Uungwana: DC wa Iringa Mjini, Richard Kasesela aomba radhi kutokana na kuteleza kwa ulimi wake

Kusamehewa ni wajibu, nami nimeshasamehe kabisa...

Lakini kanuni ya msamaha haihusiani na mtu kutowajibika kwa kubeba athari za tabia au matendo yake maovu...
Kwa manufaa ya imani zetu za dini tumekusamehe na kwa manufaa ya taifa ondoka ofisini ili vijana wetu wajifunze kutoka kwako kuwa ofisi ya umma ni sehemu takatifu.
 
Tusi ni neno lolote ambalo huwezi kumwambia mama yako au baba yako au unayemheshimu.
Hii ni definition yako ya tusi?Kwa hiyo unanilazimishia definition yako ya tusi ndiyo iwe definition yangu pia?Wewe ni nani hata utoe definition ya tusi kwa niaba ya watu wengine wa dunia hii?Yaani unanisukumizia hisia zako za maana ya tusi ndiyo iwe definition ya tusi?

Hata kumwambia mtu "macho yako" "kichwa chako" ni tusi.
Hiki kipimo chako kwamba kumwambia mtu "macho yako" au "kichwa chako" ni tusi umekitoa wapi?Yaani umetoa wapi hii SI unit ya tusi?Wewe ndiye kipimo?

Wewe ndiye unaamua kwa niaba ya watu wengine hapa duniani kuwa hili liwe tusi na lile lisiwe tusi?Yaani unataka tukutumie wewe kupata definition ya tusi?Wewe umekuwa nani kwani?
 
Huyu atumbuliwe tu. Hii nchi ina vijana wengi majobless kabisa.. huyu anapata ajira anaichezea. Atumbuliwe apewe nafasi kijana mwingine jobless.

Halafu point yangu kila siku naomba hizi teuzi watu wawe wanatuma CV na interview inapigwa ndio watu wanateuliwa. Hii ingesaidia kidogo kupinguza mijitu ya hivi.
 
Huyu Mkuu wa Wilaya, Kasesela anasubiri kutenguliwa badala ya kujiuzulu mwenyewe?

Anampima Mama kama ana masikio yanayosikia na macho ya kuona matusi aliyoyasema hadharani?

Kosa lile la kutukana hadharani linastahili kusamehewa? Lile ni kosa la jinai
Na tena katukana kwa msisitizo zaidi ya mara tatu .Hakuna kiongozi hapo just rubbish.
 
Halafu kutuliza matako ina maanisha nini?Huyo aliyekuwa anabishana naye alikuwa anatumia matako kubishana naye au mdomo! Sasa tako linahusikaje hapo?
 
Urithi wa kujimwabafai walioachiwa na marehemu Jiwe utawatesa Sana chawa wake .
Screenshot_20210425-193513.png
 
Kwani Tanzania nzima Mtu anayetakiwa Kuteuliwa katika Uongozi sehemu mbalimbali ni DC Jokate Mwogelo pekee? Acha ( Acheni ) Unafiki na kuendeleza Maslahi yenu na Kujipendekeza kwa Wakubwa nchini.
Kwani tatizo lako nini mimi nimetoa maoni yangu kumuomba Rais mama samia kwani wewe ni Rais mama samia?
 
Binafsi nimemsikiliza na nimeamua kumsamehe bila masharti yoyote na nawaomba wadau wote wa JF mumsamehe.

Ulimi hauna mfupa.

Zaidi soma: Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesela amtukana dereva bajaji mbele ya vyombo vya habari

View attachment 1764033

Big UP Kasesera, huo ndio uungwana!
Ni utamaduni mgeni katika miaka ya karibuni, kwa kiongozi kuomba radhi kwa makosa yasiyopendeza katika jamii, na Kasesera kaonyesha njia.
Siyo wale wanajiona wanajua kila kitu.
 
Big UP Kasesera, huo ndio uungwana!
Ni utamaduni mgeni katika miaka ya karibuni, kwa kiongozi kuomba radhi kwa makosa yasiyopendeza katika jamii, na Kasesera kaonyesha njia.
Siyo wale wanajiona wanajua kila kitu.
Naam, naunga mkono hili la kuomba radhi.
JPM alikuwa hana tabia ya kuwa na remorse au kuomba radhi kwa yale aliyowakera wananchi wake, mifano iko mingi:
Korosho
Uvunjaji nyumba Ubungo
Kuwapiga shangazi zao....
Kwani Bukoba tetemeko limeletwa na serikali....
Sitasomesha wazazi

Mifano hii ni ya kusikitisha kidogo, na ni wengi waliokwazika, hasa yule Kimaro wa Ubungo aliyeambiwa aache mav.i yake nyumbani!!
 
Asamehewe, kwani na yeye ni Binadaamu kama walivyo binadaamu wengine.

1. ni kawaida kabisa binaadamu akikasirishwa naye anaweza kukasirika na kutoa neno au tusi bila kutegemea.

2. Presure ya kazi na haswa jambo alilo kuwa analishughulikia linaweza pia likamfanya ashindwe kuvumilia.

kweli ni kiongozi lkn pia tusisahau naye pia ni Binadaamu sio malaika.

kweli kateleza kwa bahati mbaya, asihukumiwe kwa kosa moja, tukumbuke mazuri mengi aliyo yafanya.

tunaomba asihukumiwe wala asiadhibiwe kwa bahati mbaya iliyo tokea.
tumsamehe bure.
kila binadamu anaweza kughadhibika, hakuna mkamilifu, sio tabia yake,
 
Fukuzaaa huyu, Sabaya na Chalamila, hawa wa kufukuza kabisa, wanajifanya miungu watu hawa.
 
Back
Top Bottom