Uuzaji na ukodishwaji maeneo ya barabarani

dumbi

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
989
1,523
Habari wana jamii,leo ningependa kuwashirikisha wahusika hili swala kama hawalifahamu au labda wameamua kulifumbia macho.

Kumekuwa na tabia ya watu kuwahi maeneo ya barabarani sehemu tofauti au eneo kubwa kwa ajili ya biashara almaarufu kama machinga wakiwemo na viongozi wa serikali za mitaa na kuuza maeno hayo au kukodisha kwa wananchi wenye shida nayo.

Zile meza mnazoziona barabarani wakina mama wakiuza matunda au samaki baadhi yao wamekodishwa kwa kiasi cha shiling elf2 kwa siku au wengine wanataka kwa mwezi elf 60.

Ukitaka hilo eneo liwe la kwako bila kulipa kodi bei inaanza laki 6 ikishuka kidogo sana! kwa pembezoni mwa mji, kwa Kariakoo eneo la kununua bei inaanza Mil 1.5 kushuka chini, na hili swala likibarikiwa na baadhi ya viongozi wa serikali za mtaa na viongozi wa machinga.

Kwa hiyo kuna watu wamefanya kama mitaji yao wana maeneo 3 au zaidi wakichukua kodi kwa wanyonge kila siku au kwa mwezi.

Ushauri wangu wanohusika na maeneo hayo wafanye ukaguzi kwa watu wanaomiliki maeno mengi wanyang'anywe na kuwagawia ambao hawana kabisa, huo ni unyonyaji haiwezekani umkodishe mtu eneo la barabara wakati ni la bure.
Kama huku chini mnajilimbikizia mali ambazo sio za kwenu vipi huko juu hali ikoje?

Kwa anaetaka kujua hili swala kiundani afanye research nje ya mji kwanza kama Gongo la Mboto, Mbagala nk kisha aende town

Sio wote waliopo barabarani wamekodishwa nieleweke hapo.asante.
 
Nitafutie muuzaji mmoja mkuu Kariakoo au sehemu yoyote nzuri.
Mimi sio dalali na sikubaliani na watu kuuziana sehem za barabarani ila ukihitaji zipo nyingi ni mfuko wako na unahitaji kwa biashara gani.
 
Mimi sio dalali na sikubaliani na watu kuuziana sehem za barabarani ila ukihitaji zipo nyingi ni mfuko wako na unahitaji kwa biashara gani.
Nikutanishe Na Dalali Au Pm Contact Zake.
Bidhaa Viatu, Mavazi, Urembo & the likes
 
Back
Top Bottom