Uturuki na Irani hawaoni ndugu zao wanavyouawa Palestina, kwanini hawaingilii?

Leo ndio nimejua asee,sijawahi sikia wakimbizi wa Syria wakimbilia Qatar au wakimbizi wa Palestina wakimbilia Misri au Saudia... sidhani kama kuna kambi za wakimbizi pia. Jiulie pia kwanini Walibya badala ya kuvukia Misri wanakubali kufia bahatini kwenda Ulaya?

Wakimbizi wengi wa kiarabu wanakimbilia Ujerumani na Ugiriki pamoja na Uturuki kuwa karibu lakini wanaenda mbali dah!!🤔🤔

Naamini hata Afrika tuna nafuu kwa huruma na ujirani kuliko waarabu
Muarabu Lema kakimbilia kenya and then Canada
 
Ndio maana nimesema huu mgogoro si wakidini kama wengi wanavyo fikiri.
Huu mgogoro unarazimishwa uonekane kama wa kidini kwa maslahi ya mataifa fulani.
Kumbuka ndani ya jeshi la Israel kuna waislamu na wao ni washiriki wa moja kwa moja kwenye mashambulizi dhidi ya wapalestina.
Wakati upande wa wapalestina kuna mamilion ya wakristo ambao wana teseka na kuuawa kutokana na mashambulizi ya Israel.
Kwa hiyo ww kama ni mkirsito na unasapoti kile kinacho fanywa na Israel dhidi ya wapalestina basi tambua miongoni mwa wanao teseka na ukatili wa Israel ni wakristo wenzio.
Wakristo wengi wanasapoti taifa la Israel kwa sababu ya kiblia. Ila hawasapoti wakristo walioko Israeli wala wayahudi. Wanaihudu tu Israeli kulingana na mwongozo wao wa biblia.
 
Wakristo wengi wanasapoti taifa la Israel kwa sababu ya kiblia. Ila hawasapoti wakristo walioko Israeli wala wayahudi. Wanaihudu tu Israeli kulingana na mwongozo wao wa biblia.
Kwahiyo mungu amehalalisha mauji dhidi ya watoto yanayo fanywa na Israel?
 
Waafrika ni watu waliochanganyikiwa dini zimewavuruga hawalalamiki magaidi wa Mozambique
 
Nchi za waarabu ziliungana kuishambulia Israel, unakumbuka kilichowapata?
Na hapo ndipo nchi nyingi za kiisram zinazoizunguka Israel zikasain mkataba wa kutoishambulia au kufanya vita na Israel. Ya kwanza ikiwa Misri. Zilizobakia kusain kipindi hicho ikiwemo Uarabuni,wamesain hivi karibuni. Na kwenye huo mkataba ni kuna vipengere hakutakuwepo vita kati yao. Vile vile nchi mojawapo ikiwa na vita na nchi nyingine,nchi mojawapo kati ya hizo zilizo kwenye huo mkataba isiingilie hiyo vita. Ni kama sasa uarabuni lazima wawe kimya kufuatana na mkataba waliosain,wamefungwa mikono na miguu. Israel akili kubwa sana wale watu.
 
Kwa tafsiri hii inaonekana ni wabinafsi sana, naskia hata wakimbizi wa kipalestina wamenyimwa uraia kwenye nchi za kiarabu?
Huwezi pewa uraia Uarabuni nilikua na msela wangu msryia babu yake alizaliwa Kuwait mpaka yeye amezaliwa Kuwait ila hawajapewa uraia wa kuwait
 
Huwezi pewa uraia Uarabuni nilikua na msela wangu msryia babu yake alizaliwa Kuwait mpaka yeye amezaliwa Kuwait ila hawajapewa uraia wa kuwait
Asee wao ndio wanaharibu maana ya uislamu sasa. Kwa mujibu wao uislamu ni undugu
 
Baada ya hao wanao jiita Waizrael ( mimi nawatambua kama Walowezi kutoka maeneo mbalimbali ya Ulaya na Marekani) kujipenyeza Palestina iliyokuwa ikikaliwa na Waarab kwa miaka mingi na kujitangazia Uhuru wao mwaka 1948 chini ya Waziri Mkuu wa Kwanza David Ben Gurion!

Baada ya kuzaliwa kwa Taifa la Israel, mkakati wa kuyachukua maeneo ya wenyeji kwa nguvu ili kuwapatia Walowezivwa Kiyahudi, ulipamba moto! Waarab (Wapalestina) ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa hilo eneo, walipambana dhidi ya Wavamizi kwa miaka mingi, na kuishia kushindwa!

Kulikuwa na vita mwaka huo huo wa 1948, 1956, 1967, 1973, mpaka leo hii bado hali si shwari. Na katika vita hivyo, kuna nyakati ambapo nchi za Kiarab kama Misri, Syria, Lebanon, Iraqi, Iran, nk ziliisaidia Palestina! Lakini mwisho wa siku wote walishindwa na hao Waizrael!

Na ndiyo kipindi hicho baadhi ya nchi kama Misri, ziliamua kuingia makubaliano binafsi na Israel kupitia Makubaliano yaliyofanyika eneo la Camp David Marekani na kuongozwa na Rais wa kipindi hicho Jimmy Carter, na hivyo Misri kujitoa rasmi katika uhasama na Israel mtoa roho.
Israeli ni USA na Europe in disguise. Waliunda alliance kukabiliana na mataifa ya kiarabu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

basically izo nchi zilipigana na USA na washirika wake kwa mwamvuli wa Israel. Toka lini kataifa ka watu million 5 kazishinde nchi zaidi ya 3 tena zilizo vizuri kijeshi?

Harafu kina sisi, kina matayo wa vingunguti na buza. Tunaaminishwa, Israel ni taifa linalolindwa na mungu.
 
Acha upumbavu na uongo ni waarabu au waislamu wapi wasio wasaidia wakimbizi?

Haya tende na takwimu.

(1) Jordan inawahifadhi zaidi ya wakimbizi wa kiSyria million 1.5 ,ambao ni sawa na wakimbizi wote walioko katika nchi zote za ulaya.

(2) Uturuki inawahifadhi wakimbizi zaidi ya million 3.
(3)Rebanon inawahifadhi wakimbizi million 1
(4) Iran inawahifadhi zaidi ya wakimbizi zaidi ya million 2 wa kiafughastan.

(5) nchi kama saudia,Qatar,UAE kuna wakimbizi zaidi ya laki 8 wa kiSyria sema wao hawaishi kwenye makambi bali wamejichanga kwenye maisha ya kawaida nadhani hata ujerumani wamefanya kitu kama hicho.

Taifa la kizungu linalo hifadhi wakimbizi wengi ni ujerumani tu ikiwa na wakimbizi million 1.
Nchi zote za kizungu zilizo baki ukiziunganisha zina wakimbizi wa kiSyria wasio zidi 500,000.

Sasa sijui unazungumzia waislamu na waarabu wapi mkuu?
anasubiri takwimu za CNN na BBC huyo mkuu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom