Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 17,348
- 32,984
Wamemtumbu kwa sababu maendeleo hayana chama. Ila Iringa Manispaa ina chamaAliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa leo amekabidhi ofisi na gari mbele ya mkurugenzi wa manispaa hiyo na watumishi wote wa manispaa.
Kimbe amesema ameachia madaraka ya umeya kwa moyo mweupe ili vikao vya baraza la madiwani viendelee kufanyika na wananchi kupatiwa maendeleo. Kimbe amewataka watumishi wa Manispaa kutosikitika kwa yaliyotokea na badala yake waendelee kuchapa kazi kwa bidii.
Mkurugenzi wa Manispaa amesema wamesikitika sana kumpoteza Meya mwenye maono na aliyekuwa mchapa kazi haswa. Mkurugenzi amesema wataendelea kuifanyia kazi na kuikamilisha mipango yote makini iliyoachwa na Kimbe.
Source Eatv habari!
My take; Kama Kimbe ni mchapa kazi kwanini mmemtumbua?!!