Uupate utajiri na faida za ulimwengu zote, afu uende motoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uupate utajiri na faida za ulimwengu zote, afu uende motoni!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwana wa Mungu, Nov 14, 2008.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jamanieee, itamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, apate raha zooote hapa duniani halafu akaishie kwenda jehanum ya moto wa milele?je, itamfaa nini mtu, labda kaambiwa na mganga aue watoto wake, auwe albino, achune ngozi,akate watu viungo vya siri n.k, je, akiupata ulimwengu wooote, halafu mwisho wa siku akaishia kwenda kuungua moto jehanum ya milele? toka tumezaliwa hapa bongo tunasikia vitu hivi, watu wanauwa watoto wao ili wapate mali,cheo etc. watu wanaua albino, watu wanachuna ngozi,atu wanakata viungu vya siri, watu wanaua wenye vipara. hata hatujui who is next now? hivi jamani, sijui which group is gonna be a victim baada ya hapa, sijui wataanza kuwauwa watu warefu, sijui watu wafupi, sijui watu wanene, sijui watu wembamba, au sijui watakuwa wanawaua watu wenye kitu gani, hata hatuelewi sasa.

  Ila cha kujua ni kwamba, mwivi(shetani), mara zote huwa anakuja ili auwe, achinje na kuharibu, hivyo hiyo ni kazi yake shetani, na haitakwisha kwasababu shetani hajakufa. kikifa hiki, ataibua kingine. cha muhimu tu, watu ni kuchagua tu, wawe upande wa nani?upande wa shetani au wa Mungu. na, watu wanatakiwa wachague style ya maisha yao, waishi kishetani ambaye mwisho wa siku atawachinja?, au waishi kiMungu ili walindwe na Mungu. Uamuzi ni wenu wakuu. wasalam.
   
Loading...