Uuuwii!!Kumbe Tanzania Mfungwa Anapata Huduma Bora Kuliko Mtumishi Wa Serikali!!

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
956
120
Heri uwe Mhalifu kuliko kuwa raia mwema. Hii imethibitika jana bungeni wakati wa mawasilisho ya bajeti mbadala ya Ofisi ya Rais, Menejiment na Utumishi wa Uma iliyowasilishwa na Bi Suzan Lyimo.
Ikiwa Mtumishi wa uma wa kima chini analipwa mshahara wa Tsh.135000/- per month hii ni sawa na kutumia Tsh.750/- per day kwa familia yenye watu 6(yaan Baba, Mama, Watoto 4) wakati mfungwa mmoja bajeti yake ni Tsh.2400/- per day.
Inauma sana. Hakika Sisi Watanzania Tumelaaniwa.
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa hizo ni figa za kwenye makaratasi hali halisi inaonyesha hivyo ndio suala la kujiuliza. Isije kuwa mfungwa anambulia Tshs 400 out of Tshs 2400 inayotamkwa.
 
Mimi kila siku naumia kichwa. Hivi mfanyakazi anayelipwa Tsh.135000/- per month anamudi vipi kuishi na familia hapa mjini?

Usafiri
Chakula
Umeme
Maji
Kodi ya nyumba
Ada
n.k
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa hizo ni figa za kwenye makaratasi hali halisi inaonyesha hivyo ndio suala la kujiuliza. Isije kuwa mfungwa anambulia Tshs 400 out of Tshs 2400 inayotamkwa.
Potelea mbali kama hiyo 2400 mfungwa inamfikia au lah lkn kwenye bajeti hizo pesa si zinatengwa!! kutotumika 2400 yote kwa mfungwa hiyo ni kesi nyingine ya uadilifu wa viongozi sisi tumfikirie mwalimu anayefundisha shule za kata tena umasaini ambako hata maji unafuata km 10, Ardhi ina
 
Mimi kila siku naumia kichwa. Hivi mfanyakazi anayelipwa Tsh.135000/- per month anamudi vipi kuishi na familia hapa mjini?

Usafiri
Chakula
Umeme
Maji
Kodi ya nyumba
Ada
n.k

Kwa hili lazima afanye makeke sehemu au kazini ili avuke.
 
Hizo ni takwimu ridisha, maisha ya mfungwa wa tanzania ni duni sana kiasi kwamba mara baada ya kumaliza kifungo ni kama mtu aliyepunguziwa siku za kuishi.
 
Kajaribu huko jela uone kamaa wana raha hizo, achana na takwimu (PROPAGANDA) fuata ukweli maisha ya Jela ni balaa kabisa. Ni kweli kima cha chini kinabidi kiongezwe ili kukidhi gharama za maisha inatosha hakuna haja ya kufananisha namaisha ya Jela.
Heri uwe Mhalifu kuliko kuwa raia mwema. Hii imethibitika jana bungeni wakati wa mawasilisho ya bajeti mbadala ya Ofisi ya Rais, Menejiment na Utumishi wa Uma iliyowasilishwa na Bi Suzan Lyimo.Ikiwa Mtumishi wa uma wa kima chini analipwa mshahara wa Tsh.135000/- per month hii ni sawa na kutumia Tsh.750/- per day kwa familia yenye watu 6(yaan Baba, Mama, Watoto 4) wakati mfungwa mmoja bajeti yake ni Tsh.2400/- per day.Inauma sana. Hakika Sisi Watanzania Tumelaaniwa.
 
Tatizo hapa ni kuwa hakuna mtu ambaye ni mkweli- kila mmoja ni msanii, mf. mwajiri anajifanyya aanalipa mshahara mzuri wa shilingi 135,000 kwa mwezi na hapohapo mfanyakazi anajifanya ni mchapa kazi, magereza wanajifanya wanatumia shilingi 2,400kwakila mfungwa kwa siku na mfungwa naye anajifanya anaridhika . Ni mlolongo mrefu wa kufanya kiini macho.
 
135,000/30 =4500 otherwise lbd huo mwezi uwe na siku 180 ndo itakuwa sawa na 750 per day!Ila point yako bdo nzito kwa maslahi ya taifa!
 
asee usijidanganye .nji hii hata misaada inaishia kwenye matumbo ya watu seuse huyo mfungwa anayekabwa,nakushaur usifanye baya lolote ukidhani umwelani kuna nafuua, maharagwe na maunga yaliyooza na wanalishwa wenzio loool,wala usijaribu kuionja sumu mwana
 
Back
Top Bottom