Utumwa wa minyololo kwenye nchi yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumwa wa minyololo kwenye nchi yako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SYENDEKE, May 20, 2012.

 1. SYENDEKE

  SYENDEKE Senior Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 167
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wandugu niko kwenye sherehe za mwenge kwa sasa mwenge wa uhuru umelala mkoa wa iringa wilaya ya mafinga viwanja vya mashujaa karibu na ofisi za ccm wilaya sasa kuna waraka umetoka kwa wafanyakazi wote wa halmashauri ni lazima kuwepo na kukeshe kwenye sherehe za mwenge halafu kuna attendance ya mahudhulio kwa wafanyakazi kila baada ya masaa 5 hadi asubuhi na mwajili(Mkurugenzi) amechimba bonge la mkwala kwa yule atakaye kiuka agizo hilo inawezekana kupewa barua ya onyo kali au kusimamishwa kazi kabisa sasa hapa nina mama mmoja kiukweli ni umri umekwenda sana anasema mwanangu usione hivi naogopa kufukuzwa kazi huyu mtu hana masihala kabisa ngoje nivumilie bwana hao ndo wakubwa hata kama sijapenda kuwa hapa. KUNA HAJA GANI YA MWENGE KAMA KUNA UTUMWA KIASI HIKI. HUUU NDO MWENGE WA UHURU
   
 2. J

  Jichokuu Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndo sera,hata pale babati ilitokea 2009
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  UNASHANGAA NINI ? MBONA TULIIMBA KUWA UTUMWA WA UKOLONI NI SUMU mimi sitoweza kuutukia. Huu utumwa wa ujamaa na kujitegemea ni mbaya sana na mpaka leo unatukaanga lakini hakuna hata mmoja anaulaani. katiba yetu bado ina kifungu kisemacho kuwa Tanzania inasafiri ktk njia ya ujamaa na kujitegemea.
   
 4. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu SYENDEKE, kama upo hapo kwenye huo mkesha, wacheki askari police, wanavyoulinda huo mwenge,ni vijana wadogo wanakula moshi wa diesel mpaka asubuhi. Afya zao hazijaliwi, bora hata watengeneze mwenge wa umeme wa kuchaji toka china. Toa wazo lako hapo uone kichapo chake, this is typically worshiping the devil.
   
 5. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Huo Mwenge siku nyingi uliishageuka chombo cha wajanja kuwaibia wananchi. Wafanyakazi wilayani, hasa kwenye Halmashauri hulazimishwa kukatwa mishahara yao eti ni michango ya mwenge. Wakulima maskini vijijini nao vile vile hulazimishwa michnago ya Mwenge. Kuna huu ujinga eti mwenge unazindua miradi ya maendeleo!!! Hiyo miradi inagharimiwa na fedha za kodi zetu hata bila mwenge hiyo miradi ingeweza kuzinduliwa kwa namna nyingine. Nionavyo mimi huo mwenge ungekuwa unawashwa mara moja kwa mwaka pale Moshi, unapandishwa juu ya mlima Kilimanjaro, halafu unashushwa basi. Mnaonaje na hiyo ikiwa moja ya hoja kubwa katika kutoa maoni kuhusu Katiba mpya. Mwenge unaleta umasikini na kueneza UKIMWI.
   
Loading...