Uturuki waanza mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa Syria

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,352
Uturuki imesema, imekamilisha maandalizi ya mashambulizi Kaskazini mwa Syria, baada ya ishara zenye mkanganyiko za Marekani kuhusu iwapo itaruhusu operesheni ya kijeshi

Uturuki imesema, imekamilisha maandalizi ya mashambulizi Kaskazini mwa Syria, baada ya ishara zenye mkanganyiko za Marekani kuhusu iwapo itaruhusu operesheni ya kijeshi.

Haya ni baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuamuru vikosi vyake kuondoka katika eneo la mpaka wa Syria.

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan, ametishia mara kadhaa kuwashambulia wanamgambo wa Kikurdi katika eneo la mpaka Kaskazini mwa Syria.

Hii ni kutokana na uhusiano wa wanamgambo hao na watu wanaotaka kujitenga chini mwake. Wizara ya Ulinzi ya Uturuki, ilitoa taarifa ya kukamilika kwa maandalizi ya mashambulizi Kaskazini mwa Syria kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Awali, Rais Erdogan alisema mashambulizi hayo ya kijeshi yanaweza kufanyika wakati wowote bila kutoa ilani. Hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump, ya kuviondoa vikosi vyake Kaskazini mwa Syria imekosolewa vikali na wakosoaji wanaoiona kama kuviacha vikosi vya Wakurdi ambavyo vimekuwa mshirika muhimu katika mapambano dhidi ya kundi linalojiita dola la Kiislamu IS.

Tangazo la Trump la kuviondoa vikosi vyake limepata pia upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa chama cha Democratic pamoja na chama chake cha Republican wakionya kuwa shambulio lolote la Uturuki litasababisha mauaji ya halaiki ya Wakurdi ambao wanawashikilia wapiganaji wa kundi la IS pamoja na familia zao.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa Uturuki Fuat Oktay amemjibu Trump hii leo akionya kuwa Taifa lake halitojibu mapigo kutokana na vitisho.

Amesema, kama ambavyo Rais Erdogan husisitiza, Uturuki itashika njia yake na kushughulikia mambo yake yenyewe. Uturuki inasema, inataka eneo salama Kaskazini mwa Syria ili lisiwe maficho ya vikosi vya Kikurdi na kuruhusu karibu wakimbizi milioni mbili wa Syria kurejea nyumbani.

Wakati huohuo, Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Uturuki, yamewalenga wanamgambo wa kikurdi Kaskazini mwa Iraq katika maeneo ya Hakurk na Hafta. Hayo ni kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Uturuki na kwamba "magaidi" tisa wameuawa katika tukio hilo.

UPDATE
Ndege za Kivita za Uturuki zimeshambulia baadhi ya sehemu za Kaskazini mwa Syria hatua inayotarajiwa kuleta mgogoro dhidi ya Wanamgambo wa Kikurdi wenye ushirikiano na Marekani

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema operesheni hiyo ni kwa ajili ya kutengeneza eneo salama lisilo na Wanamgambo wa Kikurdi litakalowapa makazi Wakimbizi wa Syria

Kwa mujibu wa Majeshi ya Kidemokrasia ya Kikurdi ya Syria, maeneo yanayokaliwa na raia yalishambuliwa na ndege za Kijeshi za Uturuki huku Majeshi ya ardhini ya Uturuki yakiwa yameshavuka mpaka kuingia Syria

Operesheni hiyo imekuja siku chache baada ya Rais Trump kuondoa Vikosi vya Kijeshi Kaskazini mwa Syria baada ya kufanya mazungumzo na Rais Erdogan hatua ilipingwa vikali na Wadau mbalimbali

Wanajeshi wa Kikurdi ambao ni washiriki wa Marekani katika kupambana na Kindi linalojiita Dola ya Kiislamu (IS) nchini Syria, wanawalinda maelfu ya Wapiganaji wa IS na ndugu zao katika magereza na maeneo maalumu na sasa haieleweki kama wataendelea kulindwa
 
Kuna mchongo unatengenezwa hapo. Turkey should be careful, maana alipoambiwa ajianda kwenda kushika doria kaskazini mwa Syria, pi alionywa kuhusu kutowagusa hao Wakurd kwa namna yoyote ile.
Huu mtego Uturuki hataukwepa na hapo ndiyo sehemu za nchi za Syria, Irak na Uturuki lazima zitamegwa ili kuunda nchi ya Wakurdi.
 
Uturuki hawezi ruhusu jambo kama hilo hata kidogo.
 
Kuna mchongo unatengenezwa hapo. Turkey should be careful, maana alipoambiwa ajianda kwenda kushika doria kaskazini mwa Syria, pi alionywa kuhusu kutowagusa hao Wakurd kwa namna yoyote ile.
Huu mtego Uturuki hataukwepa na hapo ndiyo sehemu za nchi za Syria, Irak na Uturuki lazima zitamegwa ili kuunda nchi ya Wakurdi.
Anaetaftwa mturuki na alishagundua zamani sana kama yy ndio main target

Ila sidhanii kama turkey anaweza kubali jambo kama hili lakuundwa nchi ya kikurdi litokee

Halaf hawa waturkey sijui wana historia gan ya kiuhasama na hawa wakurdi maana long tyme sana aseee naona hawapikiki chungu kimoja kama Ngamia Na Mdudu
 
ugomvi wao ni kuwa Wakurdi wanataka kujitenga tu. Hamna chochote. Ni kama vile Catalonia kule Spain tu ila hawa wakurdi wana silaha.
 
Screenshot_20191009_165212_com.android.chrome.jpg
 
President Recep Tayyip Erdogan says his country's military has begun a long-planned incursion into northern Syria to take out Kurdish forces branded by Ankara as terrorists, but viewed by much of the West as key partners in the fight against Islamic State

The military operation began Wednesday, days after a surprise White House announcement that U.S. forces would withdraw from the region.

President Donald Trump is continuing to defend his decision, amid widespread criticism, saying the "stupid endless wars for us are ending!"

"Fighting between various groups that has been going on for hundreds of years. USA should never have been in Middle East. Moved our 50 soldiers out. Turkey MUST take over captured ISIS fighters that Europe refused to have returned. The stupid endless wars, for us, are ending!," Trump said Wednesday, in a series of tweets on the matter.

The U.S. announcement of a troop pullout from northern Syria, paving the way for the Turkish military operationagainst a Kurdish militia in the area, has been widely criticized by both Democrats and Republicans. Lawmakers have said the U.S. would be abandoning Syrian Kurds who had fought the Islamic State terror group alongside U.S. troops.

VOA
 
Anaetaftwa mturuki na alishagundua zamani sana kama yy ndio main target

Ila sidhanii kama turkey anaweza kubali jambo kama hili lakuundwa nchi ya kikurdi litokee

Halaf hawa waturkey sijui wana historia gan ya kiuhasama na hawa wakurdi maana long tyme sana aseee naona hawapikiki chungu kimoja kama Ngamia Na Mdudu
Tangu miaka ya themanini Kurds walipotaka kupindua serikali.
Ndani ya Uturuki ni marufuku kabisa hata kuzungumza lugha ya ki kurd. Ukisikika unazungumza ki kurdi ni zaidi ya jinai, unachukuliwa kama mhaini na mamlaka za Uturuki
 
Kuna mchongo unatengenezwa hapo. Turkey should be careful, maana alipoambiwa ajianda kwenda kushika doria kaskazini mwa Syria, pi alionywa kuhusu kutowagusa hao Wakurd kwa namna yoyote ile.
Huu mtego Uturuki hataukwepa na hapo ndiyo sehemu za nchi za Syria, Irak na Uturuki lazima zitamegwa ili kuunda nchi ya Wakurdi.
Mkuu huijui vizuri turkey itakua,yan ardhi ya turkey ikatwe apewe mkurdi!
 
mimi nilisema,marekani ni mnafiki,ameona uturuki hanunui silaha kwake,ili kujipendekeza kawatosa wakurdi ili mturuki awashambulie,ili kurudisha urafiki na uturuki,,USA sio rafiki wa kweli.
Mkuu hizi habari .nadhani umezitoa kichwani mwako..suala lililopo kuwa Uturuki inawaona SDF na YPG kama magaidi( wana mifungamano na PKK) na wakati huo Marekani inawatumia hao wakurd katika vita dhidi ya IS .
Sasa urafiki wa Marekani na Wakurd ilikuwa ni kwa ajili ya operation dhidi ya IS na si vita dhidi ya Jturuki( kwa ushahidi msemaji wa Wakurd leo ameweka wazi)...
Uturuki inawaona YPG&SDF kama magaidi kutokqna na sababu za kisiasa..wakati Marekani nayo Inawaona IS,THS,na Miongoni mwa TFSA kama magaidi au wengine ni Moderate.
Ndio Maana SDF &YPG wana uadui na TFSA na hao Wanaojiita National army(including FSA) lakini hawana uadui Sana na Assad Government...
Mkuu hii operation ni kwa mujibu wa Sasa z Utuuki na si zaidi kama unavyotaka kutuaminishq...

Lejea operations za nyuma za u
Uturuki nchini Syria ( olive branch na Euphrate shield) hata hao unawaamini Russia walijarubu kutaka kuwazuia ila wakaghaili na kuwa acha Uturuki free.

Soma zaidi ..kuliko kutoa perception zisizo na ushahidi..
 
ugomvi wao ni kuwa Wakurdi wanataka kujitenga tu. Hamna chochote. Ni kama vile Catalonia kule Spain tu ila hawa wakurdi wana silaha.
Suala la wakurdi kua na silaha wala sio labahati mbaya na ndio turkey ana pambana kwa kila namna na hao jamaa yaani kwa mali na hali
 
Back
Top Bottom