Uuzaji wa Nyumba, viwanja na mashamba kunawatia wananchi umaskini

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,592
2,000
Kwa kweli ni hali ya kuskitisha kwa kuona familia nyingi zilizokuwa zikimiliki nyumba, mashamba, viwanja na kuuza vitu hivyo kisha kugawana pesa, baada ya muda pesa zinakwisha na kurudi kwenye umaskini.

Kwenye miji mikubwa kama vile Dar, wengi wameuza majumba yao kwa watu wengine, baada ya muda pesa zinawaishia na kuwa omba omba. Ingetolewa elimu ya kuweza kuingia ubia na wanaotaka kununua, badala ya kuwauzia, wakajenga kwa ubia.

Wanaharakati, wanasheria na wadau wa nyumba kama NHC, mabenki, wangeanzisha njia za kuingia ubia na wananchi, wenye majumba, viwanja, mashamba, ingesaidia kuondoa umaskini. Wakawajengea nyumba za ghorofa za kisasa kwa ubia.
 
msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,639
2,000
mimi juzi nimejinyakulia nyumba ipo kozi ya kumi tabata kinyerezi kwa mil 20, yaani pale nazungusha mkanda na kuongeza kozi mbili juu the napauwa,aliyeniuzia anasema anaenda kufungua baa.
 
Kama hiyo biashara,haielewi vizuri kuifanya,atakujajikuta mtaji wote umekata,na umaskini ameukaribisha.
 
msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,639
2,000
ndio hapo sasa tena yeye mwenyewe ndio alikuwa ananisumbua kweli,anaona mil 20 ni hela kubwa ukilinganisha na thamani ya ile nyumba isee. tena ni kijana tu umri wangu UNAJUA KUJENGA NI KIPAJI PIA,NYUMBA SIO MATAKO MKUU

Kwa nini usimpe ushauri,atulie kwanza,shida zinapita tu,utafika wakati mambo yake yanaweza kuwa mazuri.
 
msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,639
2,000
duuuh ushauri tena ndugu,mtu amehaliana na familia yake mimi nimshauri nitaweza mkuu?
 
Job Richard

Verified Member
Feb 8, 2013
3,326
2,000
unapokiuza kitu ushajifikiria PIA MTU HAFUNDISHWI KUTUMIA PESA mbona kuna watu wametajirika kwa kuuza nyumba zao mjini na kwenda kuanzisha biashara WANGAPI WAMEUZA KARIAKOO NA SAIZ WANA MIRADI KIBAO umaskin sio kuuza bali una fanyaje hiyo pesa izalishe UTAFUNDISHWA BILA KUJICOMMIT NI BURE TU
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
48,726
2,000
Kwa kweli ni hali ya kuskitisha kwa kuona familia nyingi zilizokuwa zikimiliki nyumba, mashamba, viwanja na kuuza vitu hivyo kisha kugawana pesa, baada ya muda pesa zinakwisha na kurudi kwenye umaskini.

Kwenye miji mikubwa kama vile Dar, wengi wameuza majumba yao kwa watu wengine, baada ya muda pesa zinawaishia na kuwa omba omba. Ingetolewa elimu ya kuweza kuingia ubia na wanaotaka kununua, badala ya kuwauzia, wakajenga kwa ubia.

Wanaharakati, wanasheria na wadau wa nyumba kama NHC, mabenki, wangeanzisha njia za kuingia ubia na wananchi, wenye majumba, viwanja, mashamba, ingesaidia kuondoa umaskini. Wakawajengea nyumba za ghorofa za kisasa kwa ubia.
Elewa kitu kimoja! Kuingia ubia ni wenye mali tu wakikubaliana wenyewe, ila mara nyingi nyumba za urithi hizi wengi wao kila mtu anatka kuchukua chake mapema.
Tushaona nyumba kko, nyumba inauzwa mln 700 kwenye mgao kuna watu kama 30
Nyumba nyingine inauzwa mln 180 kwenye mgao kuna watu 23....mtu anapata hela ambayo kama akiwa hana malengo atapigika tu,
 
Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,592
2,000
Elewa kitu kimoja! Kuingia ubia ni wenye mali tu wakikubaliana wenyewe, ila mara nyingi nyumba za urithi hizi wengi wao kila mtu anatka kuchukua chake mapema.
Tushaona nyumba kko, nyumba inauzwa mln 700 kwenye mgao kuna watu kama 30
Nyumba nyingine inauzwa mln 180 kwenye mgao kuna watu 23....mtu anapata hela ambayo kama akiwa hana malengo atapigika tu,
Ndio maana nikasema,wanaharakati,na wanasheria wawasaidie,hawa watu kuwafahamisha kuhusu faida ya ubia,kwa mfano mna nyumba ndogo,na kiwanja kiko maeneo pazuri kibiashara au kimakazi,hawa wangeshauriwa kuingia ubia,ikijengwa nyumba ya ghorofa kumi,yenye pande nne,na maduka 20,kiujenzi wa maduka kuanzia chini ya ardhi,na mpaka uwani,hawa warithi thalathini kila mmmoja hata kosa,upande wa nyumba au duka,na atapangisha maisha yake,na mbia naye pia atapata sehemu yake.
Kuliko kuuza nyumba ndogo kwa ml 700,wakigawana kila mmoja akipewa 10m,baada ya mda amezimaliza,wengine wanatapeliwa na wapenzi wao(hasa kina dada,wanatapeliwa sana),wanaume ndio watahonga,pombe,starehe kwa fujo,ndani ya mwezi pesa yote imekatika.Wanarudi kwenye ufukara wa Ombaomba.
 
Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,592
2,000
mimi juzi nimejinyakulia nyumba ipo kozi ya kumi tabata kinyerezi kwa mil 20, yaani pale nazungusha mkanda na kuongeza kozi mbili juu the napauwa,aliyeniuzia anasema anaenda kufungua baa.
Haya mambo ya ubia yanafanyika,lakini hakuna wanaharakati,wala wanasheria,wanaongelea suala hili,na kujitolea kuwaelewesha watu,faida zake,na jinsi mikataba inavyokwenda.
Inasikitisha na kutia uchungu sana,kuwaona hawa watanzania wenzetu,waliouza nyumba,maeneo yao kwa wageni au matajiri fulani,yule mgeni anatafuta mbia,anajenga jumba kubwa,la kitega uchumi,hawa watanzania wenzetu wanabaki kuwa ombaomba,na kubakiya kusemwa,ile nyumba ilikuwa yao,waliuza wakagawana,sasa hawana hata shilingi,wamekuwa ombaomba.
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
4,750
2,000
Kuna mawili: anaweza akapoteza au akapatia. Nina ushahidi wa kweli kabisa mtu aliuza kiwanja akanunua baiskeli akawa anaitumia kutembeza na kuuza matunda ya msimu. Huwezi amini ndani ya mwaka mmoja aliweza kujenga nyumba na baadae kununua kiwanja. Sasa ni mfanyabiashara wa viwanja wa kuuza na kununua. Kuna watu wana business idea lakini hawana mtaji.
 
Hao wenye kufanikiwa ni wachache,kuliko wasiofanikiwa katika biashara,na labda huyo aliyefanya biashara kwa baiskeli,alikuwa na biashara,isiyo halali,biashara zisizohalali,zinatajirisha mara moja,lakini ujuwe ni kosa kisheria.
 
mkuu, ndo maana nikatangulia kuseama kuna mawili yaani kufanikiwa au kutofanikiwa. Ni kweli wengi huwa wanatawaliwa na tamaa ya pesa. lakini kuna watu pia wana rasilmali kama nyumba au mashamba ambayo ni mali lakini hayawaingizii chochote. wengine wanakufa na huku nyuma watoto wanauza hizo mali na kugawana pesa. kimsingi mtoa mada anataka watu wapate elimu juu ya uwekezaji kupitia mali walizo nazo. Hili ni jammbo jema
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,464
2,000
mimi juzi nimejinyakulia nyumba ipo kozi ya kumi tabata kinyerezi kwa mil 20, yaani pale nazungusha mkanda na kuongeza kozi mbili juu the napauwa,aliyeniuzia anasema anaenda kufungua baa.
Hadi auze kreti ngapi aje kuwa na uwezo wa kuijenga kama hiyo?
 
Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,592
2,000
mkuu, ndo maana nikatangulia kuseama kuna mawili yaani kufanikiwa au kutofanikiwa. Ni kweli wengi huwa wanatawaliwa na tamaa ya pesa. lakini kuna watu pia wana rasilmali kama nyumba au mashamba ambayo ni mali lakini hayawaingizii chochote. wengine wanakufa na huku nyuma watoto wanauza hizo mali na kugawana pesa. kimsingi mtoa mada anataka watu wapate elimu juu ya uwekezaji kupitia mali walizo nazo. Hili ni jammbo jema
Ndio hasa lengo la mada,nilioandika,kwa vile tunaowataalam,wanasheria,wanaharakati,wangewasaidia,walio na ardhi,nyumba,mashamba,ambao bado wako kwenye lindi la umasikini.
Leo tunalalamika kuhusu ombaomba,ukichunguza kwa makini hao ombaomba,wazazi au mababu au mabibi,waliacha ardhi,nyumba,mashamba,lakini viliuzwa,pesa zikatafunwa,ndio hao ombaomba,hawana ardhi tena,vizazi kwa vizazi.
 
jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,411
2,000
mi natafuta shamba barabara ya msata bagamoyo.mwnye lead naomba
Ni nayajua mshamba eneo la msata na mbele ya msata. ...

Kwa uzoefu wangu bara bara ya msata bagamoyo yapo lkn yako ndani sana na bei ghali au la mengine ni ya matapeli. ..

Mimi nilinunua Msata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom