Utumishi (PSRS) katika hili la usaili wa TRA mnainajisi Ofisi ya Rais

Retizinga

Member
Aug 7, 2016
89
70
Waswahili wanasema kukiri kosa sio udhaifu ni namna ya kujiimairisha na kuweka misingi bora ya kulizuia lisitoke lakini hali ni tofauti kwa taasisi hii ya umma iliopo chini ya ofisi ya Rais baada ya mitihani kuvuja wameweka pamba masikioni kwa kiburi kikuu wanadai hakuna mitihani uliovuja.

Inauma sana kuona hili likifanyika na usahihishaji ukiendelea, kwa mwenendo huu mnataka kutuamisha maelfu ya vijana wasomi tusio na ajira kwamba mpo kwa ajili ya kundi Fulani la watu tumieni busara na si mabavu usaili urudiwe ili watakaopata wawe wamepata kihali hizo kazi.

Pia jukumu la kutafuta ushaidi na kujiridhisha kuwa mtihani ulivuja na kuchukua hatua ni lenu msilikwepe mkatutega kwa kudai kuwa mpaka tuwalete ushaidi wa moja kwa moja ofisin kwenu.

Mwisho nitoe wito kwa waathiriwa wote wa hii dhuluma na waathiriwa na watarajiwa yaani wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa tayari kuchukua hatua madhubuti ili kukomesha ufedhuri na dhuluma zinazofanyika na chombo hiki cha umma kwa kutoa ajira kwa kujuanaa na rushwaaa bora kupotea kuliko kuishi kama watumwa kwenye nchi yetu.
 
Hatuzungumzi idadi ya nafasi kuwa ngapi na kuitwa wangapi tunazungumzia mtihani kuvuja tena dhahiri shairi alafu taasisi usika kuziba masiko ni kweli ukosefu WA ajira ni janga la ulimwengu hasa nchi zetu zinazoendelea lakin hata hicho kidogo kilichopo kismamiwe kwa haki inayestaili pata apate sio mtihani unavuja kwa uwazi kiasi Hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa.
Dogo nafasi 8 usaili mkaitwa 10,000 hapo uwezekano wa wewe kupata hiyo kazi ni 8/10,000 hata kama paper lisingevuja.

Fanya mambo mengine.
 
Angalia list ya majina walioenda oral majina ya wazazi wao a.k.a ubini wao utajua ni kwanini oral lazima iendelee no matter what.

Tu ya wanyonge ndio hio mzee.
 
Pole San Siku nyingine ukiona tangazo la tasisi kubwa kubwa usiombe wala kupoteza nauli ngojea za halmashuri
Ndugu hata hizo za halmashauri siku hizi kwa watoto wa masikini ni probability kupata,kipindi naelekea kumaliza masomo yangu ya chuo nikiwa discussion nyumbani kwao rafiki angu watu wa kipato cha kati nilimsikia mzee wa ile familia akimwambia rafiki angu "INABIDI MFUNGE MKANDA KITAKACHOPATIKANA MRIDHIKE NACHO NIMEAMUA DADA YENU ATOKE SAFARI HII" ilibid baadae nimuulize rafiki Angu kauli hii ya Mzee ilikuwa na maana gani?

Alijibu kwa kuniambia sister kakaa mtaani mwaka wa tatu hana ajira Mzee kuna mtu wa utumishi kaongea nae kampa million 5 ili amsaidie dada kupata kazi ambapo kwa kiwango hicho cha pesa hata kama atafeli usaili wa written atakuja pachikwa kwa data base,kweli haikupita muda kuna usaili wa halmshauri fulan ulifanyika kulingana na uwezo mdogo wa yule binti hakufanikiwa pita hatua ya mchujo lakin baada ya miezi michache jina lilitoka kapangiwa halmashauri fulani kazi na hili familia walijua wiki kadhaaa nyuma

Tunaposema utumishi haipo kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa fukara tuna mifano mingi iliyo hai sema safari hii ili la TRA it will be our case study
 
Kwani si walitoa Tangazo!!!??
TANGAZO LA KUAHIRISHA USAILI WA TRA ULIOTAKIWA KUFANYIKA TAREHE 23-26 AGOSTI, 2021
Aug 09, 2021
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawajulisha waombaji kazi ambao walifanya usaili wa mchujo tarehe 07 Agosti, 2021 kwa nafasi za “Tax Management Officer II”, “Customs Officer II”, “Tax Management Assistant II” na “Customs Assistant II” kuwa usaili uliopangwa kufanyika tarehe 25-26 Agosti, 2021 umeahirishwa. Aidha, usaili wa kada ya “Personal Secretary II” uliopangwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2021 umeahirishwa pia. Taarifa zaidi zitatolewa kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi Umma

09 Agosti, 2021
 
NATAKA NIWAAMBIE UKWELI WADOGO ZANGU...serikalini ajira zipo tena nyingi sana shida ipo kwa hao waliopo serikalini kwanza kabisa wengi wao wameajiriwa wakiwa na qualification ndogo sana,na pili wengi wao hawajiamini katika utendaji wao wa kazi hasa hao wazee mnaowaona maofisini...niwaambie tu ni ngumu kwa kijana mwenye shahada moja au mbili kupata nafasi sehemu hizo bila kushikwa mkono (konekshen) wengi wao wanataka mtu wanaemjua ili kuendelea kujihakikishia nafasi zao na vyeo vyao maofisini.....
 
Ndugu hata hizo za halmashauri siku hizi kwa watoto wa masikini ni probability kupata,kipindi naelekea kumaliza masomo yangu ya chuo nikiwa discussion nyumbani kwao rafiki angu watu wa kipato cha kati nilimsikia mzee wa ile familia akimwambia rafiki angu "INABIDI MFUNGE MKANDA KITAKACHOPATIKANA MRIDHIKE NACHO NIMEAMUA DADA YENU ATOKE SAFARI HII" ilibid baadae nimuulize rafiki Angu kauli hii ya Mzee ilikuwa na maana gani....
Nimempenda sana huyo mzee yupo responsible na familia yake japo hali tete! Ila kazi kaitafuta na kainunua kwa ajili ya mwanae
 
NATAKA NIWAAMBIE UKWELI WADOGO ZANGU...serikalini ajira zipo tena nyingi sana shida ipo kwa hao waliopo serikalini kwanza kabisa wengi wao wameajiriwa wakiwa na qualification ndogo sana....
😂😂😂😂😂😂😂 mizee imekamata nafasi na haitaki kuachia ngazi hata kwa ndumba wao wanakomaa tu
 
Waswahili wanasema kukiri kosa sio udhaifuni ni namna ya kujiimairisha na kuweka misingi bora ya kulizuia lisitoke lakini hali ni tofauti kwa taasisi hii ya umma iliopo chini ya ofisi ya Rais baada...
Kurudiwa hilo sahau! Watu wamelipia kazi hizo utumishi halafu nyie mnataka kuleta mambo ya kijinga! We unafikiri hao akina Kabudi na Lubuva hawajatoa chochote kitu kuhakikisha michongo hio watoto wao wanapata?

Kama huna connection atleast hakikisha una pesa basi.
 
Kurudiwa hilo sahau! Watu wamelipia kazi hizo utumishi halafu nyie mnataka kuleta mambo ya kijinga! We unafikiri hao akina Kabudi na Lubuva hawajatoa chochote kitu kuhakikisha michongo hio watoto wao wanapata?

Kama huna connection atleast hakikisha una pesa basi.
Mkono mtupu haulambwi
 
Back
Top Bottom