Uturuki na Irani hawaoni ndugu zao wanavyouawa Palestina, kwanini hawaingilii?

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,290
2,000
Kila nikiangalia video kinachoendelea hapo Gaza nashangaa sana, Waarabu wako kimya kama hawaoni. Afu Waafrika na unafiki wa kulaani kwenye media, inasaidia nini sasa?

Hakuna mzozo utakaotikea Mashariki ya Kati uache kusikia Uturuki inaunga mkono upande fulani na kusaidia silaa tena umguse Mwislamu Uturuki haiwezi kunyamaza.

Azerbaijan imeishinda Armenia kwenye jimbo la Nagorno kwa msaada wa Kijeshi kutoka Uturuki

Iran iko vizuri sana kiuchumi na Kijeshi, imetoa misaada mingi sana kwa makundi kama Hezbollah.

Uislamu ni udugu, Wapalestina ni Waislam, kwanini hawatoi msaada kwa ndugu zao Palestina? Ina mana Israel inaogopeka kiasi hicho? Kinchi kidogo kiasi hicho hata Mkoa wa Kilimanjaro mkubwa?

Waarabu ni muda wa kujitambua sasa.
 
NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
11,265
2,000
Waarabu wasikie tu redioni

Jiulize kwani nchi mfano za waarabu kukitokea vita nchini kwao wanakimbilia nchi za wakristo ulaya na marekani hawaendi nchi za waislamu wenzao?

Hata Pemba kulipotokea vurugu walikimbilia Ulaya sio Omani au uarabuni
Duh,hii ni kweli tupu.
Itokee vita nchi za kiislamu Africa alafu ukimbilie Saudia kuomba ukimbizi,haaa haiwezekani bana'piga uwa,,haiwezekani,,,!!
 
Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,290
2,000
Waarabu wasikie tu redioni

Jiulize kwani nchi mfano za waarabu kukitokea vita nchini kwao wanakimbilia nchi za wakristo ulaya na marekani hawaendi nchi za waislamu wenzao?

Hata Pemba kulipotokea vurugu walikimbilia Ulaya sio Omani au uarabuni
Kwa tafsiri hii inaonekana ni wabinafsi sana, naskia hata wakimbizi wa kipalestina wamenyimwa uraia kwenye nchi za kiarabu?
 
Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,290
2,000
Walijaribu hapo kabla kuungana, kwa bahati mbaya hawakuwa na maandalizi mazuri! Na hivyo kuishia kupigwa na hayo Mazayuni.

Ila umeshawahi pia kujiuliza hayo makombora wanayo tumia hao Wanamgambo wa Hamas na Hezbollah, na wale wa Yemen yanatoka wapi?
Tujuze mkuu,hatujui
 
Amigoh

JF-Expert Member
May 15, 2016
863
1,000
Kila nikiangalia video kinachoendelea hapo Gaza nashangaa sana,waarabu wako kimya kama hawaoni. Afu waafrika na unafiki wa kulaani kwenye media,inasaidia nini sasa?

Hakuna mzozo utakaotikea mashariki ya kati uache kusikia Uturuki inaunga mkono upande fulani na kusaidia silaa tena umguse mwislamu Uturuki haiwezi kunyamaza.

Azerbaijan imeishinda Armenia kwenye jimbo la Nagorno ...kwa msaada wa kijeshi toka Uturuki

Iran iko vizuri sana kiuchumi na kijeshi, imetoa misaada mingi sana kwa makundi kama Hezbollah.

Uislamu ni udugu, Wapalestina ni waislamu, Kwanini hawatoi msaada kwa ndugu zao Palestina? Ina mana Israel inaogopeka kiasi hicho? Kinchi kidogo kiasi hicho hata mkoa wa Kilimanjaro mkubwa?

Waarabu ni muda wa kujitambua sasa.
Sisi tunausikaje uko dini zenyewe tumeletewa tu..

Niliwahi soma historia nikaone hizi dini zote Baba yao ni mmoja sema kinachoendelea hapo ni vita ya Ndugu wawili.. hiyo vita iposiku itaisha tu akili zikiwakaa vizuri
 
The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
13,536
2,000
Waarabu wasikie tu redioni

Jiulize kwani nchi mfano za waarabu kukitokea vita nchini kwao wanakimbilia nchi za wakristo ulaya na marekani hawaendi nchi za waislamu wenzao?

Hata Pemba kulipotokea vurugu walikimbilia Ulaya sio Omani au uarabuni
Hapo ndio huwa nashangaa.

Syria wanauawa kila siku badala kukimbilia Saudia ,Oman,qatar au Dubai fasta utasikia wako Canada na ujerumani

Kuna Yule binti wa Saudi alietaka uliwa na ndugu zake alietoroka kule Thailand saivi Yuko Canada na vimini ana vaa na bacon anakula

Daaah

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,290
2,000
Sisi tunausikaje uko dini zenyewe tumeletewa tu..

Niliwahi soma historia nikaone hizi dini zote Baba yao ni mmoja sema kinachoendelea hapo ni vita ya Ndugu wawili.. hiyo vita iposiku itaisha tu akili zikiwakaa vizuri
Sasa mmoja ana nguvu kuliko mwingine ndio shida,kama ndugu basi atoke mtu wa kuamulia
 
Masoktz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,380
2,000
Kila nikiangalia video kinachoendelea hapo Gaza nashangaa sana,waarabu wako kimya kama hawaoni. Afu waafrika na unafiki wa kulaani kwenye media,inasaidia nini sasa?

Hakuna mzozo utakaotikea mashariki ya kati uache kusikia Uturuki inaunga mkono upande fulani na kusaidia silaa tena umguse mwislamu Uturuki haiwezi kunyamaza.

Azerbaijan imeishinda Armenia kwenye jimbo la Nagorno ...kwa msaada wa kijeshi toka Uturuki

Iran iko vizuri sana kiuchumi na kijeshi, imetoa misaada mingi sana kwa makundi kama Hezbollah.

Uislamu ni udugu, Wapalestina ni waislamu, Kwanini hawatoi msaada kwa ndugu zao Palestina? Ina mana Israel inaogopeka kiasi hicho? Kinchi kidogo kiasi hicho hata mkoa wa Kilimanjaro mkubwa?

Waarabu ni muda wa kujitambua sasa.
Nani kakwambia Wapalestina ni Waislamu?Nani kakwambia hawawasaidii?Unataka Wapeleke Majeshi yao?Wameshawapa silaha na mfunzo.Mgogoro wa Israel na Palestine ni Mgogoro wa KIjima (Barbaric War) Wayahudi na Wapalestina wote ni wajima wakidai kwamba wenzao ni wavamizi wa eneo lao bila kuwa tayari kuishi pamoja.Hauna maslahi ya kiuchumi wala kisiasa katika Zama hizi ndo maana wengi wanaunga mkono kwa maneno na kwa nyuma ya Pazia.
 
uberimae fidei

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
2,077
2,000
Tukumbushe ndugu yangu wengine kipindi hicho walikua hawajazaliwa,wengine walikua jela n,k
Vita vya Siku Sita, pia vinajulikana kama Vita vya Juni, 1967 kati ya nchi za Kiarabu na Israeli, au Vita ya Tatu vya Waarabu na Israeli, vilipiganwa kati ya 5 na 10 Juni 1967 kati ya Israeli na Jordan, Syria, na Misri. Uhusiano kati ya Israeli na majirani zake haukuwekwa sawa baada ya Vita vya Kiarabu na Israeli vya 1948.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,053
2,000
Tujuze mkuu,hatujui
Baada ya hao wanao jiita Waizrael ( mimi nawatambua kama Walowezi kutoka maeneo mbalimbali ya Ulaya na Marekani) kujipenyeza Palestina iliyokuwa ikikaliwa na Waarab kwa miaka mingi na kujitangazia Uhuru wao mwaka 1948 chini ya Waziri Mkuu wa Kwanza David Ben Gurion!

Baada ya kuzaliwa kwa Taifa la Israel, mkakati wa kuyachukua maeneo ya wenyeji kwa nguvu ili kuwapatia Walowezivwa Kiyahudi, ulipamba moto! Waarab (Wapalestina) ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa hilo eneo, walipambana dhidi ya Wavamizi kwa miaka mingi, na kuishia kushindwa!

Kulikuwa na vita mwaka huo huo wa 1948, 1956, 1967, 1973, mpaka leo hii bado hali si shwari. Na katika vita hivyo, kuna nyakati ambapo nchi za Kiarab kama Misri, Syria, Lebanon, Iraqi, Iran, nk ziliisaidia Palestina! Lakini mwisho wa siku wote walishindwa na hao Waizrael!

Na ndiyo kipindi hicho baadhi ya nchi kama Misri, ziliamua kuingia makubaliano binafsi na Israel kupitia Makubaliano yaliyofanyika eneo la Camp David Marekani na kuongozwa na Rais wa kipindi hicho Jimmy Carter, na hivyo Misri kujitoa rasmi katika uhasama na Israel mtoa roho.
 
Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,290
2,000
Leo ndio nimejua asee,sijawahi sikia wakimbizi wa Syria wakimbilia Qatar au wakimbizi wa Palestina wakimbilia Misri au Saudia... sidhani kama kuna kambi za wakimbizi pia. Jiulie pia kwanini Walibya badala ya kuvukia Misri wanakubali kufia bahatini kwenda Ulaya?

Wakimbizi wengi wa kiarabu wanakimbilia Ujerumani na Ugiriki pamoja na Uturuki kuwa karibu lakini wanaenda mbali dah!!🤔🤔

Naamini hata Afrika tuna nafuu kwa huruma na ujirani kuliko waarabu
Waarabu ni wabinafsi sana shangaa hata wakimbizi kutoka nchi za kiaarabu hawaruhusiwi kwenye hizo nchi zao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom