Utumishi mmefunika kombe? Kwanini Watumishi wa ajira 2014 - 2017 wawekwe daraja moja?

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Mnachokifanya sasa sio sawa kuwaweka ajira 2014, 2015, 2016, 2017 kwenye daraja moja bila kuangalia umri kazini. Mnachokifanya sasa ni kusahau miaka watumishi waliopotezewa kwenye masuala ya uhakiki na vyeti feki. Pia kuna ajira 2012 na 2013 walikaa miaka 6 bila kupanda kwa sababu za kilichoitwa uhakiki.

NINI KIFANYIKE?
Ili kusawazisha hili, inatakiwa muhesabu miaka ya mtumishi tangu aajiriwe na daraja ambalo angetakiwa awepo kisha mumuweke hapo.

Mfano: Ajira 2012, 2013 wenye degree sasa wanatakiwa wawe TGS F etc.

Ila hiki mnachokifanya sasa ni sawa na kufunika kombe ili mradi mambo yaende. Je hawa waliopoteza miaka 2, 3, 4 kupisha uhakiki wanafidiwa vipi?

Cc: Waziri - Utumishi
Cc: Katibu Mkuu Kiongozi
Cc: Rais JMT
 
Kwani utekelezaji wa hayo madaraja lini?
Lini wanabadilishiwa salaries zao?
 
Hili ni kosa kubwa, na wakipitisha hivi Bomu litakuja kulipuka.

Haiwezekani hao wa 2012/2013 wawekwe sawa na wa 2014/2016 huku
 
Kiongozi tuchape kazi nnchi yetu sote tukiona utumishi mgum tuwe wanasiasa
 
Kuna watu watajua hawajui na wataelewa hawaelewi.
Wanapingana na sheria za kazi. Hao wanaozuiya maslahi ya wenzao tuwaombee. Watanzania wanajua kuomba na Mungu anawajibu
 
Luna watu watajua hawajui na wataelewa hawaelewi.
Wanapingana na sheria za kazi. Hao wanaozuiya maslahi ya wenzao tuwaombee. Watanzania wanajua kuomba na Mungu anawajibu
Kama vile rais akiondoka anaondoka na wizara yake ya utumishi sijui kwanini hakuna muendelezo kati ya awamu na awamu
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom