Darren2019
JF-Expert Member
- Nov 23, 2019
- 1,112
- 2,379
Habari zenu wadau,
Nimejitokeza kwenye hili jukwaa kuwasilisha moja miongoni mwa kero zinazopatikana katika utumishi wa umma hasa ualimu. Kuna kipengele cha kwenda likizo ya siku 28 kwa mwaka, wanasema utapewa nauli kwa interval (yaani ukipewa awamu hii, awamu ijayo unajitegemea).
Sasa kero yangu iko wapi? Mtu hadi uambatanishe cheti cha ndoa kinahusu nini? Kwani mimi kuoa hadi niwe na cheti? Mke ambaye sijafunga naye ndoa hana matumizi?
Ok, tufanye hilo tumelipotezea, umeamua kuhesabika kama bachela, eti nauli unayotakiwa kuomba ni ya kwenda nyumbani kwenu ulipozaliwa kama ulivyojaza kwenye mkataba wa ajira, sasa najiuliza hivi na umri huu kweli likizo ni nyumbani tu?
Unaweza usinielewe, hebu chukua mfano wewe ni mwanaume umeajiriwa Mtwara na kwenu ni Mtwara ila una mke kwao ni Mbeya na wewe unapenda Mbeya na mna mpango wa kuishi Mbeya au tayari mna makazi Mbeya na ndiko mke aliko japo wewe kikazi uko Mtwara, hivyo likizo ni lazima ufunge safari ya Mtwara - Mbeya, pesa ya nauli wanakupa ya Mtwara - Mtwara, huu utaratibu uliwekwa kwa malengo gani?