chanika, Chamazi viwanja bei kubwa na viko zaidi ya km 30 toka mjini
 
Watu waliipuuza Dodoma ndo maana viwanja bado bei iko chini. Ukitoka km 7 tu nje ya mji bado bei ndogo Dar Bunju, Kibaha, Chanika, Chamazi viwanja bei kubwa na viko zaidi ya km 30 toka mjini
Vyuma vimekaza sio kama zamani.

Tatizo kubwa hapa ni huo muda.
 
Vyuma vimekaza sio kama zamani.

Tatizo kubwa hapa ni huo muda.
Chelewa chelewa utakuta mwana si wako nenda vikoba,Sacco's au benki kakope ununue chap chap uwe unawalipa taratibu kiwanja kikiwa mikononi mwako wewe endelea kulia lia hapo chadema fursa utaziona zinakupita Au ndio nyie matapeli msiokopesheka popote hata mpesa au tigo pesa au Airtel money?Kama ndio basi utalia Sana awamu hii
 
Chelewa chelewa utakuta mwana si wako nenda vikoba,Sacco's au benki kakope ununue chap chap uwe unawalipa taratibu kiwanja kikiwa mikononi mwako wewe endelea kulia lia hapo chadema fursa utaziona zinakupita Au ndio nyie matapeli msiokopesheka popote hata mpesa au tigo pesa au Airtel money?Kama ndio basi utalia Sana awamu hii
Unachangia kwa kuangali hoja imeletwa na na nani na si uhalisia wa mambo.

Narudia, siku JPM akiagiza muda uongezwe utakuja hapa na kuanza kusifia kwa jinsi ulivyo mnafiki.

Mimi nimeleta hapa kusaidia watu na sio kama unavyofikiri.

Huna tofauti na wabunge wa chama kile!
 
Chelewa chelewa utakuta mwana si wako nenda vikoba,Sacco's au benki kakope ununue chap chap uwe unawalipa taratibu kiwanja kikiwa mikononi mwako wewe endelea kulia lia hapo chadema fursa utaziona zinakupita Au ndio nyie matapeli msiokopesheka popote hata mpesa au tigo pesa au Airtel money?Kama ndio basi utalia Sana awamu hii
kabombe angalia mwenzako huyu anaewaza siasa kwa kila jambo!!
 
Leo nimekuwa wa kwanza kukupa like, japo ukweli ni kuwa kila kitu kina faida na hasara zake. Wakiongeza muda kuna watakaoliwa pesa zao pia. Yaani mtu anajitutumua kwenda kushikiria kiwanja, miezi mitatu inakatika mishe hazijasoma, kiwanja kinaondoka.
 
We ngoja hivyo viwanja watakuja kupiga navyo picha kama vile vya bagamoyo Kila siku matangazo kwenye Redio na tv

Ova
Hivyo viwanja kwa eneo la Mtumba tu ni zaidi ya 9000 bado katika hayo maeneo mengine alafu vyote vinunulike ndani ya mwezi tangu mtu upewe invoice.Sio kwa Tanzania hii hata kidogo.

Time will tell.
 
Wengi mnaochangia mada,nina mashaka nanyi kwamba hamuishi Dodoma.Kwa taarifa yenu,tayari huo mpango umeshadoda,kwa sababu alizozitoa mleta mada.

Hali ilivyo ngumu kwa sasa si kama zamani kwa tawala zilizopita,ambapo mtu angeweza kulipa viwanja 10 au zaidi kwa mara moja.

Sasa hivi Dar kuna nyumba zinauzwa,zamani ungesema bei za kutupwa,Mtu anatangaza Nyumba bei M 50 anashusha hadi 25 bado hapati mteja,.

Iliyokuwa manispaa ya mji ambayo sasa ni Jiji,walijichanganya kwa kutangaza muda mfupi wa kulipia kwa kulenga wafanyakazi wa serikali ambao wamehamishiwa hapa kwamba watavikimbilia.Ukweli ni kwamba wafanyakazi wengi wa serikali hawana interest ya kuwekeza makazi Dodoma,wengi wao wanaishi robo Dodoma Robo tatu ni Dar,habari ya kujenga Dodoma haiwaingii akilini,hii imepelekea mpango wa jiji kuuza hivyo viwanja kwa kasi na kwa bei mbaya Kufeli mapema asubuhi.

Wito kwao,waangalie upya huo mpango wao,kwa kuzingatia hali halisi ya kipato cha sasa cha wafanyakazi na wananchi wa kawaida.
 
Single News | Dodoma City Council
thumb_580_800x420_0_0_auto.jpg

Salary Slip kwa hili leo nakuunga mkono, Dodoma sasa viwanja vimekuwa ghali kuliko Miji mingine na masharti aliyotoa Mkurugrnzi wa jiji na Madiwani ni uroho wa pesa
wakati wapo CDA viwanja vya makazi vilikuwa bei ya juu sana ni 4,500 na biashara vilifikia 5,000 na bado watu mpaka leo hawajamaliza madenilicha ya kupangiwa zaidi ya miezi 6 au mwaka, viwanja hivi vipo jirani kabisa ya Jiji la Dodoma
Huko Mtumba na njia panda ya Kikombo ni zaidi ya kilomita 20 (sawa Dar mpaka Kibaha) Iyumbu nako barabara na ulinzi bado si salama
Ni mihemuko tu ya Madiwani kwani hata kwa miaka 5 bado hapatakuwa pamejengwa kwa huduma zote ikiwemo nyumba za ibada na Hospital
na mimi naomba muda uongezwe pia bei iangaliwe kwani si ya mwaka huu ni kwa miaka 7 ijayo
Kitu alichokifanya Mkurugenzi Kunambi ni kuua biashara za Walanguzi ambao walikuwa wakihodhi viwanja na kuja viuza bei ya juu
kwa mpango huu nawaona Madalali wote wamelegea na macho yamewatoka kwani huwezi nunua viwanja mpaka 10 kwa kuhodhi kwani lazima hela ipotee
 
Back
Top Bottom