Uturuki na Irani hawaoni ndugu zao wanavyouawa Palestina, kwanini hawaingilii?

Mkuu Waarabu walishaungana mara nyingi kuipiga Israel lakini hawajafanikiwa! Mwaka 1956,1967,1973 hawajawahi kuishinda Israel,labda ukiondoa vita vya mwaka 2006 ilipopambana na Hezibollah!
Hatimaye waliishia kugawanyika na wengine wakirudisha uhusiano na Taifa hilo dogo!
Irani inajitahidi na nadhani ndiye anayefadhili vikundi vya Hezibollah na Hamas lakini bado ni shughuli pevu kupambana na Taifa hilo dogo.
Mkuu tupe madini kwa nini israel inaonekana ni Taifa dogo lakini linakuwa na nguvu kuzishinda hizo nchi zingine zilizo ungana???? kuna siri gani kwa israel kuwa na nguvu hivyo??? tunaomba Elimu mkuu
 
Unatuokota sio.
Screenshot_20210514-212505.png
 
Walijaribu hapo kabla kuungana, kwa bahati mbaya hawakuwa na maandalizi mazuri! Na hivyo kuishia kupigwa na hayo Mazayuni.

Ila umeshawahi pia kujiuliza hayo makombora wanayo tumia hao Wanamgambo wa Hamas na Hezbollah, na wale wa Yemen yanatoka wapi?
... kuna ule umoja wao wa kidugu oic sijui uliishiaga wapi ule; hausikiki tena. Au kwa kuwa ma-sponsor akina Ghadafi hawapo tena?
 
Mkuu Waarabu walishaungana mara nyingi kuipiga Israel lakini hawajafanikiwa! Mwaka 1956,1967,1973 hawajawahi kuishinda Israel,labda ukiondoa vita vya mwaka 2006 ilipopambana na Hezibollah!
Hatimaye waliishia kugawanyika na wengine wakirudisha uhusiano na Taifa hilo dogo!
Irani inajitahidi na nadhani ndiye anayefadhili vikundi vya Hezibollah na Hamas lakini bado ni shughuli pevu kupambana na Taifa hilo dogo.
Uturuki hana ubavu wa kukanyaga pale kuisaidia Palestina! Juzi juzi Edogan alisikika akimwomba Putin wa Russia kuungana ili kuiadhibu Israel.Russia hawajatoa na wala wala hawatatoa jibu lolote!
Kihistoria kweli Israel imewapiga sana waarabu,lakini zama zimebadilika hawatakiwi kuogopa hivyo. Erdogan anaingilia migogoro mikubwa saivi tunaona. Alidungua mpaka ndege ya Urusi,kwanini anakuwa muoga? Shida ni silaha,mbinu au uchumi?
 
... kuna ule umoja wao wa kidugu oic sijui uliishiaga wapi ule; hausikiki tena. Au kwa kuwa ma-sponsor akina Ghadafi hawapo tena?
Unaambiwa usimtegemee sponsor, sponsor hufa🤣🤣☝️
 
una ushahd mzee au unajisemea tu kimhemko. ushawah kufika huko ukaona uhalisia? unajua baba yake wazir mkuu wa sasa ni mzawa halis wa hapo? ukiacha wayahud wa kuja unatakiwa kujua walikuwepo wayahud wazawa hapo.
Baba yake amezaliwa Poland na hata kama angekuwa amezaliwa hapo haiondoi uzungu wake( Benjamin Netanyahu ni mzaliwa wa hapo). Hao wanaojiita jews ni wazungu kuliko hata waitaliano. Haiingii akilini wakazi wa hilo eneo karibu wote waondoke alafu waje wazungu na ngozi nyeusi kutoka walikotoka wanakwambia wana asili ya hapo. Kama kuna mamia ya wayahudi waliondoka kweli( pia siamini) basi wengi wao wangekuwa maeneo ya karibu na hapo na sio ulaya wala Afrika.
 
Asee jamaa husomagi historia wewe
 
Leo ndio nimejua asee,sijawahi sikia wakimbizi wa Syria wakimbilia Qatar au wakimbizi wa Palestina wakimbilia Misri au Saudia... sidhani kama kuna kambi za wakimbizi pia. Jiulie pia kwanini Walibya badala ya kuvukia Misri wanakubali kufia bahatini kwenda Ulaya?

Wakimbizi wengi wa kiarabu wanakimbilia Ujerumani na Ugiriki pamoja na Uturuki kuwa karibu lakini wanaenda mbali dah!!

Naamini hata Afrika tuna nafuu kwa huruma na ujirani kuliko waarabu
Na wakifka huko wanaishi kwa amani kuzidi hata.makwao.
 
Israel anapambana na Hamas ni kakikundi kadogo sana ila anahangaika nako. Now kiongozi wa Hamas amesema kuishambulia ISRAEL kwao ni rahisi zaidi kuliko kunywa maji na wametangaza FULL WAR.
 
Baba yake amezaliwa Poland na hata kama angekuwa amezaliwa hapo haiondoi uzungu wake( Benjamin Netanyahu ni mzaliwa wa hapo). Hao wanaojiita jews ni wazungu kuliko hata waitaliano. Haiingii akilini wakazi wa hilo eneo karibu wote waondoke alafu waje wazungu na ngozi nyeusi kutoka walikotoka wanakwambia wana asili ya hapo. Kama kuna mamia ya wayahudi waliondoka kweli( pia siamini) basi wengi wao wangekuwa maeneo ya karibu na hapo na sio ulaya wala Afrika.
Unachoongea Hakina mantiki kabisa. Kwani kuna mtu anayewajua hasa waIsraeli halisi wa enzi hizo walikuwaje? Kuna mtu anadhani kuwa farao alikuwa mwarabu lakini Afrika nzima hapo swali ilikuwa imetawaliwa na waafrika, waarabu wamekula tu kwa kuangusha tawala za kiafrika na kujitwalia maeneo. Je wewe unajua wamisri wa swali wako wapi?

Kama hatujui wayahudi ama wapalestina wa swali walikuwaje basi hatuna uwezo wa kujua leo Nani ni nani? Kabla ya ukoloni hakukuwa na mipaka Wala nchi. Hata asili ya waingereza ni Ujerumani na nchi za scandinavia.
Kitu Cha MUHIMU ni kuheshimu uti. Na kuishi kwa fair (equity)not equal(equality).

Haya maneno hayasaidii wapalestina kufa. Cha msingi ni kuondoa mgogoro Ili damu isizidi kumwagika.
 
Kihistoria kweli Israel imewapiga sana waarabu,lakini zama zimebadilika hawatakiwi kuogopa hivyo. Erdogan anaingilia migogoro mikubwa saivi tunaona. Alidungua mpaka ndege ya Urusi,kwanini anakuwa muoga? Shida ni silaha,mbinu au uchumi?
Jiulize kwann anaogopa?
Kama silaha wanazo,sasa shida iko wapi?
 
Baba yake amezaliwa Poland na hata kama angekuwa amezaliwa hapo haiondoi uzungu wake( Benjamin Netanyahu ni mzaliwa wa hapo). Hao wanaojiita jews ni wazungu kuliko hata waitaliano. Haiingii akilini wakazi wa hilo eneo karibu wote waondoke alafu waje wazungu na ngozi nyeusi kutoka walikotoka wanakwambia wana asili ya hapo. Kama kuna mamia ya wayahudi waliondoka kweli( pia siamini) basi wengi wao wangekuwa maeneo ya karibu na hapo na sio ulaya wala Afrika.
binafsi nimefika karibu mara 5 hyo nchi na kwa kias nawajua. wako wayahud wazawa na wako wayahud waliotoka maeneo mbali mbali. hawa jamaa wametawanyika karibu nchi nying sana hasa za kiarabu. na cha kusikitika watu huwa hawawaongelei wayahud waarabu au waafrika au wahndi. wao ni hao Ashkenaz tu. bro hawa watu wanapigania vita ya ujima. kwamba wayahud walishapata kichapo huko nyuma kutoka iran wakatawanyika baadae baadh yao wakajipanga wakarudi. wakaja wakapewa tena kichapo na warumi baadh yao wakajikusanya wamerud hivi ninavyoongea nchi zote za kiarabu na persia pamoja na uturuk wapo wayahud wazawa. wote wametokana na mtawanyiko wa mara kwa mara. wako ulaya amerika australia nk. na unatakiwa kujua hawa jamaa ni kabila moja tu kati ya yale 12 yaliyokuwepo. yale mengine yalipotea. ndio hayo unayosikia myahud wa yemen nk. pia nilikuta kabila la wasamaria wapo hapo miaka yote. ibada zao ni kama wayahud ila wanajiita wasamaria. nilichokuwa najaribu kukuambia ni kuwa hawa watu wanajuana. ni kama vile cc wachagga huko nyuma sio kwamba uchaggan cc ndio waanzilishi mzee kuna watu walikuwa wanaitwa wakahe wazee waliwapa kichapo wakachukua eneo lao. ndio life lilikotokea. wazungu wameenda amerika wameua watu wakachukua ardh yao hvyo hvyo australia Akusin. nk. sasa wenyeji wakirud mnapambana anaeshinda ndio mwenye nchi ukishindwa ukajipange.shida iliyopo hil la israel limechukua sura ya dini. watu hawajui kuwa wapo wapalestina waislam na wakristo pia kadhalika na israel pia. japo wapalestina wengi ni muslm na waisrael weng ni Jew. so watu hawatak kungea ukweli.
 
Hawa wayahudi wa sasa hivi ni feki, hawa ni wazungu wanaojifanya wayahudi. Wamebumba DNA kuonekana wana asili ya hapo middle east. Wayahudi wa asili wanatakiwa wafanane na wairan, syria, lebabon(levantines). Na kuna ngozi nyeusi pia wanadai ni wayahudi, sijui lini wataacha huu ujinga wa kutaka asili isiyowahusu.
Kinachofanya useme kuwa wayahudi wanapazwa kufanana na waarabu ni kipi? Mbona wamoroko na wamisri ni tofauti? Au ?
 
Back
Top Bottom