Utundu Lissu wa kuomba hela ya kula ulaya ni zaidi ya umatonya

Dec 13, 2018
30
140
UTUNDU LISSU WA KUOMBA HELA YA KULA ULAYA NI ZAIDI YA UMATONYA.

Leo 13:15pm,16/02/2019.

Sifurahishwi na tukio la Tundu Lissu kugeuka omba omba Ulaya ilihali anaweza kurudi nyumbani kuja kulima Alizeti kule Singida na kujipatia pesa pasipo kuwa omba omba ulaya,au arudi akasaini kwa mwajiri wake ama amwombe mwenyewe mwajiri wake amwambie minajiri ya yeye kuwepo nje wataelewana tisa, kumi sifurahishwi sana na hii tabia ya waafrika kuwasubiri wazungu waje kutatua mambo yetu wakati ni rahisi na Sisi tunaweza kuyatatua wenyewe ila hatutaki tu,Tukisimama kidete tunaweza kujitegemea sisi wenyewe kwa maana tunayo kila rasilimali ya kujitegemea sisi wenyewe.

Katika Zama za maendeleo tungependa kusikia Tundu Lissu akiongelea kuvaa nguo zilizotengenezwa Tanzania "made in Tanzania", kuangalia television zilizotengenezwa Tanzania na vipindi vyenye mahadhi na utamaduni wa Mtanzania.Ila Tundu Lissu bado anaamini kila kinachomhusu mzungu ni bora na sasa anataka kuishi Ulaya, Akiongea na kuchanganya na maneno ya kiingereza ili aonekane ana akili atakuja na maneno kayatoa kwenye kamusi utadhani hajui kiswahili,Tundu Lissu bado anaamini kiingereza ni bora kuliko kiswahili na anathubutu kusema eti Mheshimiwa Rais hajui kiingereza.

Wakati wa Utumwa,Waafrika tulipofika katika mashamba ya pamba Marekani tuliweza kuwasiliana pasi hao mabwana mabeberu kuelewa. Hii iliwakera sana mabeberu hao waliposikia tukiwasiliana vyema pasi wao kuelewa,Mabwana hao wakatunga sheria watoto wote wa watumwa wanapaswa kwenda boarding school kuanzia umri wa miaka 7, na walipofika bwenini ilikuwa ni marufuku kuongea lugha nyingine yeyote na lugha zetu za kiafrika ziliitwa za kishenzi.Watoto wetu walikaa miezi sita na kurudi nyumbani kwa wiki mbili. Hii ilikuwa njia ya kuua lugha nyingine zote na watoto wote waliongea Kiingereza.Leo Tundu Lissu anatukumbusha machungu haya tuliyofanyiwa na washenzi wazungu.

-Je ni kweli Tundu Lissu ameishiwa hela uko Ulaya!?

-Wazungu wangemtukuza na kumuhifadhi Tundu Lissu ikiwa tu wangepata uhakika wa 100% kama Tundu Lissu atakuwa rais wa Tanzania. Unaweza kuekewa namna gani wazungu wanavyokusaidia Ili hali macho na akili zao zipo kwenye Madini, Gesi na Maliasili zote zitakazowapa faida, kama wamekosa uhakika basi kwa kutumia lugha yao watasema "Tundu Lissu is just an insect disturbing them in their lunch time " Hivyo basi Tundu Lissu ni kama inzi anayewasumbua wakati wa Chakula cha mchana.

-Kama Wazungu hao wamethibitisha Tundu Lissu atakuwa rais wa Tanzania na watamtumia kama kibaraka wao, basi dollar nyingi zitakuwa zinamsubiri Tundu Lissu mahali fulani na anachotakiwa kufanya Tundu Lissu ni kutakatisha fedha hizo kwa kuitisha Harambee kuonyesha watu wamemchangia Dolar nyingi na kanunua nyumba Ubelgiji ambayo ataitumia kuishi kama akishindwa kuwasaliti Wananchi wa Tanzania,Amini nawaambieni Machekibobu wale wanaokusanyika kuongea nae pale Marekani hawana uwezo wa kumchangia Lissu ikiwa hata Misiba yao tu unawashinda na wanaishia kuchanga dolar 10,20 au 30 kugharamia usafiri wa kumleta mwenzao nyumbani, hivyo basi kwa namna yoyote ile kama Tundu Lissu atatokea na Maburungutu ya dollar basi mtambue ni pesa za Mabeberu.

-Je unaweza kuhituhumu Marekani na kuibuka mshindi.

-Si rahisi kuipakazia Marekani inaiuzia Tanzania ndege mbovu halafu uende kwao wakupe mapokezi sambamba na mapokezi atauopewa msaliti wa kichina ama msaliti wa kihindi sembuse wewe msaliti wa kitanzania, Lazima tufikiri vyema ndugu zangu, na yanayompata Tundu Lissu yawe ya mfano kwa Wasaliti wengine wa Taifa la Kizalendo.

Zitto Kabwe,Tundu Lisu na Chadema walipinga mpango wa Marekani kuiuzia ndege za Boeing Tanzania kabla hata baada ya kununua kwa lugha ya kwao Wamarekani anasema "Tundu Lissu insulted Americans as he said they were selling not new planes but used planes!!!!!!" Hili lilikuwa kosa kubwa la Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Chadema.

It is not easy to cheat Americans easily by cheap lies of Tundu Lisu.Chadema were against government of Tanzania to buy planes from their company Boeing . Chadema and Tundu Lissu they continued insulting Boeing by allegging without any reliable evidence that Boeing is selling used Boeing planes to Tanzania.They tarnished the good brand name of Boeing that has been built for years.Americans are furious with Tundu Lissu and his Chadema for the issue of Boeing deal with Tanzania.

United States of American has various means of approaching developing Nations.
United States of America can not jeopardize bilateral relationship with Tazanian government simply one MP named Tundu Lissu from opposition party has been shouting nonsense from foreign Western donor states to punish Magufuli Government.America don't work like that,besides they are not angels,and they do remember the killing of Malcom X and Martin Luther King.

-Pengine ni Filamu ya kutafuta Umaarufu duniani.

-Tangu kuwepo kwake Nairobi taarifa zilisema kuwa Ndugu TUNDU LISSU,ametayarishiwa mazingara mazuri sana ya kuweza kupewa Uhamiaji/Ukimbizi wa kisiasa kati ya nchi tatu ( Ujerumani, Sweden,Ubelgiji na Canada ).

Inasemekana ya kuwa Ndugu Lissu alishapeleka maombi kadhaa ya Ukimbizi wa Kisiasa, likihusiana na kutaka kuijengea picha mbaya nchi yetu ili ziwepo presha za Wazungu za kuitoa CCM Madarakani baada ya Chadema kushindwa kwa hoja zao na sera zao mufilisi.

-AU yaanza kujitegemea.

-Wakati Tundu Lissu akipitisha bakuli la kuomba Ulaya, Umoja wa Afrika umeanza kujitegemea kimaendeleo,tukiichukulia Afrika kwa Nchi ya mfano basi tutaitumia Rwanda,licha ya nchi hiyo kukabiliwa na vita na matatizo ya kikabila wananchi wa Rwanda hivi sasa wanajiamini wenyewe na viongozi wao wakiongozwa na Rais Paul Kagame..

Wananchi wa Rwanda waliamini katika sera za kimaendeleo za Rais wao aliyekuwa na nia na maono ya kuifanya Rwanda kuwa Taifa kubwa licha ya udogo wa eneo ililonalo.

Tanzania ni mfano mwingine wa nchi ya kiafrika iliyoamua kujitegemea, Ujenzi wa taasisi thabiti na zenye nguvu nchini unaofanywa na Rais John Magufuli utafutilia mbali ulaji rushwa, ghasia zenye uchochezi wa kisiasa, ukiukwaji haki za binadamu na ukosefu wa heshima kwa utawala wa sheria.

Lakini katika Umoja wa Afrika Mageuzi kadhaa yaliyopendekezwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kabla ya kumuachia Mwenyekiti wa sasa ambaye ni Rais wa Misri ameacha mapendekezo ya kujitegemea kifedha kwa Umoja wa Afrika na yamejadiliwa kwenye kikao cha 30 cha Marais na viongozi wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Africa.Malengo ya Mageuzi hayo ni kujitegemea kifedha kwa Umoja wa Afrika.

Nimalizie kwa kuipongeza Tanzania ambayo inafanya vizuri na ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme na sasa inalenga kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali,hii ni taswira njema kwa Umoja wa Afrika ambao unaekekea kujitegemea katika nyanja zote za kiuchumi, Kisiasa na Kijamii, Shukrani za dhati kwa Rais Kagame na Rais Magufuli kwa kuwezesha Afrika kujitegemea.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
 
SELF PROCLAIMED UNITED STATES GOVERNMENT SPOKESMAN, Msemakweli Chakubanga.
Na serikali yetu iliyokuwa ikiomba unga wa yanga toka Marekani na mchele wa kitumbo toka China!
Mlimnyima hela yake halali ya tiba mkitegemea atakufa kwa kukosa tiba sasa mnaona yuko kama nyie mnalalama kwa hasira zenu za chuki.
 
Bora Tal anayeomba pesa za kujiuguza ulaya kuliko anayeomba pesa za kuhonga wabunge kuua democrasia na kufuga mazuzu Kama nyinyi
 
SELF PROCLAIMED UNITED STATES GOVERNMENT SPOKESMAN, Msemakweli Chakubanga.
Na serikali yetu iliyokuwa ikiomba unga wa yanga toka Marekani na mchele wa kitumbo toka China!
Mlimnyima hela yake halali ya tiba mkitegemea atakufa kwa kukosa tiba sasa mnaona yuko kama nyie mnalalama kwa hasira zenu za chuki.
Huo unga unaufahamu au unaongea tu?inawezekana umesimuliwa nadhani hata kwenye suruali ulikuwa hujatoka
 
hizi tabia za umatonya kila mwanaukawa anazo .wanaukawa ni ombaomba tu
Kumbuka hata akina mzee Aikaeli Mbowe wali wafadhili viongozi wakati wao walikuwa smart pesa ya mboga ilikuwa haiwapigi chenga kuombana na kufadhiliana haikuanza leo
 
Ombaomba ni nyinyi wajinga mnaomsujudiwa Jiwe ili mkono uende kinywani. Umemsikia Nchemba huko, anamshukuru Rais kwa kupona katika ajali ya gari, Sasa huu si upumbavu uliopitaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wewe na mimi ambao tunalishwa na kodi za mabeberu tujiiteje. Kwasababu kila cku tunaomba msaada na bila mabeberu kutupa pesa bajeti haifiki popote. Kweli wahenga wasiona mbali na kusema Nyani Hanoi kundule. Akiliona la mwenzake hufurahi na kurukaruka wakati nae ni kama wao. Usiandike maneno mengi kabla unafikiria
 
Kimsingi sasa hivi Africa imeanza kujitambua. Fikra hasi za kusema kwamba kwamba kila kilicho bora kinatoka kwa wazungu naona zimeanza kutoweka. Wapo wachache ambao wanataka kutuaminisha kwamba wazungu ndio bora na kila tatizo tulipatalo basi mtu mahiri na mzuri wa kulisemea ni mzungu. Watu hao kama alivyo Tundu Lissu tena wakiwa ni wasomi, wanaturudisha nyuma kwa kudharau Uafrica walio nao hata wao wenyewe.

Juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wetu kujenga miundombinu ambayo kwa akili za kawaida hakuna Rais aliepata ujasiri wa kuijenga itasaidia sana kuifanya Tanzania tupae kiuchumi. Miradi kama Ujenzi wa reli, ujenzi wa bwawa la umeme, ununuzi wa ndege sambamba na ujenzi wa viwanja vyake, ujenzi wa barabara, ujenzi wa jiji jipya la Dodoma, ujenzi wa hospitali na vituo vya afya nchi nzima, uimarishaji wa sekta ya utalii, ujenzi wa bandari na miundombinu mingi sana ni chachu kubwa ya maendeleo. Kwa mtu asieona mbali na mjinga wa kutegemea vya wazungu atadharau na kuona kama tunapoteza muda.

Mtu mjinga ataona shida tunazopitia kwa kuwa na miradi hii mikubwa ataona ni mtaji wa kukejeli na kutukana. Lakini ni dhahiri kuwa miradi hii ikikamilika tutapata pesa nyingi sana za kigeni na hivyo kuinua mapato yetu na uchumi utakuwa na maisha yatakuwa bora zaidi. Tumuunge mkono Rais wetu kwa kazi kubwa anayoifanya ya kujenga taifa litakaloweza kujitegemea.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom