Utumwa mpya ndani ya Kanisa

Ukweli huu ngumu kumeza, tujipe moyo lkn uangalie na sehemu ya kujipa moyo,huwezi sema unajipa moyo maji yatachemka huku umeweka mawe jikoni badala ya mkaa, nevaaaaa
 
Halafu ujinga ni ujinga tu si suala la mtu kwenda shule au kutokwenda kuna watu wanajazwa ujinga huku huku shule,hawa mnao waona wamekosa elimu ndio maana wanaibiwa huko makanisani ndio hawa hawa hujisifu kwa kuwa na elimu ya dunia kuliko wenzao wa upande wa pili ambao wao elimu ya dini ndio wameiweka mbele na kuwa nyuma kwenye ya dunia..

Unakuta mtu anafikiri elimu yake ndio inayomfanya aone hakuna Mungu hivyo wenye kuamini Mungu wamekosa elimu,hii ni dhana ya kijinga kabisa.
 
Kwa watu wavivu wa kufikiri kama nyie hicho ndio kichaka chenu cha kujifichia,mtu hujawahi hata kushuhudia tukio lenye kuhusishwa na uchawi na ukalichunguza ili upate ukweli ila mnakuja humu kusema tu hakuna uchawi mara hakuna Mungu,jiulize una hoja gani ya msingi inayokufanya upinge uchawi zaidi ya msimamo tu usio na nguzo yeyote.
Hujathibitisha Mungu yupo.

Hujathibutisha uchawi upo.

Thibitisha.
 
Huwa unakera na misimamo uchwara sijawahi kusoma hoja zako zilizo base kwenye reasoning na logic kuhusu uwepo/kutokuwepo Mungu.
Bado hujathibitisha Mungu yupo, unakerwa na swali muhimu tu la kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu huwezi kuthibitisha.

Kwa sababu Mungu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
 
Kuna muda umeuliza Mungu yupi, nikapatwa na mashaka kuwa wewe unawajua mungu wangapi?

Si swali la kutaka kujua uwepo wa Mungu zaidi ya ligi za kitoto, unataka uthibitishe vipi labda..? Kwa kuona, kusikia, kugusa, kunusa au kuhisi?
Bado hujathibitisha Mungu yupo, unakerwa na swali muhimu tu la kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu huwezi kuthibitisha.

Kwa sababu Mungu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
 
Kuna muda umeuliza Mungu yupi, nikapatwa na mashaka kuwa wewe unawajua mungu wangapi?

Si swali la kutaka kujua uwepo wa Mungu zaidi ya ligi za kitoto, unataka uthibitishe vipi labda..? Kwa kuona, kusikia, kugusa, kunusa au kuhisi?
Thibitisha Mungu wako yupo kwa njia iliyo logically consistent na isiyoweza kuwa contradicted.
 
Nimeituma kama nami livyoikuta namani itawagusa wengi an ndio hali halisi iliyipi kwa sasa.

UTUMWA MPYA NDANI YA KANISA

Pale udadisi unapokwenda likizo (reasoning)
Ndani ya Kanisani,watu kwa kukosa maarifa wanaibiwa. Kwa bahati mbaya hatujifunzi kutoka kwa Wabeloya, hawa walikuwa wadadisi.

Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonike. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli.

Watu Wanaibiwa kwa kupitia magonjwa yao , wanaibiwa kwa kupitia umaskini wao, wanaibiwa kwa kupitia kukata tamaa kwao , wanaibiwa kwa kupitia kutokujua kwao.

Wengi wao shida zao haziondoshwi ingawa mtumishi wa bwana (The man of God ) anaendelea kuneemeka.

Wanaibiwa kwa kutumi jina la yule ambaye alipotakiwa kulipa kodi ilibidi amtume mfuasi wake kupata hela kwenye kinywa cha Samaki.

Wanaibiwa kwa kutumia jina la yule ambaye alikuwa hana mahali pa kulaza ubavu wake .

Huu ninauita wizi wa bila kutumia nguvu.

Wizi huu unatokea sana Africa nzima ambapo waumini kiupofu wanafuata na kutimiza maagizo ya uongozi.

Kwa uaminifu mkubwa wanapanga foleni kununua miujiza kwa njia ya mafuta, maji , chumvi, vitamba nk. Kwa mtu yeyote anayejiita Mtumishi wa Mungu (The man of God).
Wengi wao wakihubiriwa kuwa kuna laana ya ukoo au kizazi ili hali maandiko yanatufundisha kuwa laana zote zilimalizwa pale msalabani .
Changamoto nyingi walizo nazo wakristo wengi Barani Africa kama umaskini na baadhi ya magonjwa,sio za kiroho,bali ni Ujinga.Mafundisho mengi kwa waumini ni juu ya laana ya kizazi au Ukoo (Generational curse) ingawa Mambo mengi ni ujinga wa kizazi au ukoo (Generational ignorance)

Katika Makala yake iliyochapishwa na jarida la Modern Ghana , toleo no.215 la April 2019 Mwandishi Kay Musonda ansema!

Afrika kwa sasa inashuhudia aina mpya ya utumwa kupitia Ukristo (ulokole). Aina hii ya utumwa wa imani imewafanya watu wengi kuwa wavivu wa kufikiri na uwezo wa kutafakari mambo umedumazwa.

Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu. Wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa. Wanajituza wao zaidi kuliko kumtukuza yule wanayemhubiri.

Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama, Serena Williums, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia kutransform dunia kama akina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi waliodedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.

Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana kama Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wakongwe kama Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.

Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.

Wao wataongelea mtu aliyepata kazi kimiujiza licha ya kukosa sifa za kupata kazi hiyo, kwa sababu tu aliombewa na kupewa mafuta ya upako siku ya interview ya kazi.

Wataongelea kuhusu kijana aliyetoa mshahara wake wote kwa miezi mitatu mfululizo kwa Mchungaji wake kama mbegu ya mafanikio, baadae akawa 'Boss' kazini.

Au wataongelea kuhusu kijana aliyefeli sekondari lakini baada ya baba yake kumalizia ukarabati wa nyumba ya Mchungaji, alipokea barua ya kupata 'admision' chuo kikuu bila hata kurudia mitihani.

Wachungaji hawa hutumia 'miujiza na shuhuda feki' kama njia ya kuwafumba akili wafuasi wao. Kule Afrika kusini kuna Mchungaji alidanganya kufufua mtu. Hata alipoomba msamaha bado kuna waumini wanaendelea kumuamini na kumsujudu.

Wachungaji hawa wamegundua haya ndio mahubiri yanayopendwa sana huku Afrika. Hawataki kuhubiri kuhusu Aliko Dangote alivyoanza biashara na magumu aliyopitia.

Wanahubiri kuhusu mama Janeth aliyekua mama Ntilie huko Enugu, lakini alipotumia mtaji wake wote wa shilingi laki 5 kununua mafuta ya upako kwa Nabii fulani, ghafla biashara yake ikakua na sasa anamiliki mahoteli makubwa pande zote za nchi. Yani bila mtaji, bila business plan, bila timeline ghafla tu akamiliki mahoteli. Na waumini watashangia kwa kusema Ameen.

Aina hii ya ukristo imepanda mbegu ya uvivu wa kufikiri kwa vijana wengi wa Afrika ambao wanalazimishwa kumuona Mungu kama Mfadhili wa wavivu, au wasiostahili. Kwamba mwanafunzi hata asiposoma anajua akipewa mafuta ya upako atafaulu tu siku ya mtihani. Mfanyabiashara hata asipokua mbunifu anajua akienda kwa 'baba wa miujiza' biashara yake itapanuka ghafla bin vuu. Mfanyakazi hata asipowajibika kazini anajua akitoa fungu la kumi kwa 'Dokta Upako' atapanda cheo.

Kwa baadhi ya makanisa Africa namna pekee ya kufanikiwa ni kufanya kile wanachokiita kupanda mbegu, kupaka mafuta ya upako au kunyunyuziwa maji ya baraka. Eti wanaofanikiwa haraka ni watu 30 wa mwazo wanaokimbilia mbele ya kanisa kila mmoja akiwa ameshika noti ya dola 100.

Aina hii ya mahubiri inawafanya watu waamini kwamba Mungu hawapendi wanaojituma na kuwa wabunifu katika kazi, badala yake anawapenda zaidi wanaotoa zaka, sadaka, malimbuko na fungu la 10 hata kama ni wavivu. Hii sio sawa hata kidogo kwa sababu Biblia inakataa uvivu kwa nguvu zote ( *Mithali 12:27 Bali mtu mvivu hapiki Mawindo yake; Bali Mwenye bidii anazo mali za thamani).*
_
Watu wanaaminishwa kwamba ukishatoa sadaka kanisani unaweza kuamka kila siku asubuhi ukapayuka 'Mimi ni Milionea' halafu ukavuta shuka na kuendelea kulala fofofo, ukisubiri sadaka uliyotoa ikupe muujiza wa kuokota hela, ili upate mtaji wa biashara unayoiwaza.

Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive". Huu ni utani.

Waambieni wanaofanya utani huu kwa kofia za Uchungaji, Uaskofu, Unabii au Utume kwamba wanamkosea Mungu. Waambieni Mungu wetu ni Mungu wa kanuni, na hana kanuni ya kuwabariki wavivu. Tuache kufundisha waumini wetu kwamba uvivu unalipa kupitia miujiza.

Mafanikio ni matokeo ya bidii, ubunifu na weledi. Biblia inazungumzia kuhusu karama. Hebu kila mtu atumie karama alizopewa kwa bidii, ubunifu na weledi aone kama hatafanikiwa. Sio sahihi kuwaambia watu wabweteke tu na kusubiria mafanikio kama kusubiria daladala kituoni kwa sababu tu wamepakwa mafuta ya upako.

Mungu alishatubariki *tangu wakati wa uumbaji wetu. Ni wajibu wetu kujibidisha katika yale tufanyayo ili baraka zake ziambatane nasi ( *Kumb 28:6 Utabarikiwa uingiapo utabarikiwa na utokapo).*

Wazungu na Wachina wanazidi kushindana katika kuitawala dunia kwenye mambo mbalimbali kuanzia viwanda, biashara, sayansi na teknolojia. Sisi tuko 'busy' kununua maji ya upako tukiamini yatatufanya tuwe kama Jack Ma au Bill Gates. Upuuzi.

Tumeumbwa kuitawala hii dunia (Mwanzo 1:28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbw chenye uhai kiendacho juu ya nchi). Tutumie vipawa na karama tulizopewa ili kutimiza kusudi hilo la Mungu. Tusiruhusu Askofu, Mchungaji, Nabii, mtume au kiongozi mwingine yeyote wa dini atutawale akili zetu kwa kutuhubiria mafanikio ya miujiza. Wao wanaishi kifahari kwa sadaka za waumini wao, huku waumini wakiendelea kuwa mafukara wa kutupwa.

Biblia inasema kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa ( *Mithali 1:7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu).* Tutafute maarifa, tufanye kazi kwa bidii, na tumuabudu Mungu katika Roho na kweli. Kwa kufanya hivyo tutapata MAFANIKIO katika mambo yote tuyafanyayo.

NB: Makala hii inazungumzia baadhi ya makanisa ya kilokole sio yote. Dont generalize. Yapo makanisa ya kilokole yenye misingi bora, lakini mengine yamejaa upotoshaji. Haya ndio yaliyozungumzwa hapa. Tafsiri isiyo rasmi imefanywa
na Malisa GJ.
Tukutane wiki ijayo panapo majaliwa.
Na bahati mbaya kwetu, tuliemkabidhi jukumu la kuangalia usalama wetu, tunamlipa kodi zetu, SERIKALI, anajua yote, anashangilia. Tunatumikishwa na imani, tunaswagwa aheri ya kondoo.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.
Hujathibutisha uchawi upo.
Thibitisha.
Uthibitisho haufanyi kiwepo ambacho kiuhalisia hakipo wala kukosakana uthibitisho haifanyi ukweli kuwa uongo,watu wavivu wa kufikiri lazima mkimbilie kwenye uthibitisho maana ndiyo kichaka chenu cha kujificha,nikikuuliza hapo kama ulishawahi kukutana na tukio katika maisha yako lenye kuhusishwa na uchawi nahakika hujawahi kukutakana na hicho kitu kifupi huna hata.uelewa na hicho unachopinga ila cha kushangaza mnadai uthibitisho.
Kama kweli mnajiamini na mna mawazo huru tuchambue haya matukio yenye kuhusishwa na uchawi na nyie mtoe hoja za misimamo yenu kuhusu kutokuwa na uchawi sio mnaishia kusoma mawazo ya huko wenye kuwaambia hakuna uchawi bila wenye kuchunguza mnakuja kupinga tu humu.
 
Silaha ya wajinga wengi wanaoogopa kuitwa wajinga hukimbilia hiyo nukuu hudhani kufanya hivyo kutawafanya wasiwe wajinga
Kama ilivyo kwenu ujinga wenu mnauficha kwenye kudai uthibitisho,yani unakuta mtu hata hana uelewa wa kutosha na jambo analopinga ila nae amekariri kudai uthibitisho maana anajua ndio kichaka cha kujifichia.
 
Uthibitisho haufanyi kiwepo ambacho kiuhalisia hakipo wala kukosakana uthibitisho haifanyi ukweli kuwa uongo,watu wavivu wa kufikiri lazima mkimbilie kwenye uthibitisho maana ndiyo kichaka chenu cha kujificha,nikikuuliza hapo kama ulishawahi kukutana na tukio katika maisha yako lenye kuhusishwa na uchawi nahakika hujawahi kukutakana na hicho kitu kifupi huna hata.uelewa na hicho unachopinga ila cha kushangaza mnadai uthibitisho.
Kama kweli mnajiamini na mna mawazo huru tuchambue haya matukio yenye kuhusishwa na uchawi na nyie mtoe hoja za misimamo yenu kuhusu kutokuwa na uchawi sio mnaishia kusoma mawazo ya huko wenye kuwaambia hakuna uchawi bila wenye kuchunguza mnakuja kupinga tu humu.
Sasa kama huna uthibitisho kuhusu Mungu wako, una uhakika ganibkwamba yupo na si hadithi tu?
 
Sasa kama huna uthibitisho kuhusu Mungu wako, una uhakika ganibkwamba yupo na si hadithi tu?
Labda nikuulize.

Wewe unasema hakuna Mungu ni kwa sababu tu hakuna uthibitisho?
Je,wewe una uhakika kuwa ni kweli hakuna Mungu na si vinginevyo?
 
Labda nikuulize.

Wewe unasema hakuna Mungu ni kwa sababu tu hakuna uthibitisho?
Je,wewe una uhakika kuwa ni kweli hakuna Mungu na si vinginevyo?
Licha ya kutokuwa na uthibitisho Mungu yupo.

Habari za kuwapo kwake zina contradiction.

Hapa unaambiwa Mungu anajua yote, mpaka yajayo.

Pale unaambiwa Mungu alivyoumba watu, akaona hajapendezewa na tabia zao, akakasirika na kutaka kughairi , akawapiga gharika.

Sasa huyo Mungu mjuzi wa yote mpaka anataka kughairi kwani hakujua hayo ambayo hakuyaoenda yatatokea?

Kila habari ya kuwepo na Mungu inapoletwa ukiichunguza unaikuta ina contradictions.

Kwa sababu Mungu hayupo.
 
Kama ilivyo kwenu ujinga wenu mnauficha kwenye kudai uthibitisho,yani unakuta mtu hata hana uelewa wa kutosha na jambo analopinga ila nae amekariri kudai uthibitisho maana anajua ndio kichaka cha kujifichia.

Kama kudai uthibitisho ni ujinga hivyo utakubali kila kitu unachoambiwa kua ni kweli kwasababu utakua mjinga kudai uthibitisho???

Swala la kudai uthibitisho sio ujinga inategemeana na kwa namna ulivyolitumia ukilitumia vibaya ku force likupe uthibitisho wa visivyopo kua havipo ni lazima ulione lakijinga

Swala la uthibitisho lingekua lakijinga basi hata benk zisingekuwepo, kwasababu watu wangeseza kuchukua mikopo ya mamilion ya pesa bila kuwepo na nyaraka zenye kuthibitisha mali anazomiliki kama dhamana

Ukishajua kuhusu inventions za watu hususani katika finctional characters, utagundua kuamini vitu hivyo kua viko real bila uthibitisho ni ujinga uliopitiliza
 
Back
Top Bottom