Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,142
- 6,947
Kwa kweli ni hali ya kuskitisha kwa kuona familia nyingi zilizokuwa zikimiliki nyumba, mashamba, viwanja na kuuza vitu hivyo kisha kugawana pesa, baada ya muda pesa zinakwisha na kurudi kwenye umaskini.
Kwenye miji mikubwa kama vile Dar, wengi wameuza majumba yao kwa watu wengine, baada ya muda pesa zinawaishia na kuwa omba omba. Ingetolewa elimu ya kuweza kuingia ubia na wanaotaka kununua, badala ya kuwauzia, wakajenga kwa ubia.
Wanaharakati, wanasheria na wadau wa nyumba kama NHC, mabenki, wangeanzisha njia za kuingia ubia na wananchi, wenye majumba, viwanja, mashamba, ingesaidia kuondoa umaskini. Wakawajengea nyumba za ghorofa za kisasa kwa ubia.