Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,133
- 10,843
Serikali ya raisi Tayep Erdogan imejiondoa rasmi kwenye mkataba wa kimataifa unaotaka kuwalinda wanawake dhidi wa matendo ya udhalilishwaji. Hatua hiyo imetajwa kuwa ni ushindi mkubwa wa viongozi wahafidhina wa chama cha AK kinachoongozwa na Rais huyo wakishutumu mkataba huo kama kichocheo cha talaka nyingi nchini humo na pia kuhamasisha ndoa za jinsia moja baina ya wanawake na wanawake.
Kwa mujibu ya wahafidhina hao wa AK nchi hiyo ina sheria nyingi katika wizara tofauti ambazo zinatosha kuwalinda wanawake na jamii nyengine dhidi ya udhalilishwaji.Pamoja na sheria hizo mahakama nazo zimetengeneza kifaa cha kielektronik cha kuwafuatilia wakosaji sugu wanaowadhalilisha wanawake.
Chama cha upinzani cha CHP tangu ulipoanza uvumi wa nchi hiyo kujitoa kimekuwa kikiwahamasisha wanachama wake kuandamana kupinga uamuzi huo kwa madai kuwa kujitoa kwa nchi hiyo kutoka mkataba wa kuwalinda wanawake kutaongeza vitendo vya kudhalilishwa kwa wanawake pamoja na mauwaji dhidi yao.