Utumishi wa umma Bongoland ni job security au poverty security?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kuna hii kasumba kuwa utumishi wa umma Bongo faida yake kubwa ni pamoja na job security ukilinganisha na private sector.

Lakini kiuhaliasi ni job security au poverty security?

Kama mtu anapata promotion baada ya miaka 7 au zaidi badala ya 3, na malimbikizo yaliyotokana na kucheleweshewa mshahara mpya tangu akabidhiwe barua ya promotion nayo kuchukia miaka kulipwa, je utumishi huu sio poverty security?

Iwapi thamani ya mtumishi wa umma wa Bongoland?

Kitu Kingine, pitia salary slip zao uone zilivyojaa makato ndio utakumbuka ile kauli ya watu kuishi kwa mbinu!

Hakika ndio maana Bongo ni moja ya Taifa la watu wasio na furaha katika hii sayari na sijui kama kuna siku watatoka katika hilo kundi.

Wabongo kama watoto yatima ndani ya nchi yao!!

Nina mpango wa kuandika kitabu kuhusu maisha ya mtumishi wa umma wa Bongoland labda mabwana wakubwa wakikisoma watajiongeza kusaidi kundi hili linaloonekana kusahaulika.
 
Kazi nzuri Tanzania ni siasa tu.

We fikiria kibajaji std VII anaongoea hewa na matusi tu bungeni, lakini anacholipwa ni mshahara wa watumishi wataalam zaidi ya watano.
 
Awamu hii imekuwa ngumu na chungu mno kwa watumishi wa umma. Kuna watu wana roho mbaya sana, na ndio wanaoishi miaka mingi.
 
Back
Top Bottom