Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Ukweli niliamua kuacha kazi mwishoni mwa Mwaka 2016 na nikaamua kurudi kijijini na nyumbani kwetu Idukilo Shinyanga na kuanza kazi zangu za biashara. Kilichonifanya niache kazi ni kutokana na tu na maamuzi ya kibabe ya watu wenye mamlaka kuamua kibabe kuhusu mambo ya mtumishi wa umma hata kama hajapenda.
Kwa kifupi nilihamishwa kibabe kutoka mkoa ambao tayari nilishawekeza na kutokana na mshahara mdogo wa utumishi wa umma basi kipato changu cha ziada kikawa kinanifanya niishi vizuri.
Hilo likawakera binadamu wenzangu wakanisema vibaya na kuniundia majungu tu hadi nikahamishwa kupelekwa Dar es Salaam
Dar es Salaam yao ikanishinda - pamoja na kushawishiwa sana kwamba mambo yataniendea vizuri nikaona siwezi kumudu nikaacha kazi na kwa umri wangu ulivyo nisingeweza kustaafu kwa hiari.
Naambiwa eti vihela vyangu vya pensheni nisubiri nifikishe miaka 55 - na sasa nimebakiza miaka minne sasa kuifikia hiyo 55 - Mwenyezi Mungu anijalie nisife angalau nivipate hivyo vihela.
Pamoja na kutokuwa kwenye ajira kwa kweli kadri siku zinavyoenda naona watumishi wenzangu waliobaki bado wanaendelea kunyanyasika sana. Kuna mambo kadhaa ambayo yamejitokeza katika awamu hii ambayo yanaonekana kama kuboresha utumishi lakini kumbe yanakandamiza zaidi, nimeorodhesha kwa mtiririko ufuatao:
1. Kwa sasa hivi watumishi wa umma hawafikiriwi kabisa kwenye mambo ya uhamisho - mtu anaomba uhamisho lkn hajibiwi na utumishi wapo kimya tu. Yule ambaye hajaomba uhamisho anahamishwa kibabe - tena anahamishwa bila hata kupewa stahili zake za kiutumishi anaambia atalipwa malimbikizo.
2. Watumishi wengi wameandikiwa barua za kupandishwa vyeo lakini mabadiliko kwenye mishahara yao hayafanyiki. Kinachofanyika sasa ni kuziandika barua hizo kwa tarehe ya mbele ili wasidai malimbikizo - mwenyewe mpaka ninaacha kazi mwishoni wa 2016 sikuwa nimerekebishiwa mshahara pamoja na kuwa nilishapata barua ya kupandishwa cheo kwa miezi zaidi ya 8 nyuma. Nasimuliwa na wenzangu tangu niondoke wamebadilishiwa barua za kupandishwa vyeo mara kibao ili kuzuia wasidai malimbikizo.
3. Hata watumishi ambao wanakaimu nao wanakaimishwa zaidi hata ya miaka miwili bila kulipwa stahiki zao na wanapotolewa kwenye nafasi za kukaimu hawana tena nafasi ya kudai maslahi waliyokaimia.
4. Kwa sasa hata Sheria ya Utumishi inadaiwa imebadilishwa na Katibu Mkuu wa utumishi anaweza kukuhamisha popote pale, kukupunguza cheo au hata kukupandisha tu cheo hata kama hustahili na hawezi kufanywa chochote.
5. Wanasiasa kama kina Mkuchika kwa sasa wanawachukia watumishi wa umma - kumekuwa na mpambano ambao upo indirect, wanasiasa hawaongelei kabisa maslahi ya wafanyakazi katika mtazamo chanya. Juzi Mkuchika kaongelea kuhusu kucheleweshwa kwa mafao ya wastaafu lakini hakuongelea kabisa kuhusu wafanyakazi ambao bado wapo kazini na wana madai kibao.
Hakuongelea kuhusu nyongeza za mishahara, hakuongelea kuhusu manyanyaso ya uhamisho wa kibabe, hakuongelea kuhusu ajira mpya na za wazi ambazo hawataki kuziziba, hakuongelea kuhusu, kuthibitisha wale ambao wanapandishwa vyeo, hakuongelea kuhusu malimbikizo ya madai mbalimbali ya watumishi km malipo ya uhamisho, nyongeza za mishahara, nyongeza za pensheni, nk.
Kwa ujumla wanasiasa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi wamekuwa kitu kimoja. Wanawanyanyasa na kuwanyonya watumishi wa umma. Watumishi wa Umma wanawafanyia wanasiasa kazi zao, wanawalipa viongozi wa vyama vya wafanyakazi ada zinazowajaza matumbo yao lakini wanasiasa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi wamenyamaza kimywa. Hii sio haki, tena sio haki kabisa.
Kilichobaki kwa wenzangu mlio bado kwenye ajira msimame kidete kuangalia maslahi yenu, wanasiasa na vyama vya wafanyakazi hawana maana kwenu, waondosheni kwa kutumia utaratibu wa kidemokrasia - ondoa wanasiasa kwa kura na ondoa viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwa kura. Mtaniona mimi mwoga - sawa mie mwoga lkn mwaka huu hata Chama changu cha Mapinduzi naona sitakipa kura.
Nimeamua hata kama sitagombea lakini nitapigia kura upinzani isipokuwa tu pale mgombea wa CCM mwenye moyo wa dhati kuyaondoa hayo atajitokeza na kwa sura yake nikaamini anaweza kufanya kitu. Tusipofanya uamuzi mzuri kina Mkuchika wataendelea tu na maneno yao yasiyo na msaada wowote.
Asanteni na Mwenyezi Mungu azidi kutuepusha na balaa la #COVID19
Keep distance and please vaa Barakoa.
Its Tila Lila2 me