Uuzaji wa nyumba bila makubaliano

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Mimi ninaishi eneo la Manzese Uzuri. Katika eneo hili kuna familia moja ambayo imeishi nje kwa wiki mbili sasa. Familia hiyo ilikuwa inaishi kwenye nyumba ya uridhi. Nyumba hiyo waliachiwa watu wawili ambao ni mwanaume na mwanamke baada ya wazazi wao kufariki. Kaka mtu alihama eneo hilo na kwenda kutafuta maisha eneo lingine. Kwa sasa naskia amejenga nyumba yake na anaisho na familia yake kwa raha mustarehe.

Katika nyumba hiyo ya urithi alikuwa anaishi bibi mmoja na watoto wake, wajukuu na wapangaji. Kaka mtu alimtaka dada yake wauze hiyo nyumba ili wagawane fedha. Lakini dada mtu alikataa kwa sababu anaishi kwenye hiyo nyumba na kodi anayopata inamsaidia kuendesha maisha yake. Na faida nyingine hapati kero ya kudaiwa kodi ila yeye anadai kodi. hiyo kodi apatayo hamgawii kaka yake. Kwa sababu hizo alikataa kuuza nyumba hiyo.

Kaka mtu kuona hivyo aliamua kuuza nyumba hiyo kwa mfanyabiashara mmoja aitwaye Makanya. Kwa sababu bibi mwenye nyumba na familia yake walikataa kuhama ilibidi mnunuzi wa nyumba atumie nguvu ya dola kuwatoa wapangaji na mama mwenya nyumba. Toka wakati huo familia hiyo ipo nje. Mvua ikinyesha ni yao, jua pia ni lao. wanatia huruma sana. Cha kushangaza nimesikia hata fedha za kuuza nyumba hiyo mama huyo alikataa kuzipokea.

Na mwisho ni kwamba hata wakati wa kesi huyo mama alikwa haendi hata mahakamani hadi hukumu ilipotoka.

Je familia hiyo isaidiweje?
 
Nenda pale Legal and Human Rights Centre pale Magomeni Usalama au nenda pale kituo chao cha Buguruni...! Wao hutoa msaada wa sheria buree kabisaa....! Au nenda pale NOLA hapo mwenge karibia na HOngera Bar (bamaga) Nao pia hutoa msaada wa sheria bure kabisaa....!
 
Back
Top Bottom