JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,458
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amemwambia mwenzake Volodymir Zelensk wa Ukraine kwamba taifa lake lipo tayari kutoa kila usaidizi katika mchakato wa majadiliano kati ya Urusi na Ukraine.
Ofisi ya Rais ya Uturuki imesema ahadi hiyo imetolewa wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu baina ya viongozi hao.
Erdogan amesema uokozi wa majeruhi na raia katika Mji wa Mariupol lazima uhakikishwe. Katika mazungumzo hayo kiongozi huyo wa Uturuki aliongeza kwa kusema taifa lake linajiweka katika dhamana ya msingi wa usimamizi mzuri wa suala hilo.
Ukraine imekuwa katika jitihada ya kusaka hakikisho la kiusalama kutoka kwa mataifa mbalimbali wakati wa mazungumzo.
Source: DW