Utunzaji wa vifaa vya umeme majumbani, ofisini

MWENYE HEKIMA

JF-Expert Member
Mar 3, 2012
373
230
Habari za siku na karibu Studio.

Bila shaka haujambo na unaendelea vizuri na michakato ya maisha. Leo ningependa tuongelee juu ya njia bora za kutunza vifaa vya elektroniki nyumbani, ofisini na kila sehemu vitumikapo.

Njia hizi zitasaidia kwa namna moja ama nyingine kupata matokeo bora zaidi kutoka katika kifaa chako husika.

Jinsi ya kutunza Friji na Freezer
Wengi hutumia kifaa hiki kutunza chakula vivyo hivyo hutumika kupozea vinywaji baridi. Ili friji au freezer yako idumu zingatia yafuatayo, safisha pembe za mlango wa friji au freezer yako, tumia maji ili kuondoa taka zilizogandamana.Punguza barafu iliyoganda katika kuta za friji kwani hizi husababisha friji kutumia umeme mwingi zaidi na hivyo kukuongezea bili ya umeme. Unaweza kupunguza au kutoa barafu hizi kwa kuzima friji hadi ziyeyuke, au futa na maji ya moto, au hair dryer au kwa kutumia feni.Usiweke mzigo mzito sana katika shelf za friji au freezer.Tumia upepo wa vaccum cleaner ili kupuliza vumbi angalau mara mbili kwa mwaka, kifaa hiki hupatikana kwa mafundi friji pia mafundi computer.Chomoa katika soketi wakati wa mvua.

Jinsi ya kutunza Computer/Laptop
Update mara kwa maraTumia Antivirus iliyokuwa inayokuwa updated angalau kila siku. Ku update hakuchukui muda mrefu kama una update kila siku huchukua hata dakika kadhaa tu. Ninashauri anti-virus hii ya AVG Free Antivirus kwani ni bora sana.Zima computer yako kwa kufuata njia mahususi na sio kuchomoa tu nyaya au kuzima ukutani.Kwa laptop pindi inapokuwa imetumika kwa muda mrefu na ikachemka sana jaribu kuizima/sleep/hibernate kwa muda ili ipoe hivyo utasaidia kuifanya iwe na kasi zaidi.Dumisha nguvu na uimara wa betri kama unatumia laptop.

Tafadhali mpendwa mgeni, je,ungependa kujua zaidi kuhusu kifaa gani na jinsi ya kukitunza ili kiweze kuwa na manufaa zaidi kwako. Usisite kinitaarifu nami nitaandaa post kwa ajili yako wewe. Asante kwa kusoma hii. Nyingine ni bomba pia!
 
Mkuu hii AVG free antivirus ina tofauti yoyote na ile Kaspersky? Maana mara nyingi tukienda huko madukani tunapoulizia antivirus tunashauriwa kununua hii Kaspersky.
 
Back
Top Bottom