Utumishi wa Umma ni kwa yeyote, sio kwa ajili ya Fulani!

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,970
45,848
Imekua nongwa pale Fulani akisitishiwa utumishi wake toka ofisi ya uma!

Ikumbukwe kwamba kila anayeshika nafasi katika ofisi ya uma, jukumu lake la kwanza mpaka mwisho ni kuhakikisha kua umma unafaidi weledi wake!

Serikali inatumia kwa mabilioni kila mwaka kusomesha wataalam katika kada mbali mbali ambao watatumika kulijenga Taifa!

Ofisi ya umma, haina mwenyewe kwamba, akikosekana yeye basi Taifa litasimama! Kilichopo tu ni kuzingatia taratibu za kibinadamu katika kubadilishana nafasi!

Hata kama mhusika atakua hajafanya kosa lolote hiyo siyo kinga ya kuondolewa katika nafasi yake, kwani kuna watanzania wengine ambao pia ni qualified na wanaweza Fanya vyema kuliko aliyekuwepo awali!

Sioni sababu ya kulalamika pale Fulani anapotoka sehemu Fulani kwani naamini kwamba kila MTU anauwezo wa kuwa Fulani, ni jambo la kupeana nafasi tu, na kama Fulani anastahili sana basi hakuna ulazima wa kupeleka wengine shule kwakua yeye yupo!

Ni ubinafsi tu wa wanadamu na kukosa busara ndiko kunakotunyima kusonga mbele kama Taifa!
 
Mkuu ndio maana huwa tunashangaa ccm kuendelea kulazimisha kubaki madarakani hata kama wananchi wamewachoka. Utashangaa wanatumia jeshi na tume ya uchaguzi kuhakikisha wanabaki madarakani, kumbe ni suala la kutokuwa na nongwa tu kwamba ukichokwa toka achia wengine sio lazima kulamisha wakati umeishiwa mbinu.
 
Mkuu umezungumzia mambo mengi sana na mazito bila kua na ushahidi wowote, sio afya kwa mjadala kutoa tuhuma zisizo na ukweli wowote!
 
hapo nilipohighlight,niaje mkuu...?
 
Mkuu ndio maana huwa tunashangaa ccm kuendelea kulazimisha kubaki madarakani hata kama wananchi wamewachoka. Utashangaa wanatumia jeshi na tume ya uchaguzi kuhakikisha wanabaki madarakani, kumbe ni suala la kutokuwa na nongwa tu kwamba ukichokwa toka achia wengine sio lazima kulamisha wakati umeishiwa mbinu.
Hili jiwe limerushwa gizani pole yao waliokutana nalo.Heri ya mwaka mpya.
 
Mkuu nifafanulie inakuwaje mtu akiwa na sifa zinazostahili then hakuna haja ya kusomesha wengine ?
Ahaa, maana yangu ni kua, kuna faida gani ya kuingia gharama kusomesha watu wengine kwa maelfu ilhali tayari yupo anayefit katika nafasi husika? Kwanini tusitumie hizo fedha kwa mambo mengine na kumwacha yeye aendelee kushika nafasi hiyo mpaka afe?? Point is hakuna mtu aliyemkamilifu inapokuja katika utendaji na yeyote anaweza tumika mradi anatimiza vigezo vya msingi!

Swala la utumishi wa umma ni kwa yeyote anayetimiza vigezo! Hivyo ukiondolewa ni katika kupokezana tu ili kuboresha utendaji ili kufikia lengo kuu la kuleta maendeleo and not otherwise!
 
Mkuu ndio maana huwa tunashangaa ccm kuendelea kulazimisha kubaki madarakani hata kama wananchi wamewachoka. Utashangaa wanatumia jeshi na tume ya uchaguzi kuhakikisha wanabaki madarakani, kumbe ni suala la kutokuwa na nongwa tu kwamba ukichokwa toka achia wengine sio lazima kulamisha wakati umeishiwa mbinu.
Naona umetoka nje ya mada;

Ninacho zungumzia hapa ni utumishi wa uma usiohusisha wanasiasa! Huko kwingine ni jambo jingine linalohitaji mjadala wake tofauti na huu!
 
Ahaa, maana yangu ni kua, kuna faida gani ya kuingia gharama kusomesha watu wengine kwa maelfu ilhali tayari yupo anayefit katika nafasi husika? Kwanini tusitumie hizo fedha kwa mambo mengine na kumwacha yeye aendelee kushika nafasi hiyo mpaka afe?? Point is hakuna mtu aliyemkamilifu inapokuja katika utendaji na yeyote anaweza tumika mradi anatimiza vigezo vya msingi!

Swala la utumishi wa umma ni kwa yeyote anayetimiza vigezo! Hivyo ukiondolewa ni katika kupokezana tu ili kuboresha utendaji ili kufikia lengo kuu la kuleta maendeleo and not otherwise!

mmmnh mkuu,sasa hao walioshikilia hizo position wakivurunda,utawapata wapi watu wengine wa kureplace kama utakuwa hujasomesha wengine?

usiposomesha wengine means,mtu akiwa incompetent ataendelea kuishikilia position as hakuna wa kumreplace,.............somesha,mtu akijua kuna watu wenye weledi kama yeye ambao hawana kazi atafanya kazi kwa bidii,lol

Mkuu hii sio sawa,
 
Mkuu naona tunazungumzia jambo lile lile ila katika lugha tofauti!
 
Ahaa, maana yangu ni kua, kuna faida gani ya kuingia gharama kusomesha watu wengine kwa maelfu ilhali tayari yupo anayefit katika nafasi husika? Kwanini tusitumie hizo fedha kwa mambo mengine na kumwacha yeye aendelee kushika nafasi hiyo mpaka afe?? Point is hakuna mtu aliyemkamilifu inapokuja katika utendaji na yeyote anaweza tumika mradi anatimiza vigezo vya msingi!

Swala la utumishi wa umma ni kwa yeyote anayetimiza vigezo! Hivyo ukiondolewa ni katika kupokezana tu ili kuboresha utendaji ili kufikia lengo kuu la kuleta maendeleo and not otherwise!
Kwa mawazo yako haya unajiaibisha.
Unadhihirisha kuwa wewe ni kiazi mbataya
 
Mkuu naona tunazungumzia jambo lile lile ila katika lugha tofauti!

Wewe unasema watu wasisomeshwe kama yupo mmoja mwenye sifa,mie nasema wengi wasomeshwe,ili hao walioshikilia position na sifa mbali mbali,wasiperform vibaya,wakijua watakua replaced anytime.tuna mitazamo tofauti,ila sometimes kujieleza mie ni janga,lol.so happy new year.lol
 
Naona umetoka nje ya mada;

Ninacho zungumzia hapa ni utumishi wa uma usiohusisha wanasiasa! Huko kwingine ni jambo jingine linalohitaji mjadala wake tofauti na huu!

Unatofautishaje watumishi wa umma na wanasiasa wakati wanasiasa ndio wenye maamuzi kwa watumishi wa umma? Kwanini wanasiasa kwako huoni kama wanapaswa kubwana na hili wazo lako bali watumishi wa umma tu?
 
Mkuu umezungumzia mambo mengi sana na mazito bila kua na ushahidi wowote, sio afya kwa mjadala kutoa tuhuma zisizo na ukweli wowote!

unaitwa stroke? mmh sio jina zuri kujipa natumai halina uhalisia na namna ulivyo.maelezo yako yamejikita kutetea chama cha makupe(CCM) ambacho kinawasulubu makabwela na kuzidi kujineemesha.Wananona huku watawaliwa wakikondeana,kupauka na kutoa harufu ya kuudhi kwenye kwapa zao.stroke upo?2020 unajua nn kitatukia?
 
Unatofautishaje watumishi wa umma na wanasiasa wakati wanasiasa ndio wenye maamuzi kwa watumishi wa umma? Kwanini wanasiasa kwako huoni kama wanapaswa kubwana na hili wazo lako bali watumishi wa umma tu?
Tofauti ya wanasiasa na hao wengine IPO mkuu, kwakua mwanasiasa anachaguliwa na watu wengi kwa kura, ila hao wengine either wanaajiriwa au wanateuliwa (appointments) ingawa huyo wa awali ndiye anayekuja kusimamia wengine kutokana na taratibu tulizojiwekea kisheria!

Kwamba hao wanasiasa wabanwe, wenye maamuzi ya kuwaweka walipo ni wananchi kupitia uchaguzi mbali mbali! Wananchi wakiamua wameamua!
 
unaitwa stroke? mmh sio jina zuri kujipa natumai halina uhalisia na namna ulivyo.maelezo yako yamejikita kutetea chama cha makupe(CCM) ambacho kinawasulubu makabwela na kuzidi kujineemesha.Wananona huku watawaliwa wakikondeana,kupauka na kutoa harufu ya kuudhi kwenye kwapa zao.stroke upo?2020 unajua nn kitatukia?
Siyo kazi yangu kujua kitakachotokea 2020; Mimi nayajua ya jana na Leo tu, anayejua hayo ni Mungu pekee! Mimi na wewe hatuna uwezo huo!
 
Back
Top Bottom