Utumishi wamwaga mamia ya kazi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumishi wamwaga mamia ya kazi...

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mr CarryFoward, Apr 22, 2010.

 1. M

  Mr CarryFoward Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) (NAFASI 21)
  SJFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo;
  Uchumi (Economics) Takwimu (Statistics)
  Sayansi ya Uchumi Kilimo (BSc Agriculture Economics &Agribusness)kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
  MSHAHARA .
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Tsh: 322,460/= na kuendelea hadi Tsh: 401,880/= kwa mwezi.
  MAJUKUMU YA KAZI
  Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
  Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
  Kufanya utafitJ na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
  Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi namaendeleo ya jamii.
  Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
  MASHARTI YA KAZI
  Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania.
  Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na picha moja ya Passport size za hivi karibuni.
  Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe namba za simu za kuaminika. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.Testmonials, Provisional Results, Statement of results HAVITAKUBALIWA.
  Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni wiki mbili baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
  Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  Katibu, Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, SLP.2483, Dar es Salaam.  MTAKWIMIJ DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) - (NAFASI 11)
  (A) SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au Hisabati au sifa zinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia "Information Commnication Technology (ICT)
  (B) MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Tsh: 322,460/= na kuendelea hadi Tsh: 401,880/= kwa mwezi.
  (E) MAJUKUMU YA KAZI
  Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na kuratibu takwimu Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)
  Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.
  MASHARTI YA KAZI
  Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania.
  Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na picha moja ya Passport size za hivi karibuni.
  Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe namba za simu za kuaminika. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.Testmonials, Provisional Results, Statement of results HAVITAKUBALIWA.
  Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni wiki mbili baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
  Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  Katibu, Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, SLP.2483, Dar es Salaam.

  AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) (NAFASI 19)
  (A) SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika mojawapo ya fani za; Ushirika, Uchumi, Uhasibu, au Masoko kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
  (B) MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Tsh: 322,460/= na kuendelea hadi Tsh: 401,880/= kwa mwezi.
  (E) MAJUKUMU YA KAZI
  Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture)
  Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
  Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
  Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishikatika vyama vya ushirika vya Msingi.
  MASHARTI YA KAZI
  Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania.
  Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na picha moja ya Passport size za hivi karibuni.
  Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe namba za simu za kuaminika. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.Testmonials, Provisional Results, Statement of results HAVITAKUBALIWA.
  Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni wiki mbili baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
  Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  Katibu, Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, SLP.2483, Dar es Salaam.  AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE OFFICER GRADE II) À(NAFASI68)
  (A) SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (SA in Social Works or Sociology) au Stashahada ya juu ya Ustawi wa Jamii (Advanced Diploma in Social Works) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
  (B) MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Tsh: 322,460/= na kuendelea hadi Tsh: 401,880/= kwa mwezi.
  (E) MAJUKUMU YA KAZI
  Kuendesha Usaili wa wahudumia (Watu wenye Ulemavu, Wazee, familia zenye matatizo, watoto na washitakiwa).
  Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi Wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.
  Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii.
  Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
  Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandiklshaji vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster care) na vituo vya walezi wa watoto wadogo mchana.
  Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama, walojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.
  Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali
  Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali toka kwenye familia za watu wenye dhiki
  Kuhoji na kuandaa taarifa za washitakiwa.
  Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya mafunzo ya Ufundi Stadi vya watu wenye ulemavu, Mahabusu za watoto na shule za maadilisho.
  MASHARTI YA KAZI
  Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania.
  Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na picha moja ya Passport size za hivi karibuni.
  Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe namba za simu za kuaminika. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.Testmonials, Provisional Results, Statement of results HAVITAKUBALIWA.
  Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni wiki mbili baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
  Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  Katibu, Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, SLP.2483, Dar es Salaam.  AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) - (NAFASI 3)
  SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (SA. in Sociology or Social Sciences) au Stashahada ya Juu ya ya Maendeleo ya Jamii au Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya Vijana (Advanced Diploma in Social Works or Community Development or Youth Development) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serkali.
  MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Tsh: 322,460/= na kuendelea hadi Tsh: 401,880/= kwa mwezi.
  MAJUKUMU YA KAZI
  Kuratibu na kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini
  Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya Vijana
  Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa Vijana na Elimu ya Familia kwa kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO)
  Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana
  Kuratibu shughuli mbalimbali za NGO zinazoshughulikia masuala ya Vijana Kuandaa mipango ya kuboresha malezi ya Vijana
  Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali
  Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo Vijana i1i kuwawezesha kujiajiri
  Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiairi.
  MASHARTI YA KAZI
  Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania.
  Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na picha moja ya Passport size za hivi karibuni.
  Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe namba za simu za kuaminika. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.Testmonials, Provisional Results, Statement of results HAVITAKUBALIWA.
  Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni wiki mbili baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
  Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  Katibu, Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, SLP.2483, Dar es Salaam.  AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II) (NAFASI10)
  SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo (Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Tsh: 322,460/= na kuendelea hadi Tsh: 401,880/= kwa mwezi.
  MAJUKUMU YA KAZI
  Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na M afunzo
  Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa vyama na vilabu vya michezo
  Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
  MASHARTI YA KAZI
  Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania.
  Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) pamoja na picha moja ya Passport size za hivi karibuni.
  Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe namba za simu za kuaminika. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.Testmonials, Provisional Results, Statement of results HAVITAKUBALIWA.
  Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni wiki mbili baada ya Tangazo hili kutoka gazetini kwa mara ya kwanza.
  Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  Katibu, Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, SLP.2483, Dar es Salaam.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ombeni wenye vigezo timilfu ila msishangae mkikuta nafasi zishajazwa!
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mbon sioni 'deadline' y akutuma maombi?
   
 4. M

  Mr CarryFoward Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  Mwisho ni wiki 2 toka tangazo litoke, ambayo ni jana nafikiri.
   
 5. M

  Mr CarryFoward Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  Hivyo itakuwa MAY 5, 2010
   
 6. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ninajaribu hii nami nipate ajira serikalini. lakini hiii salary hii jamani watoto watashiba kweli?
   
 7. B

  Bicha New Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante nduguyangu, Acha nichangamkie
   
 8. c

  costa Member

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida ya serikalini,kazi hadi ushikwe mkono!Tutafika?!Surely,kutangaza ni formality tuh!
   
 9. GP

  GP JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahahaah, kuna marupurupu kibao inategemea na kitengo ulicho!,
  wengine hata huo mshahara hawaugusi wanakula marupurupu mara safari, mara semina, mara warsha, mara kongamano etc!
   
 10. c

  costa Member

  #10
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fallen Tower at Bunda Town..jpg

  Hebu angalieni hiyo skendo jamani!
   
 11. b

  bwanashamba Senior Member

  #11
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ee bwana uhuu mnara wapi tena aukuua mtu
   
 12. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  inauma kuona watu wanatangaza kazi mtu alipwe laki nne. sijui watz tutaondokana lini na umasikini huu.mwezi mzima laki nne.
   
 13. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  we GP ni true hiyo ya kwamba hawagusi m-salary?
  ngoja nichangamkie mtaalam, nijaribu kupeleka kabahasha kangu ka -kaki!
   
 14. c

  costa Member

  #14
  Apr 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnara wa tigo huo! wazee wa 50 cent .....!wilayani bunda...!
   
 15. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Si bora ingekuwa laki nne kamili? hiyo TGSD ikishakatwa take home ni 258,000/= sasa kazi kwako ni akili kichwani tu.
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  So sad! Pango la yyumba ya familia ya kawaida kabisa si chini ya laki tatu (300,000) kwa mwezi. Hawa wanaishije?
   
 17. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hilo pango la nyumba sio la "Mtamzania wa kawaida" bali la "Mtanzania asiye wa kawaida". Mtanzania wa kawaida anakaa chumba cha elfu 5-7 kwa mwezi ( piga hesabu nyumba ya aina hiyo yenye vyumba vitano ni kiasi gani kwa mwezi...lesi zani fifty k!!!. Zaidi ya hapo huyu mtanzania wa kawaida lazima awe mwizi.......... (Mawazo yangu tuuuu!)
   
 18. J

  Jey New Member

  #18
  May 11, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ufisadi kwa stahili hii hautatokomea ng'oooooh!!!!! Watanzania wenzetu wanatuangamiza kwa kweli duh....! nchi inaelekea kubaya :angry:
   
 19. M

  MJM JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Halafu Muungwana anasema kama hawataki waondoke serikalini. Kweli watanzania hatuna chetu tena siasa ni uchumi.
   
 20. M

  MJM JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hizo za 5,000 - 7,000 zinapatikana wapi hapa Dar au ni huko kunakoitwa UNHABITAT maana kuna maeneo nasikia yanaitwa hivyo.
   
Loading...